Najua, ila tafsiri yake analipwa posho nyingi kuliko mshahara na huo ni ufisadi.
Mkuu haujui!
Raisi hatumii mshahara ama posho zake kujigharamia kwa chochote ukijuacho wewe hapa duniani.
Maneno ya Rais yanaumba kama ya mwenyezi Mungu, akitaka hichi kiwe na kinakuwa atakavyo!
Makazi, usafiri, kula na kuvaa ambayo ndiyo mahitaji muhimu binadamu anasotea, kwake ni bure.
Rais hanuniwi, kila akutananaye naye kila siku na muda wote ni tabasamu la upendo ama la bandia!
Rais hakurupushwi ama kupigiwa hodi,mpaka ajiamkie mwenyewe kwa muda wake atakao.
Mema yote hayo hupungua kidogo sana anapostaafu na mengi takribani yote hubakia kama yalivyo, yaani mishahara, posho, ulinzi, usafiri, makazi pamoja na mambo mengine ya muhimu!
Unadhani kwa nini maRais wengi hawapendi kutoka madarakani?