Je, Msajili wa Vyama vya siasa alikaa lini na IGP akaambiwa kuna kikao?

Je, Msajili wa Vyama vya siasa alikaa lini na IGP akaambiwa kuna kikao?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Ni lini Msajili wa vyama alikaa na IGP wakapanga kuwepo kwa kikao Cha IGP na vyama vya siasa?

Nani aliyeandaa agenda za kikao hicho?

Ni vyama vipi vilifika kwa msajili kuomba kuwepo kikao Kati ya IGP na vyama hivyo?

Hiki kikao kipo chini ya sheria gani? Maamuzi ya kikao hicho yatatekelezwa kwa sheria gani na yasipotekelezwa na upande mmoja yatakuwa na athari gani?

Je, ipo sheria yakuzuia shughuli za kisiasa kusubiri IGP akae kikao na vyama vya siasa?
 
Haya mambo yako hivi, mbona ni rahisi kuyaeleza na kuyaelewa?

Tabia mbovu sana tuliyonayo waTanzania ni kutohoji chochote kinachosemwa na viongozi hawa wa ngazi za juu. Tunachukulia kama ni sheria kwa kila tamko linalotolewa na hawa viongozi, hata kama tamko lenyewe linapingana na sheria zilizopo.

Rais akisema kitu chochote, hiyo ni amri, hata kama amri hiyo inakiuka sheria!

Ndiyo maana, hata hawa waliopo ngazi za chini, wanachukulia matamko yao ni kama sheria, hawategemei kuhojiwa kwa matamko hayo.
Na ukiwauliza wananchi wengi watakwambia huwezi kushindana na serikali, hata kama serikali hiyo inakanyaga haki zako

Mtungi alipoyasema hayo, yeye alijua ametoa maagizo ambayo hayatakiwi yahojiwe na mtu yeyote, pamoja na kwamba matamko yake yanakiuka taratibu.

IGP na wasaidizi wake, ni mara ngapi umesikia wakitamka maagizo yao kuwa ndiyo sheria, huku maagizo yakiwa yanakinzana na sheria zenyewe!

Na ubaya zaidi, hakuna hata mmoja wetu aliyechukua wajibu wa kwenda mahakamani ili uamzi utolewe kuhusu uhalali wa maagizo yanayotolewa kiholela tu na kuwa kama ndizo sheria zenyewe.

Wananchi wanaridhika kabisa; kwa sababu hawahoji chochote.
 
Kwa upande wangu nakiona ni kikao muhimu sn sababu watakaoendelea kuumia ni vyama vya upinzani, Sirro ana mabomu, risasi, mahabusu na mahakama ndiyo kinachompa kiburi, vita yoyote ile humalizwa kwa mazungumzo.
Wapinzani makini wakihudhuria ni mwanzo wa kufanyiwa vikao vingine vya kipuuzi kama hiki huko tuendako. Kwani nchi hii hamna sheria na kanuni za kuongoza shughuli za kisiasa hadi kuanzishwe vikao haramu na mtu tu aliyekaa ofisini kwake hapo Mchafukoge?
 
Wapinzani makini wakihudhuria ni mwanzo wa kufanyiwa vikao vingine vya kipuuzi kama hiki huko tuendako. Kwani nchi hii hamna sheria na kanuni za kuongoza shughuli za kisiasa hadi kuanzishwe vikao haramu na mtu tu aliyekaa ofisini kwake hapo Mchafukoge?
Haya tumieni nguvu lakini watakaoumia ni wapinzani, watapigwa mabomu, kuwekwa mahabusu, risasi au kufungwa kabisa.
 
Back
Top Bottom