Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Mtoto ni mtoto!!hakuna haramu wala halali as long as Mungu ameruhusu azaliwe...kabla ya kuletewa dini mambo yalikuaje,maana Mungu hakuumba dini ila mwanadamu!
 
Chief

Kuna kitu kimoja naomba ujue,mwenye shamba ndio mwenye mazao yake,yaani mfano Mimi Nina mke hlf wewe ukatembea na mke wangu na kuzaa nae basi ujue huyo mtoto ni wangu Mimi kisheria kwasababu Mimi ndio mwenye mke, mahusiano yangu na mtoto ni ndoa

Ni Sawa Sawa na wewe ukizaa na mwanamke Kwa zinaa,wewe Yule sio mwanao kwasababu kiunganishi chako na mtoto kisheria hakuna,ndio utakuwa biological father lkn kisheria huyo mtoto hatambuliki na sheria ya Dini,hivyo hawezi kukurithi wala wewe huwezi kumrithi hata kidogo .

Ila Kwa mama Hana Shaka kwasababu huyo ni mwanae na wanaweza kurithiana
Labda Sheria ya dini ya kiislamu, yaani umzalishe Binti huko nje alafu useme sio mtoto wako kwa sababu ya Sheria ya dini, acheni kunyanyasa wanawake na kuwabagua. Hapa ndio mnafanyaga dini zionekane ubabaishaji.
 
Kisheria mtoto wa zinaa ni WA mama Tu,tambua au tofautisha juu ya sheria za Dini na nje ya sheria za Dini

Sasa kama unafuata Dini basi tambua mtoto wa zinaa ni WA mama
Why mwanamke na sio mwanaume?
 
Labda Sheria ya dini ya kiislamu, yaani umzalishe Binti huko nje alafu useme sio mtoto wako kwa sababu ya Sheria ya dini, acheni kunyanyasa wanawake na kuwabagua. Hapa ndio mnafanyaga dini zionekane ubabaishaji.
Kwanini husemi wazinifu mpaka wanazaa nje ndio wababaishaji?

Haki siku zote itabakia kuwa haki hata kama huipendi chief

Kama ni muislamu basi huwezi kukwepa sheria,Sisi hatujakombolewa na damu ya mwanadamu,sheria ni sehemu ya mafundisho yetu.
 
Kwa mujibu wa imani ya kiislamu mtoto ambaye amezaliwa nje ya ndoa hatambuliki Kwa mujibu wa Sheria kama mtoto wa Baba husika.

Kwasababu kizazi au uzao WA familia unatakiwa upatikane ndani ya ndoa ya kisheria au ndoa iliyofungwa Kwa misingi ya Dini,na nje ya hapo huyo ni mtoto wa zinaa ambaye kisheria anatambulika kama mtoto wa mama aliye mzaa Tu.

Ingawa kikawaida atafahamika kama mtoto wa Baba Fulani lkn kidini huyo Baba hatambuliki na hivyo kuna haki Fulani ambazo Baba hawezi kumfanyia mtoto wake.

Moja wapo ni huyo mtoto hafai kuitwa Jina la ubini WA Baba yake,Hilo Jambo ni haramu Sana na Mungu ameshalikemea tayari, ingawa Kwa bahati mbaya Sana Kwa kutojua wengi wamewapa majina ya ubini wao hao watoto wa nje ya ndoa.

Na lingine ni kumuozesha kwenye ndoa, Baba Hana haki ya kumuozesha binti yake WA nje ya ndoa Kwa mumewe kwani ndoa hiyo ni batili na haifai kabisa.

Lingine huyo mtoto hawezi kumrithi Baba yake kwasababu kisheria huyo mtoto sio WA huyo Baba,Bali Baba anaweza kumpa sehemu ya Mali huyo mtoto,lkn mara Tu huyo Baba anapokufa basi huyo mtoto Hana haki ya Kurithi chochote.

Lakini sio vibaya huyo Baba kumhudumia huyo kijana Kwa malezi na mahitaji mbali mbali maadam Tu yeye ndiye sababu ya kuja Hicho kiumbe hapa duniani.

Na mtoto ambaye Hana Baba kisheria anaweza kuitwa Kwa jina la mama yake, Kwa mfano ETUGRUL BEY ASHA au Kwa jina la ubini Kwa upande wa mama yake.

Kubwa ni kutambua uzao mzuri ambao hata kizazi chako kinaweza pata haki stahiki ni kizazi ambacho kinatokana na ndoa takatifu ambayo IPO Kwa mujibu wa Sheria.

Na hata wale ambao wanafunga ndoa za kiserikali basi watambue kidini Hicho kizazi Chao hakitambuliki na Sheria za Dini Kwa maana Baba Hana watoto hapo Ila watoto ni WA mama.

Ni hayo Tu!

Kazakh destroyer
Msonjo
Nurain
adriz
professional Driver
baby zu
Unataka uite ubini wa nani afu baba akifa umlete mwanao apate mgao c ndio
 
Unataka uite ubini wa nani afu baba akifa umlete mwanao apate mgao c ndio

Mtoto wa nje ya ndoa ima anaweza kuitwa Kwa jina la mama yake au ubini WA mama yake.

Na huyo mtoto Hana haki ya kumrithi Baba yake Bali mama yake, na Baba hamrithi huyo mtoto, Ila unaweza kumpa Mali lkn ukifa Hana haki ya kukurithi
 
Haramu ni haramu uwezi ita jina la ubini wa kao baba kwa mtoto haramu uyo anapewa majina ya kwao mama yake sAbu mama yake tyr kashakua haramu
Uharamu WA mama na mtoto unaingiaje hapo chief

Yatosha kuitwa mtoto wa nje ya ndoa au zinaa
 
Sasa hii dini ya HAKI mbona inakinzana na haki za mtoto kwa makosa ya wazazi wao
Haki siku zote inaambatana na wajibu,maana utazini na kusema haki yako na kulaumu Dini ya haki inakunyima haki

Sheria IPO kuwajibisha na kurekebisha
 
Mtoto ni mtoto!!hakuna haramu wala halali as long as Mungu ameruhusu azaliwe...kabla ya kuletewa dini mambo yalikuaje,maana Mungu hakuumba dini ila mwanadamu!

Wewe unazungumza Kwa matamanio yako.

Kama hujui Dini imetoka wapi basi ni changamoto kubwa sana
 
Msinyanyase watoto kwa kigezo cha dini.

Watoto wote wana haki sawa ya kupata malezi/mapenzi ya wazazi wao.
Watu haohao wameshikilia Ismail ni mtoto wa Abraham ili hali kazaliwa na kijakazi wa mke wake.
 
Kwanini husemi wazinifu mpaka wanazaa nje ndio wababaishaji?

Haki siku zote itabakia kuwa haki hata kama huipendi chief

Kama ni muislamu basi huwezi kukwepa sheria,Sisi hatujakombolewa na damu ya mwanadamu,sheria ni sehemu ya mafundisho yetu.
Binadamu ni zaidi ya hiyo dini au ndoa, unaijua haki ww au unataka kuleta Sheria zisizo na KWELI ndani yake, ikiwa haki ndio inatafutwa basi hakuna haramu kwa kiumbe hai kwa kuwa sio mpango wako ww mwanadamu. Ndoa ni utaratibu wa kurasimisha umiliki wa kimahusiano kati ya mtu na mtu hapa Duniani zisikutoe ufahamu ukajiona unahaki zaidi ya wengine.
 
Watu haohao wameshikilia Ismail ni mtoto wa Abraham ili hali kazaliwa na kijakazi wa mke wake.
Baada ya mama Sara kumkabidhi hajara Kwa Ibrahim alimkabidhi kama mke tayar

Je Una shida na Hilo chief?
 
Binadamu ni zaidi ya hiyo dini au ndoa, unaijua haki ww au unataka kuleta Sheria zisizo na KWELI ndani yake, ikiwa haki ndio inatafutwa basi hakuna haramu kwa kiumbe hai kwa kuwa sio mpango wako ww mwanadamu. Ndoa ni utaratibu wa kurasimisha umiliki wa kimahusiano kati ya mtu na mtu hapa Duniani zisikutoe ufahamu ukajiona unahaki zaidi ya wengine.

Kwanza ujue unazungumza katika muktadha gani?

Mada imejikita katika sheria za Dini ya kiislamu.

Sasa kama una mambo yako mengine naomba utupishe
 
Back
Top Bottom