Je, kweli ni ngumu kuishi na mwanaume aliyewahi kuoa?

Je, kweli ni ngumu kuishi na mwanaume aliyewahi kuoa?

@
Asante kuniita Aaliyyah, nadhani hili linajibiwa vizuri na wanawake..wale waliopitia huu uzoefu.

Ila naweza kusema tu huenda hao wanaume wanakuwa na ile tabia ya kulinganisha, kwamba wewe sio bora kama ex wife, una madhaifu mengi ni bora yule wa kwanza, labda uchafu, huwezi kupika vizuri, hunipi kipapa vile nataka, una mdomo nk. Huwa kuna tabia ya kulinganisha...ni mawazo tu, sina uzoefu!
Asante mkuu kwa mchango wako
Kma ni hivo bas Kuna shida kubwa
 
Mama yangu alikuwa ananiambia hivyo, nilikuwa msichana mdogo, sikuwahi ku hoji Sana sababu ni zipi?
Lakini nilimsikiliza na kufuata maneno yake, na namshukuru Sana.

Kutakuwa kuna sababu labda mawasiliano, comparisons za mke wa Kwanza na wa pili, majukumu etc
 
Natumaini mkopoa?
Katika piatapita zangu nikakutana na mada Kwamba mwanamke kama hujawahi kuolewa bas usikubali kuolewa na mtu ambae alishawahi kuoa ama Kuishi na mwanamke Yani hata wale waliowahi Kuishi pamoja bila ndoa

Rafikiyangu ameolewa na mwanaume wa aina hiyo ambae alishakuwa na mume na ana watoto before hajamuoa

Katika mazungumzo yetu mara nyingi Huwa anasema ni ngumu Kuishi na mwanaume aliewahi kuoa ikiwa mwanamke pia hukuwah kuolewa

Mara ya pili akarudia neno hilo Hilo
Sikutaka kuhoji sana sababu nilishasikia mahali nimeona niliweke hapa Kwa wataalamu na watu wenye uzoefu

Je ni kweli Kuishi na mwanaume aliewahi kuoa au Kuishi na mwanamke ni changamoto?
Huwa wapoje Hawa watu ambao ndoa zao za mwanzo zimevunjika
Si ngumu kuishi, msingi wa mahusiano yao nu upi, hiko ndicho kitawabeba au kitawaangusha
 
@

Asante mkuu kwa mchango wako
Kma ni hivo bas Kuna shida kubwa
Ndio maana wanasisitiza, "Marry your first", unakuwa na uzoefu wa mtu mmoja, huna wa kulinganisha nae, hujui wengine wanafananaje.

Ila sisi tunaonjana sana, ukija kukutana na mume/mke lazima tu utalinganisha, utafananisha tu...mbona huyu anaongea sana, mbona mchafu, mbona ana tabia hizi...bora wa mwanzo, alikuwa mzuri zaidi kwenye eneo fulani...

Ni ngumu sana kusahau hasa ukikutana na kitu hukutegemea(in a negative way). Ila akija anayejulia mambo....aaah raha tu!!

Halafu kingine, tunaoa/tunaolewa na watu tusiowapenda, mtu anaingia kwenye ndoa kwa sababu fulani ila sio kwa vile amempenda mwenza wake.
 
Miss Aaliyyah mambo ?

Kwanza sina experience na hili jambo lakini nakuahidi kulifanyia utafiti ili nipate uhakika. Halafu nitaweka mrejesho.
Ukiwa mwanamke bwana ni Raha tu .
Sasa dada kaleta swali badala utoe mawazo yako ila umejipa kazi kwenda kufanya utafiti alafu ulete mrejesho ila ningekuwa ni Mimi nimeuliza vipi jamani wanume wenzangu ni kweli nikiwa bahili nitakuwa tajiri ungenipa jibu la mkato ,Mara utajua wewe .

Aisee wanawake waheshimiwe tu .
 
Anhaa kum
Mwanaume tuliowahi kuoa sasa ni rasmi tumeanza kunyanyasika humu😂😂😂😅
😀😀 Kumbe na wewe umewahi kuoa ?
Dah ni kweli naona ni kazi kweli maana hata Mimi hata nikipata demu yeyote lazima nianze kumfananisha na mke wangu wa zamani hasa usafi ,kauli nzuri ni hapo najikuta naachana na wengi sababu nilishamzoea yule kitabia na kisosholojia inakuwa ngumu kukubali tabia mpya za mdada mwingine .
Ila najipa Imani nitafanikiwa kufit kwenye life la mtoto wa mtu ,few days
 
Kuna mwamba hajawahi kuoa ila kukaa na mwanamke miezi 8 , 6 ....mara mwaka mara miezi 3 kawaida baada ya hapo wanatimuana.

Sijui kuoa ni mpaka cheti Cha ndoa na harusi na Pete au huyu anakua kundi Gani......

Mimi naona watu wengi wameoana siku hizi sema informal.
 
Kivip mkuu sijaelewa kwenye msingi wa mahusiano hapo
Mwanaume alietoka kuoa anakuwa amebeba experience (bad or good), so vitu vingi vitakuwa si vipya kwake, now wameanzaje mahusiano yao hapo ndipo msingi wa yote. Walianza kwa upendo, mwanaume / mwanamke alipenda kweli, au it was random attachment?
Kama hakukuwa na upendo but sense of majukumu ndio viliwakutanisha ndivyo watakavyo chukuliana wakiishi pamoja

Wakichukiliana kwa mapenz, wataenda hivyo hivyo ila kama walichukuliana kwa majukumu ndivyo vitavyo wakuta
 
Back
Top Bottom