Je, Msajili wa Vyama vya siasa alikaa lini na IGP akaambiwa kuna kikao?

Huko alipo anakung'atia meno. anaona unamvurugia dili lake.
 
Siyo kosa Lao au lrtu Bali ni ukosefu wa elimi ya uraia. Muulize Anna Tibaijuka wakati ule alipoanzisha bawata, na kutaka Kuanzisha Elimu ya uraia. Kilichofuata ni nini?. Hakika tuna safari ngumu na ndefu. Wengine wanajita ni mamba na safari haiwahusu Bali ni ya kenge pekee mwisho wa siku mamba wanageuka kuwa kenge na wenyewe.
 
Kuna wakati unafika, suala la makubaliano kama nchi ni la muhimu kuliko uweledi wa kuongozwa kama nchi. Nnaloliona kinachotafutwa ni utengamano wa kisiasa ndio kinachotafutwa.
 
Huwa kuna walioruhusiwa kupiga wenzao mabomu,risasi au kuwafunga bila
utaratibu?.Sheria zetu zinaelekeza hivyo?
watu wanauliwa wanavunjwa miguu, nenda kwenye vituo vyao uone watu wanavyopigwa kama punda mpaka Rais kaliona hilo juzi kasema, upelelezi kwao ni kupiga hakuna kingine
 
Vita yoyote humalizwa kwa njia ya mazungumzo

Mazungumzo ya vyama vya upinzani na polisi? Seriously?

Wewe unaamini polisi wanaamua wenyewe kupiga na kuvuruga shughuli za wapinzani? Kwamba wanaweza kushawishiwa waache hiyo roho mbaya?

Naona siku mbwa wa jirani akikung’ata utataka “mazungumzo” na huyo mbwa badala ya mmiliki wake. Btw, Sirro na Mutungi ni dugu moja.
 
Mkuu polisi wameshika mpini na ww umeshika makali sijui nani ataumia?
 
watu wanauliwa wanavunjwa miguu, nenda kwenye vituo vyao uone watu wanavyopigwa kama punda mpaka Rais kaliona hilo juzi kasema, upelelezi kwao ni kupiga hakuna kingine

Viongozi wakuu serikalini wote wanajua kinachoendelea polisi - miaka nenda, miaka rudi. Na ndio mkakati wao: wananchi wawe na hofu na jeshi la polisi; wasithubutu “kuichezea” serikali.

Hizo kauli kwenye media ni za kisiasa kuwapumbaza wanyonge. Polisi wataendelea kuwa hivyo hivyo kwa kadri watawala wanavyokuwa na “blank cheque” ya kufanya chochote nchini bila kuhojiwa. Polisi ndiyo fimbo yao dhidi ya waleta “chokochoko”.
 
Utaanzaje kumhoji mtu aliyeshika silaha na anakulazimisha umtii?
Wananchi sio wajinga.
Ukimtesa mtu unatesa na mke wake, watoto wake, na ndugu zake wasio na hatia.
Hawa wanaotesa wenzao ndiyo hawatumii akili, sio wananchi wasio na hatia ambao baadhi ni 'malaika' wasiojua hata kusema.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu polisi wameshika mpini na ww umeshika makali sijui nani ataumia?

Simple logic.

Polisi WANATUMWA kukupiga na kukuvunja miguu. Wakitumwa hakuna utakachowaambia wakuelewe. Jaribu kuongea na mbwa anayekufukuza akuume badala ya kuongeza kasi kumkimbia.

Ukitaka polisi wasikupige, tii sheria bila shuruti. Hakikisha pia unatii bila kuhoji maagizo yote yanayotolewa na Rais na viongozi wa serikali. Ukifanya hivyo polisi watakupita kama vile hawakujui.

Police ni “law enforcers”. Hapa kwetu pia ni enforcers wa maagizo ya Rais ambayo ni juu ya sheria na katiba. Utajadiliana nao kwa ajenda ipi?
 
Ndiyo ujue hali ni mbaya zaidi
 
Ndiyo ujue tuna katiba ya hovyo kabisa, Rais wa S.A mwaka huu aliitwa kuhojiwa na polisi kwa matumizi mabaya ya fedha za umma, huku wanaweza hata kumuhoji DC?
 
Haya tumieni nguvu lakini watakaoumia ni wapinzani, watapigwa mabomu, kuwekwa mahabusu, risasi au kufungwa kabisa.



Hivi hao jamaa wangeendekeza ubinafsi na uoga wa kiwango hata robo ya chako, sijui wewe ungekuwa wapi?
 
View attachment 1927597
Hivi hao jamaa wangeendekeza ubinafsi na uoga wa kiwango hata robo ya chako, sijui wewe ungekuwa wapi?
kuhusu uhuru muda wa wakoloni kutawala uliisha kulingana na mikataba ya kimataifa, ndiyo maana unaona hakuna nchi inayotawaliwa tena. Kati ya wote Madela pekee yake ndiyo alipata shida wengine utadanganywa
 
kuhusu uhuru muda wa wakoloni kutawala uliisha kulingana na mikataba ya kimataifa, ndiyo maana unaona hakuna nchi inayotawaliwa tena. Kati ya wote Madela pekee yake ndiyo alipata shida wengine utadanganywa
Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…