Haya mambo yako hivi, mbona ni rahisi kuyaeleza na kuyaelewa?
Tabia mbovu sana tuliyonayo waTanzania ni kutohoji chochote kinachosemwa na viongozi hawa wa ngazi za juu. Tunachukulia kama ni sheria kwa kila tamko linalotolewa na hawa viongozi, hata kama tamko lenyewe linapingana na sheria zilizopo.
Rais akisema kitu chochote, hiyo ni amri, hata kama amri hiyo inakiuka sheria!
Ndiyo maana, hata hawa waliopo ngazi za chini, wanachukulia matamko yao ni kama sheria, hawategemei kuhojiwa kwa matamko hayo.
Na ukiwauliza wananchi wengi watakwambia huwezi kushindana na serikali, hata kama serikali hiyo inakanyaga haki zako
Mtungi alipoyasema hayo, yeye alijua ametoa maagizo ambayo hayatakiwi yahojiwe na mtu yeyote, pamoja na kwamba matamko yake yanakiuka taratibu.
IGP na wasaidizi wake, ni mara ngapi umesikia wakitamka maagizo yao kuwa ndiyo sheria, huku maagizo yakiwa yanakinzana na sheria zenyewe!
Na ubaya zaidi, hakuna hata mmoja wetu aliyechukua wajibu wa kwenda mahakamani ili uamzi utolewe kuhusu uhalali wa maagizo yanayotolewa kiholela tu na kuwa kama ndizo sheria zenyewe.
Wananchi wanaridhika kabisa; kwa sababu hawahoji chochote.