Sheria ingelenga kumuadhibu baba ningeielewa ila hapa inamwadhibu mtoto asie na kosa lolote , hajazini hakuomba kuzaliwa , hakujileta dunian ...
Chief
Tatizo lenu mnayaangalia mambo baada ya Athari kutokea lkn hamuangalii ni Kwa namna gani ya kuzuia uchafu kama huo usitokee.
Sheria imewekwa kuzuia huo upuuzi usiwepo sas watu kama nyinyi ndio mnatengeneza mazingira ya mambo hayo kuendelea kuwepo
Mnaona haki ya mtoto wa zinaa kunyimwa lakini hamuangalii watoto wenye haki halali kupotea,unapokuwa na watoto wa ndoa ndani na hapo hapo ukawa na watoto wa zinaa nje,unajua maana yake nini?
INA maana kile ambacho ulikuwa uwape watoto wako WA ndoa takatifu unapunguza baadhi ya haki zao na kwenda kulisha au kuwavisha watoto ambao wamepatikana katika njia ya haramu na mbaya mbele ya Allah, je hiyo sio dhuluma?
Msitafute huruma Kwa mambo ambayo yapo nje ya mpango wa Allah, njia sahihi ni kizazi ambacho kunapatikana katika ndoa halali na huo ndio utukufu WA mwanadamu,sasa kama tunazaa zaa ovyo je tunatofauti gani na wanyama?
Mwisho ifahamike kwamba huyo mtoto wa zinaa,anaweza kuishi na familia yako kwasababu Una haki ya kumlea coz wewe ndio sababu ya kuja kwake duniani,unaweza kumwandikia WOSIA WA Mali.
Lakini hawezi kukurithi kwakuwa huna nasabu naye,na huwezi kumrithi,na kama ni mtoto WA kike huwezi kumuoza kwasababu wewe sio Baba yake kisheria.
Narudia tena msitumie nguvu kubwa kutetea uovu Bali tumieni nguvu kubwa ili vizazi vyetu vije kuachana na Tabia za ovyo na chafu mbele ya Allah