Internet ni mahitaji muhimu la binadamu wa sasa, sio anasa wala matumizi mabaya! Internet ni kama maji, unatakiwa uwe nayo 24/7.
Watu wa corporate world wananielewa, siku hizi kuna Internet banking, huna haja ya kupeleka hundi benki, huna haja ya kupanga foleni kuchukua bank statement, kufanya malipo, kupokea malipo n.k, e-documents etc. Siku hizi watu hawatembei na kalamu mfuko wa shati kusaini documents au kuziandaa.
Mashambani kuna weather forecast apps, unapata taarifa na mienendo ukiwa umelala.
Vilingeni huko kuna CCTV cameras zimeungwa na Internet, ukiamka unacheki vilinge vimelalaje, mpaka panya unawaona!
Kuna tajiri mmoja ana gari kibao za mizigo, zimefungwa camera za mitandao, kazi yake yeye ni kuangalia magari yapo wapi kila akiamka, na dereva alisimama wapi, akafanya nini? 😁
Mzungu mchawi na uchawi wake ni Internet. 😁