Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

I only appeal to sense.

Je hayo uliyoandika kwako binafsi yanakujakuja kuwa ni sahihi.

Kimantiki, kibaiolojia huyo ni mtoto wa huyo baba na ndio ukweli. Sasa kikija chanzo kingine au mamlaka nyingine ikasema kinyume na hivyo kimantiki inakuwa inasema uongo(kinyume na ukweli).

Ukweli siku zote haupingani na ukweli bali unajaziaga nyama tu. Maana ukweli ni mmoja. Tafakari. Chukua hatua ...
 
Chief wewe ulisema hao watoto wa nje ya ndoa wamejaaliwa na Mungu ndio maana unaona sawa Tu,ndio nikakujibu je wote waliojaaliwa wapo sahihi?

Nikatoa mfano hapo majambazi na wauza unga.

Mwanaume anawajibishwa Kwa kuwekwa Mbali na mtoto Kwa maana ananyang'wa mtoto na haki zake ikiwemo kurithiwa na kuitwa Jina la ubini wake
 
Hili la kubagua watoto limeongeza ukatili katika jamii kwa asilimia nyingi mno.
Kuna wale wauaji wa,,, aaah sijui kiswahili chake, ma serial killer ndivyo wanavyotengenezwa mtoto akue anaambiwa wewe ni kidudumtu, asijaliwe na apate uonevu kama huu kutengwa. Akigeuka akawa myama unyamani si tumejisababishia wenyewe matatizo katika jamii?

Kama jambo halileti afya ni kheri kuachana nalo tu. Kama suala ni zinaa basi adhabu ielekezwe kwa walioitenda... huyo baba na huyo mama sio kumlabel mtoto majina mabovumabovu
 
Mmekaa kikandamizi sana,ona lawama zote mnamsukumizia mwanamke…Hata katika mahusiano ya mapenzi kawaida nani huwa initiator kama sio mwanaume? Sasa mwanamke anakujaje hapo?ok sawa na je waliobakwa? Wao ndo wamesababisha?
Hili li dini linakandamiza wanawake
 
Labda huko kwenu,yaani hata leo mmewangu akajichanganya akamzaa huko yaani atampa haki zake atake asitake,mfanye starehe zenu afu mje kumhusisha mtoto
Yaani haki zake nakwambia utampa tu,
 
Mkuu kuna mambo ya kureason lkn zinapokuja Sheria za Mola wako aliyekuumba wewe na Mimi huna haki ya kuleta maoni yako
Ingekuwa reason haihitajiki basi tusingepewa. Tena kutoitumia ndio litakuwa kosa.

Yaani upewe utashi halafu ukatae kuutumia na uone ni sawa.

Kwa kuwa sheria na aya na kila kitu vyote vimepitia kwa wanadamu kabla ya kutufikia sisi. Reason inahitajika kujua ipi mbivu ipi mbichi lazma tu reason bhana.

Uzuri ni kwamba ukweli TRUTH hauiogopi reason, kwa sababu unajisimamiaga imara wenyewe.
 
Chief kila kitu kimeumbwa na Mungu,binadamu baada ya uwepo hapa duniani hakujua lolote Bali alikuja kupewa elimu ya mambo mbali mbali na Mola wake.

Mungu ndio mmiliki WA kila kitu hapa duniani Sisi tumepewa kama wasimamizi WA mambo hapa duniani.

Kwahiyo Mungu si mahitaji WA hizo pesa kwasababu Hana matumizi nazo Ila anataka tuzitumie Kwa kuwasaidia waja wake wenye uhitaji hapa duniani,ndio maana sadaka inatakiwa wapewe watu maalumu na kuendesha mambo ya ibada mbali mbali yaende Sawa.

Kwakifupi utaratibu upo WA kuyaendea mambo vizuri vile Mungu anavyotaka Ila binadamu Sisi ndio mafisadi
 
Kuna mambo ambayo yapo wazi kabisa hauhitaji kureason, je kwa mfano kumuabudu Mungu unahitaji kureason?

Kufuata sheria mathalani usizini,usiue au kuiba je unahitaji kureason?

Mungu kuuwawa na watu wake hapo utahitaji reason,Mungu kuwa na mtoto hapo utahitaji kureason
 
Chief tumesikia maoni yako
 
Kwahiyo wadiz unataka kusema kuna Mungu wa Africa na Ulaya?

Anyways linapokuja swala la Imani ni kubwa Sana na very complicated lakini naheshimu maoni yako brother
Namaanisha kuna version za mitazamo Africa ilikuwa Mungu yuleyule wa Jana Leo na kesho hata bila uwepo wa Biblia ya Leo, Wala ukristo na uislam
 
Mahitaji ya mtoto hayana uhusiano na uzinzi wetu. Nimeshazini nimezaa huyo mtoto ni halali yangu na atapata haki zote hata kama dini haitaki. Viongozi wa dini wanaruhusiwa kununa. Sitelekezi mtoto, ni vile haijanitokea tu nikazaa nje ya ndoa.
Mkuu mbona ww ni mtu muelewa sana inakuwaje unashindwa kunielewa ?

Nimesha kwambia kuwa hujakatazwa na wala si haramu kwa ww kumuhudumia mtoto uliye mzaa nje ya ndoa ila hautakuwa na nguvu ya maamuzi, mamlaka wala haki yeyote mbele ya huyo mtoto kama baba.

Mfano kama ni mtoto wa kike akihitaji ruhusa ya kuolewa kutoka kwa wazazi wake mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi ni mama yake na sio ww.

Na hauna haki ya kudai hisani yeyote kutoka kwa huyo hata awe tajiri kama Mo haijalishi umemlea au hujamlea.

Nadhani ume nielewa hakuna sehemu ambayo unakatazwa kulea.
 
Unajua jinsi mtu anavyosoma na kujiona ana elimu kubwa basi huona Dini hazina maana na upumbavu.

Na Baya zaidi humuona Mola wake sio chochote kwakuwa Tu ana afya njema,ana bando la kuingia Jf na familia yake inakula.

Sawa mtuache Sisi wapumbavu tumuamini Mungu wetu
 
Mtoto wote walio zaliwa nje ya ndoa ni haramu kwa mujibu wa dini zote kuanzia Ukristo, Uislamu, na hata uyahudi usitake kujifariji hapa.

Tena mayahudi linapo kuja suala la kuzaa nje ya ndoa ni wakali mno na wakigundua wanakutenga.
 
Ndoa ndio inakupa uhalali wa kumiliki zao linalopatikana .
Kwa mfano unaweza kwenda kujenga nyumba kwenye kiwanja ambayo ina hati ya jina la mtu mwingine ?
Swadakta chief umesema kweli
 
Chief tumepokea maoni yako
 
Mkuu sio kwamba sijakuelewa, ni kwamba nimezikataa hizo sheria na taratibu na kuamua kuwa sio za kuzizingatia pale jambo kama hilo linapotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…