Je, mama analikimbia kundi lililompigania kuhakikisha anakikalia kiti? Kwann?

Je, mama analikimbia kundi lililompigania kuhakikisha anakikalia kiti? Kwann?

Swali la kujiuliza ni je, mama analikimbia kundi lililompigania? Kwann?
Kukujibu tu na siasa zakonza Uhasama uhasama, ni Hivi

SSH kama Amri Jeshi, hahitaji kukimbilia au kujificha kwenye kundi lelote lile and especially lililojaa mawakala na vibaraka wa Nje, haswa hilo unalodai, lilimpigania.

Anahitaji kuwepo nyuma ya Watanzania wanaohitaji ulinzi wakati wanapohitaji ulinzi wa Rasilimali zao.

Wacha kuendekeza Ukoloni mamboleo.
 
Naamini nyuma ya mama kuna watu wazito hasa wa kimkakati walioamua kuyaua haya makundi mawili msoga na sukuma gang.

Mama anaenda kuyazika haya makundi rasmi. Namaanisha hivi haya makundi yanaenda kufa.Mbinu inayotumika pamoja na akili ni za hali ya juu mno! Naona kuna ujasusi humu!
Mbinu inayotumika siyo nzuri. Kwasabb kama lengo ni kuyaua makundi basi kuzodoana na kukashifiana kulipaswa kuepukwa.

Anachokifanya Makonda ni kuibomoq ule upande wa Samia gang na kuutukuza upande wa sukuma gang.
 
Anachokifanya Makonda ni kuibomoq ule upande wa Samia gang na kuutukuza upande wa sukuma gang.
Mbinu inayotumika ni kuwagombanisha kisha wapotee, ukiangalia tayari dalili zimeanza kujionyesha! Nahisi deep state imeamua taifa kwanza makundi baadae!

Raisi mteule hatatoka katika makundi haya! Samia hana makundi bali anatumika kuyaua haya makundi kwani ni hatari kwa mustakabali mzima wa taifa!

Mbinu inayotumika ni ya kijasusi! Unatakiwe ufahamu kuwa kuna TISS ndani ya TISS! Namaanisha hivi kuna usalama ndani ya usalama! We humuoni yule mzee wa.... ametulia unafikili kapenda kutulia?Wenye nchi wameamua kuwa inatosha na hakuna makundi!
 
Sote tuzikumbuka tetesi na minong'ono iliyokuwa imezagaa mara tu baada ya kifo cha Magufuli. Tetesi zilidai kundi la watu watiifu kwa Magufuli hawakutaka mama akikalie kiti hicho. Walifanya kila liwezekanalo ili waweke mtu wao.

Ikatokea kundi la "wenye nchi" likawa na akili kubwa na ushawishi mkubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama wakakakomaa na kuhakikisha mama anakalia kiti.
Kufuatia kadhia hiyo, tuziona watu wengi waliokuwa watiifu kwa Magufuli wakionja joto ya jiwe baada ya mama kukikalia kiti. Akina Bashiru, Polepole, Ndugai, Lukuvi, Kabudi, Hapi, Sabaya, n.k waliondolewa kwenye nyadhifa zao ili wasiwe karibu na sinia la mema ya nchi.

Lkn sasa tunaona mwelekeo wa mama ni kulisogeza kundi la mwendazake taratibu kwenye sinia la mema ya nchi. Uteuzi wa Makonda, Biteko na Mnyeti unathibitisha haya.

Swali la kujiuliza ni je, mama analikimbia kundi lililompigania? Kwann?

Kwanini unaonekana kuwa Mr or Mrs mtabiri na muota ndoto. Kwanini CCM ikupe Shida. Naona Tz wote wanaCCM. Mana hamna ubunifu wala maono. Mnatembelea ndoto na utabiri.
Hawa wanasiasa wanajua wapi wanatoka na wapi wanataka kwenda. Hawana uadui wa kihivyo. Makundi mnatunga wenyewe kwa interests zenu. Muwe na cheap popularity.
 
Sote tuzikumbuka tetesi na minong'ono iliyokuwa imezagaa mara tu baada ya kifo cha Magufuli. Tetesi zilidai kundi la watu watiifu kwa Magufuli hawakutaka mama akikalie kiti hicho. Walifanya kila liwezekanalo ili waweke mtu wao.

Ikatokea kundi la "wenye nchi" likawa na akili kubwa na ushawishi mkubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama wakakakomaa na kuhakikisha mama anakalia kiti.
Kufuatia kadhia hiyo, tuziona watu wengi waliokuwa watiifu kwa Magufuli wakionja joto ya jiwe baada ya mama kukikalia kiti. Akina Bashiru, Polepole, Ndugai, Lukuvi, Kabudi, Hapi, Sabaya, n.k waliondolewa kwenye nyadhifa zao ili wasiwe karibu na sinia la mema ya nchi.

Lkn sasa tunaona mwelekeo wa mama ni kulisogeza kundi la mwendazake taratibu kwenye sinia la mema ya nchi. Uteuzi wa Makonda, Biteko na Mnyeti unathibitisha haya.

Swali la kujiuliza ni je, mama analikimbia kundi lililompigania? Kwann?
Amegundua wale wanamtumia kama chambo..wanataka kupiga dili tu.

Kuna wakati hata waliokuvusha daraja unaweza kuwazamisha ikiwa wanahatarisha future yako. Hata JK aliwasaliti Lowasa na Rostam waliompa hadi uraisi.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Sote tuzikumbuka tetesi na minong'ono iliyokuwa imezagaa mara tu baada ya kifo cha Magufuli. Tetesi zilidai kundi la watu watiifu kwa Magufuli hawakutaka mama akikalie kiti hicho. Walifanya kila liwezekanalo ili waweke mtu wao.

Ikatokea kundi la "wenye nchi" likawa na akili kubwa na ushawishi mkubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama wakakakomaa na kuhakikisha mama anakalia kiti.
Kufuatia kadhia hiyo, tuziona watu wengi waliokuwa watiifu kwa Magufuli wakionja joto ya jiwe baada ya mama kukikalia kiti. Akina Bashiru, Polepole, Ndugai, Lukuvi, Kabudi, Hapi, Sabaya, n.k waliondolewa kwenye nyadhifa zao ili wasiwe karibu na sinia la mema ya nchi.

Lkn sasa tunaona mwelekeo wa mama ni kulisogeza kundi la mwendazake taratibu kwenye sinia la mema ya nchi. Uteuzi wa Makonda, Biteko na Mnyeti unathibitisha haya.

Swali la kujiuliza ni je, mama analikimbia kundi lililompigania? Kwann?
Hakuna kilichompigania zaidi ya katiba ya Tanzania.

Tusidanganyane. Kazi ya Mungu haina makosa.

Nje ya mada; Hivi unafahamu "Sexless" kwa Kiswahili?
 
Hivi unafahamu "@Sexless" kwa Kiswahili?
Hili ni jina halina kiswahili wa kiingereza. Kwani Hilo jina lako FaizaFoxy kiswahili chake kikije?
Ametulizwa akatulia yeye pamoja na vijana wake! Ukijua hili wenzio wanajua hili! Taifa lina wazee wake a.k.a deep state!
Hakuna kitu deep state ipo nchi za watu, siyo hawa walevi wa mnazi wa hapa kwetu. Huyu mzee mm namuaminia mno.

Mama akiendelea na ujinga wake wa kumparura kwa kumtumia Makonda tutaimba parapanda
 
Hapa cdm wanabaki njia panda, jiwe alikuwa anawadunda, wakalalamika, mama akawapa mkono wa amani, wakamwita dhaifu, amerudisha wanaowadunda, wanalia tena.

Wakati mama anahubiri Siasa za kistaarabu, Lissu na genge lake walikuwa wanamtupia matusi ya nguoni, haya Sasa, mmeletewa miksa pilipili kichaa na ndimu

Kwa hiyo mama ameamua kuwarudisha genge la wahalifu ili kushughulika na Chadema?
 
Watu mavi debe, starring kaingia na farasi:

1699748852538.png
 
Swali la kujiuliza ni je, mama analikimbia kundi lililompigania? Kwann?
Hivi hawa watu wote (hao wenye makundi unaowaongelea), wote akili zao ni kama za kukutu, au siyo?

Leo wakikoswakoswa kuchinjwa, kesho wanatupiwa punje za mtama tu na kugeuka kuwa kitoweo?

Pengine huu mfano hauendani sana na nilicholenga kukieleza, lakini ni mfano unao karibia kuwa sawa na hali yenyewe ilivyo.

Hilo kundi la akina Kabuti na wenzake, kama sasa wanarudishwa ili wampiganie mama; hawa watu kweli watakuwa na akili sawa vichwani mwao, baada ya kuyaona yote anayoweza kufanya huyu mwanamke kuihujumu nchi? Wakiwa tayari kumpigania, wanapigania maslahi ya nani, au hilo wao hawalijali kabisa? Katika mioyo yao, watakuwa wanamsaliti huyo huyo waliedai wanamfuata wao (JMP), maanake Samia kaonyesha wazi kuwa hana lolote analoliamini lililofanyika wakati yeye akiwa Makamu wa Rais.

Na hilo kundi la pili, pamoja na kwamba hutaja ni la akina nani hasa (akina Kikwete na genge lake zima, akina Roast?); wakati huu wakiwekwa pembeni, ili kundi la mahasimu wao lipambane kumrudisha mtu wao. Kwa hiyo wanajua wamepewa likizo tu, mambo yatakapokuwa sawa, mama akirudishwa madarakani wanarudi kwa kasi mpya zaidi?

Lililo wazi ni kuwa haya makundi yote yanapambania maslahi yao binafsi, hakuna anayejali maslahi ya waTanzania
Kwa maana hiyo, bila kujali ni kundi lipi linapewa kipaumbele na huyo anayewatumia, waTanzania hawana budi kuutambua ujinga huu na kuukataa.
 
CCM kama ilivyo hahitaji hizo siasa za Kikanda. Kama ilivyo, SSH ni mgombea, kama ilivyo keshapita na kwa matokeo ya 2020 hakuna wa kubadilisha matokeo 2025 na huo ndio Ukweli.
Umejipa mamlaka makubwa sana usiyo kuwa na uwezo nayo. Huu "ukweli" unao ushikilia wewe, ni mungu ndiye kakukabidhi ukweli huo ili uje huku kuusambaza kwa waliomo JF?
 
Back
Top Bottom