Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
Tutake tusitake Kama wapigakura ni watanzania hawa waliolala Mkuu jibu ni Jakaya kikwete hata akitaka kubadili katiba aenbdele kipindi cha 3 atashida tuu.status quo will always win.

Na haleti mabadiliko yoyote atazidi kusari na kuwachi mafisadi wenzake waendele kufanya wanachotaka.Histori inatueleza hana kasumba ya kuleta maendeleo so tusitegemee chochote

Na lawama wanabeba vijana wa Tanzania hakuna mwengine
 
Atakuwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa sababu ya mfumo uliozoeleka ndani ya CCM. Hakuna anayeweza kujitokeza ama hata akijitokeza akakubaliwa kupinga Kikwete asiendelee. Akina Zitto bado wanafanya makosa ya hapa na pale hawawezi kushika nchi 2010 hata kama watajitokeza kugombea urais.
 
Mkuu Waberoya,

Nakuunga mkono, hakuna ubishi hapa. Historia itapiganiwa hata iweje; kwa hiyo bila ubishi ni JMK.
 
Standards and Speed - Samweli Sitta.
 
kwa jinsi ambavyo maisha ya mwananchi yako hohe hahe mtu atakayekuwa raisi 2010 ni yule atakaye sambaza kanga, t shirt, kofia tanzania nzima. Na vile vile kugawa wali na pilau kwa wananchi ambao wakipata vitu hivi hawatavipata tena mpaka 2015. Kwa wananchi wengi uchaguzi kwao maana yake ni nguo mpya zenye rangi ya njano na kijani, pilau kwa sana na shilingi elfu tano. Na wala sio kiongozi bora anayejali maisha ya mpiga kura au nchi yake.Anayebisha aseme na alete proof.
 
Jakaya Mrisho Kikwete..na amini atakuwa rais tena...Lakini naomba kuwa sikio la kufa sasa lisikie dawa...alete mabadiliko ya kweli

Mabadiliko ya kweli yatoke wapi? La kuvunda halina ubani ndugu yangu....Tumeula wa chuya kwa miaka kumi mfululizo......!!! Ni ukweli tupu japo ni mchungu na unauma!
 

100% CORRECT.....!! Unajua wengi wetu humu wako nje ya nchi, na walio ndani ya nchi ni wale walioko kwenye viyoyozi na internet access ya 24 hrs! Lakini 80% ya Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura huwa wanapiga kura kutokana na nani kawapa nini! Bado ni masikini wa fikra, mali, elimu ya yote unayoyafikiria!

Nguzo kuu ya ushindi wa CCM kwenye chaguzi zetu ni UMASIKINI wa Watanzania......! Ndio maana CCM haiwezi kupambana na umasikini kwa kuwa wanajua Wataongeza uwezekano wa kung'olewa madarakani. UMASIKINI wa Watanzania ni "MTAJI" wa uchaguzi kwa CCM
 
Nguzo kuu ya ushindi wa CCM kwenye chaguzi zetu ni UMASIKINI wa Watanzania......! Ndio maana CCM haiwezi kupambana na umasikini kwa kuwa wanajua Wataongeza uwezekano wa kung'olewa madarakani. UMASIKINI wa Watanzania ni "MTAJI" wa uchaguzi kwa CCM

No wonder elimu ya uraia ni mwiko kutolewa kwa watanzania, something has to be done really so that wananchi wajue kuwa kura moja haiwezi kunuliliwa kwa kanga moja kwa miaka mitano, it is a serous joke,
 
Ni mimi na wewe tutakaopiga kura ndio tutakaoiongoza nchi yetu
 
Heshima Mbele,

Ni muda mrefu sijapita hapa na kuandika makala kuhusian na mstakabali wa taifa letu.Nipo na nimekuwa nikipita hapa mara kwa mara kuangaia vijana na wazee wanatoa michango gani kwa taifa hili.

Kipimo cha usaniii kinaongezeka kila siku na kibri(tabia ya mwenyezi Mungu) imekuwa ikitawala sana kwa sasa.Khali ya kimaisha kwa watanzani wwengi ni ngumu sana kwa sasa na imesababishwa na udhalimu na Genge la watu wachache wabinafsi wenye kupenda Fedha .

Genge Hili ndilo limejenga Mtandao wa kutawala milele na wanendelea na Kupanda Mbegu ambzo zinakaribiana na zile za DECI,ila nitaomba serikali(wananchi) wakate Mbegu za DECI na kumua kuchagua kile wakitakacho.


Juzi na kila wakati nimekuwa nikipokea salamu za masikitiko mengi sana toka kwa ndugu zangu akilalamika jinsi khali walivyochoka na utawala huu.Wanahudhunika kwa kuwa wamepuuzwa,wanachekwa na wale ambao wanaona walizaliwa ili wawe watawala na wawe na nguvu kuliko Muumba.

Kuelekea 2010 na kuanzia saa hii na leo hiinaomba kuamsha hisia kali zaidi ya zile za kimasai,Taifaa linaeleka kubaya na kama tusipochukua hatu ampema basi nchi itapata anguko kwa kuwa kila mtu atakuwa akilalama na watakata tamaa.

Kuelekea mapinduzi ya Ukweli naomba sasa tuanze kwa kuwapa Nafasi Vijana ili waweze kuonesha wanaweza.Wazee walishashindwa na walishakataa kuachia vijana wakiogopa vijana watajua yale machafu waliyo nayo.

Miaka minne imetosha na mwaka wa tano unakuja ni kukamilisha ratiba ,ila nawaapia wana wa adamu,kiukweli kabisa kama mkiendelea kuwachagua wasanii kamwe mjue maisha hayatakuwa Bora.Na hatua za kuchukua ni chache ni hizi hapa;

Hatua ya kwanza ni tuanze na viongozi wa serikali za mitaa,Chagueni wale walio Bora ambao wana weza kuleta Mabadiliko Bila kujali dini ,itikali ama nasaba yoyote.

Pili,Kwa vuyama vya Upinzani kuanza kujenga taifa litakaloikomboa nchi hii na kwa kuanzia namuunga Mkono zitto zuberi kabwe na niko Nyuma yako.Mhe. Zitto apewe uenyekiti na mambo mengine yatafuata baadaye,nina imani na huyu kijana toka wakti flani nilipokutana naye ujerumani,aliniambia nia yake kulikomboa taifa hili,dhamira yake inaonesha ana uwezo hivyo tumuunge Mkono.

Tatu,kuanzia sasa hivi msipokee Hongo ama chochote toka kwa wale wabunge ambo wameanza kudi katika majimbo yenu kuwahadaa,achaneni nao waambieni Bakora mlishazianda na 2010 hamtafanya makosa kama ya 2005.Msiwachague kamwe na ikiwezekana mwuwafukuze warudi mjini.

Mie mwenyewe nakiri nilikosea ,na sikumjua vizuri niliyemchagua .hata pale Mhe. John cheyo alivyo niambi haumjui huyu.Sasa nimetambua bila yeye Maisha Nora yatapatikana.Najua hapendi kupingwa ila nataka ajue mimi ndiyo nimesema haya.

Inawezekana kama tukiwa na Tumaini Moja na kwa kumtumaini Mwenyezi Mungu(S.A.W).Inshallah tutafika !


wenu

Niandikie gembe@jamiiforums.com
 
Last edited:

nilikuwa nampa tano sana mgombea ambaye angetoka chadema hasa ktk vita ya mafisadi na ufisadi ila kwa yaliyotokea sasa huko chadema mmmmhhh......ccm (kikwete) atashinda tu
 
nilikuwa nampa tano sana mgombea ambaye angetoka chadema hasa ktk vita ya mafisadi na ufisadi ila kwa yaliyotokea sasa huko chadema mmmmhhh......ccm (kikwete) atashinda tu

Mkuu,
Umekata tamaa mapema hivyo?
 
Ni kweli mwanafalsafa.
Nakubali.
Bulesi anasemaje hapo?

Nikweli kuwa sio kila mkuu wa nchi anawekwa na Mungu, bali mwenyezi Mungu ndiye mwenye mamlaka juu ya UHAI wa hao wanaoongoza nchi!! Bila kuwa na uhai hawawezi kuwa viongozi.
 


Jakaya Mrisho Kikwete
 
Nikweli kuwa sio kila mkuu wa nchi anawekwa na Mungu, bali mwenyezi Mungu ndiye mwenye mamlaka juu ya UHAI wa hao wanaoongoza nchi!! Bila kuwa na uhai hawawezi kuwa viongozi.

Hapa sioni jipya.
Hata uhai wa Fisi si uko mikononi mwa Mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…