Je, maamuzi ya Rais Samia ni State Capture?

Umelete hoja nzuri... Tatizo ni uelewa wala si maandamano. Waelewesheni watu waelewe kwanini mnataka waandamane...
Kingine jipambanueni ili wananchi wawaelewe vizuri!
Ninaposema wananchi namaanisha wale wa vijijini!
 
Kwahiyo before Magufuli CCM Ilikua inashinda uchaguzi?

Walikuwa wanaiba kura sio kupora mchakato. Walikuwa na afadhali, na kadiri siku zilivyokuwa zinaenda walikuwa wanazidi kupoteza majimbo yao. Magufuli kwa kiburi cha madaraka na kupenda sifa, akaamua kupora mchakato kinyume kabisa na uhalisia wa umma.
 
Hoja ya mcng ni ccm walikua wanaiba kura. Jitaidi kupambana na mfumo mzima wa ccm na sio Magufuli tu.Mabadiliko hayawezi kuja kwa nyinyi kupambana na marehemu.
 
Nipe nauli mkuu niende kwenye hilo kaburi nikaondoe chuki. Hapa naweka msisitizo ili isitokee kiongozi muovu kama yule kupata tena nafasi ya kuongoza nchi hii.
 
Hoja ya mcng ni ccm walikua wanaiba kura. Jitaidi kupambana na mfumo mzima wa ccm na sio Magufuli tu.Mabadiliko hayawezi kuja kwa nyinyi kupambana na marehemu.

Mapambano na mfumo hayajawahi kusimama, bali yeye aligeuka akawa zaidi ya tatizo la mfumo, na sasa ameotesha mbegu mbaya kabisa ya kunajisi uchaguzi. Kwa sasa ni ngumu mno kurudisha imani ya wapiga kura, ni hadi kufanyike jitihada za dhahiri za kuondoa mifumo hii dhaifu ya uchaguzi, nayo ni kupatikana katiba mpya. Kinyume na hapo wapiga kura hawataweza kufika hata 5m nchi nzima.
 
Nipe nauli mkuu niende kwenye hilo kaburi nikaondoe chuki. Hapa naweka msisitizo ili isitokee kiongozi muovu kama yule kupata tena nafasi ya kuongoza nchi hii.
Ni kweli unaweka msisitizo, lkn Yule alishakufa, umekuwa na chuki mno, yaani uki argue nawana CCM yyte unayemuongelea muda wote ni Magufuli, kuna wengine walisha choka na Hilo jina la Marehemu mkuu wangu, yaani ni kma vile anakutesa Sana jaribu kuangalia michango yako Kwa siku unamtaja huyo meenda zake mara ngapi, Je, kuna siku inapita hujamtaja? Punguza stress Kwa mtu ambye Hana effect tena. Kumtaja taja every hoja ni kma unamwinua.
Samahani kma ntakuwa nimekukosea mkuu wangu, kma ujuavyo siku zote wewe ni kiongozi wangu.
 
Na ile ya Magufuli ya kuteua watoto wa Dada zake, wajomba na mabinamu zake, kabila lake na ukanda wake kwenye nafasi mbalimbali nyeti unaiitaje?
 
Dhalimu mwendazake ataendelea kutajwa sana tu na kamwe hatutaacha kumtaja kwa udhalimu wake usio na mfano dhidi ya Watanzania hadi vitukuu wetu nao waijue hiyo jehanum tuliyopitia na aliyetupitisha huko.
Sijaongea na wewe wala kukutaja, naongea na GT wangu ninayemwamini, we huna effect yyte naongea na mpambanaji kindaki ndaki!
 
Hatuwezi kupowa kuanika UFEDHULI alioufanya huyo mungu wenu wa Chato kwa Watanzania. Zitto kabwe alisema last two weeks na Mwingira kasema juzi. Hatupoi mpaka dunia nzima ijuwe kuwa tulikuwa kwenye himaya ya shetani kwa mwaka 2015-20.

Wewe G4rpolitics Fanya yako kwanza hatuombi bando kwako, na muda ni wakwetu. Mbona nyinyi mkimsifu hatuwaingilii? Kila mtu ashinde mechi zake
 
Sijaongea na wewe wala kukutaja, naongea na GT wangu ninayemwamini, we huna effect yyte naongea na mpambanaji kindaki ndaki!
Ukimtetea Mwendazake wewe ni adui wa utawala Bora na demokrasia. Tutakushambulia bila kujali unajibizana na nani. Misukule wakubwa nyie
 
Sijaku quote narudia naongea na GTs only.kama Una Imani na Mwingira nenda kanisani kwake.
 
Lakini Katiba Mpya ninayotaka itoke kwa wananchi na si wanasiasa na wabunge!!
Ina maana ile iliyopitishwa na bunge la katiba inayosubiri kura tu ya raia (siku Ccm wakipenda) huitaki.
 
Ukimtetea Mwendazake wewe ni adui wa utawala Bora na demokrasia. Tutakushambulia bila kujali unajibizana na nani. Misukule wakubwa nyie
Ndiyo maana nikasema naongea na GTs only Ona sasa, unaongelea Mimi kutetea, soma nilicho kiongelea na nioneshe wapi nilipomtetea, misimamo yngu ya kisiasa huijui hivyo usitake kuni force.
 
Mkuu kwa taarifa yako kwa udhalimu alioufanya ni kama vile ninamtaja mara chache kwa siku. Inapaswa nimtaje sana ili nimuinue kama unavyosema. Alipokuwa hai hakuruhusu kusemwa, acha tumseme sasa. Nyerere amekufa muda mrefu kuliko yeye, mbona bado tunamtaja? Kama ni kukwazika inabidi nikuombe msamaha ww, maana ndio unakonda kwa kusikia tukianika ufedhuli wake.
 
Na ile ya Magufuli ya kuteua watoto wa Dada zake, wajomba na mabinamu zake, kabila lake na ukanda wake kwenye nafasi mbalimbali nyeti unaiitaje?
Naona hunielewi. Nafikiri wewe ni mmoja wa wafaidika. Two WRONGS don't make a RIGHT!!!!
 
Walishajihakikishia ulinzi wa vyombo vya dola kwa hiyo wanafanya vyovyote watakavyo.......
 
Watu gani!?? Watanzania hawa hawa!!? Una utani siyo bure???
 
JPM alichowaonyesha wahuni ni kuwa ukitumia dola vizuri ,hakuna mtu wa kukufanya lolote,,,, ss yy kapumzika jiandaeni kufanyiwa vitu vya ajabu mbele ya macho yenu ,na hamtafanya lolote zaidi ya kulalama in anonymity🙂🙂
 
Awamu ya nne imerudi kwa mlango wa nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…