Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?

Hajakosea... Kumbe....?

Yaani kusema lazima tupate huyu... Na sio Mama kama katiba inavyosema unasema porojo?
Lakini jamaa, ngoja inakujaaa kwa mbali.... Lakini si pekee. Pia Makonda japo hakuwa na tiketi yoyote alikuwa anahaha kwa team walioshikilia, mana matumaini ndio yaleee....
Tupo pamoja. Na huyu balozi kimaneno vipi, alikuepo?
 
Lakini jamaa, ngoja inakujaaa kwa mbali.... Lakini si pekee. Pia Makonda japo hakuwa na tiketi yoyote alikuwa anahaha kwa team walioshikilia, mana matumaini ndio yaleee....
Tupo pamoja. Na huyu balozi kimaneno vipi, alikuepo?
Wote walikuwepo kuleta figisu
 
Labda bado walikuwa wanajadiliana na ku debate wenyewe kama ni kweli hawanaye tena kwa hofu kubwa anaweza kuibuka tena ikawa kizungumkuti, bwana yule alikuwa anatisha[emoji16]
Askofu Rashid aliwaongopea.kuwa hayo ndiyo maeneo yake ya kujidai hivyo wapige kimya kwani angemfufua.
 
Nchi yetu haijawai kutokewa na tukio kama hili ,shida ilikua kwenye mrithi unadhani kwa Nguvu zile za Hayati watu wake wangekubali kirahisi kuacha asali ile ?
Kikubwa nadhani ni St Peters walikua wanaweka mambo sawa ili baadae kusiwe na Conflicts na kweli Wazalendo walishinda vita ile
 
Uliyoyaeleza siyo sahihi, japo hupo mbali na ukweli.

1) Kuhusu Nyerere, madaktari wanajua, kuna mahali fulani binadamu mgonjwa akifikia, huwezi ku-reverse. Kipimo kimoja kikubwa ni uwezo wa ubongo. Mwalimu Nyerere alifikia mahali ambapo uhai wake ulishikiliwa na machines za ICU. Baada ya kutoonekana dalili za kuurejea uhai, waliamua kupima uwezo wa ubongo. Ndipo ilipoonekana kuwa ubongo upo katika kiwango ambacho hawezi kuishi tena. Mawasiliano yakafanywa na familia na Serikali, ndipo maabdalizi ya msiba yakaanza. Na siku iliyokubaliwa zikaondolewa machine. Kwa hiyo alifariki siku ilipotangazwa.

2) Christmas, ifahamike hakukuwepo na utunzaji wa kumbukumbu za tarehe nyakati hizo, na mfumo wa kuhesabu miezi na tarehe ulikuwa tofauti na sasa. Kwa hiyo kilichofanyika ni kujitahidi kuwa katika kipindi alichozaliwa, lakini bila ya kuwa na uhakika wa siku. Inajulikana nyakati ilipofanyika sensa, inafahamika kipindi ambacho wachungaji walikuwa wakipeleka kondoo maeneo hayo aliyozaliwa Kristo Yesu, inafahamika watoto wa kiume walipouawa kwa mamlaka ya Herold. Matukio haya yalisaidia kujua nyakati ambazo Yesu alizaliwa.

3) Kuhusu Magufuli, siyo kwamba tarehe kamili haifahamiki, siyo kwamba alikuwa kwenye uhai wa kushikiliwa na machine, na hivyo alifariki siku walipoondoa machine. Ukweli ni kwamba alifariki, lakini wenye mamlaka wakaamua kukaa kimya, na kuamua kutangaza siku waliyotaka wao. Kama ni kuandaa mazingira, bado walikuwa na uwezo wa kutoa tangazo tarehe 17, lakini wangeeleza tarehe kamili aliyoaga dunia. Kwa kweli sikuona umuhimu wa kudanganya tarehe ya kifo chake.

Lakini vyovyote iwavyo, haibadilishi chochote, japo inafahamika kuwa wananchi wana haki ya kupewa taarifa sahihi.
 
Yote matatu umejaribu kuyatetea lakini haijalishi. Wote hao ni binaadam kama sisi na mwisho wetu ukifika umefika, itangazwe isitangazwe ni faida na matakwa ya wanaoamua, kwangu its all the same. Hainiumizi kichwa.
 
naomba siku ukiandika huo uzi unitag na mimi.
 
Hivi hata hao waliondele na ratiba walikuwa hawaehtuki... Hadi mwingine akajirhalilisha eti jamaa yupo anapiga mzigo! Kwa tukio, lile. Inadhihirisha kuwa wasaidizi wawili wale ni ceremonial au Wakati ule wa giza..
Walikuwa ceremonials!
Sitaki kuamini kama walikuwa hawajui.
Facial expression zao hazikuwa na nuru.

Kuna wakati No2. akiwa kwenye mkutano wake wa mwisho na usiku wake kutangazwa taarifa yenye simanzi alitamka maneno yenye ukakasi, ingawa baadaye alirekebisha lakini GT walishaelewa kitu

Aliwaambia wasaidizi wake wawili kwamba wasipofanya vizuri watakuwa wateja wake, baadaye alibadili na kusema 'mtakiwa wateja wetu mimi na.......
 
Japo miaka inaendelea kupita bila ukweli halisi kuwekwa bayana, this is the day na kuna siku itafika ukweli huu utawekwa bayana!, swali tunalojiuliza bila majibu, ni walikuwa wanafanya nini na huo... kwa siku 5 nzima mpaka tulipojulishwa?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…