100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 10,825
- 38,702
Katika siku za karibuni, tumeendelea kushuhudia hali ya wasiwasi na maswali mengi kutoka kwa wananchi kuhusu kuzimwa kwa mitandao ya kijamii kama Facebook, YouTube, na X (zamani Twitter), hasa pale ambapo kuna matukio ya kisiasa yanayowahusisha wapinzani wa serikali au wanaharakati wanaoikosoa serikali. Hali hii hujitokeza mara kwa mara wakati wa mikutano ya waandishi wa habari, maandamano, au mazungumzo ya moja kwa moja (live broadcasts) kutoka kwa viongozi wa upinzani au wakosoaji.
Swali kuu linabaki, Je, ni sahihi kwa kampuni za mitandao ya simu kufuata maagizo ya serikali kuzima huduma ambazo ni haki ya msingi ya wananchi?
Kitaalamu huwa wanafanya blocking at ISP Level (Internet Service Provider) blocking at ISP level , Hii ndiyo njia inayotumika sana. TCRA au idara ya serikali hutoa agizo kwa ISP (kama Vodacom, Airtel, Tigo, TTCL, nk) kupiga marufuku domain au IP address ya huduma fulani, mfano youtube.com au facebook.com, kampuni husika hupitisha maagizo haya kwa firewalls au DNS filtering, hivyo wateja wao hawawezi kufikia mitandao hiyo.
Je, Ni Haki Kuzima Mtandao Kwa Sababu ya Mtu Mmoja Kuongea?
Ni sawa na kufunga barabara zote kwa sababu mtu mmoja anatembea bila leseni. Ni hatua ya kupita kiasi, disproportionate response, na haipaswi kufumbiwa macho...
Makampuni ya simu yachague kusimama na wananchi, si kukandamiza kwa niaba ya mamlaka.
Mitandao ya simu lazima itetee haki za wateja wao.
Sio wakiambiwa zima wao ni kuzima tu, kuna watu hawapo kwenye siasa kipato chao chote hutegemea mitandao kama youtube, instagram na facebook...
TCRA inapaswa kuwa wazi na kuwajibika kwa wananchi , kwa sababu kazi yao ni kusimamia mawasiliano, sio kuyakata....