Kuna wengine walikuja hapa kwangu wakiwa wa 3, nikakubali wanifundishe kupitia vile vijarida vyao. Kila siku wananipima kwa kuniambia niwaulize maswali, nikawaambia naomba kwanza biblia mnayotumia niisome halafu maswali yangu yatokane na tafsiri ya biblia yetu.Umenikumbusha,
Nilipokuwa katika mkanganyiko mkubwa baada ya kusoma BIBLIA, nilitaka kujua Yesu ni nani Hasa.
Nilipokuwa katika kuwaza, wakaja watu wawili na kugonga geti LANGU na kujitambulisha kuwa wao ni mashahidi wa YEHOVA.
Walisema hakuna Roho mtakatifu,
Wakasema pia Yesu ndiye Mikael Malaika mkuu,
Kwamba kwao, Yesu ni Malaika.
Nilipowahoji maswali kiundani walinikimbia.
Mashahidi wa YEHOVA ni dini ya uongo ya mpinga Kristo.
Ikiwa upo huko, hama haraka, kuzimu inakwita.
Wakaleta, baada ya kumaliza kijarida cha kwanza, nikawauliza swali MTU ANAPATAJE WOKOVU? wakafurahi sana, wakaleta maandiko mengi sana, tulipoyasoma kwenye biblia yako, kukawa na contradiction
Wao wanasema wokovu unapatikana kwa ushirika wa imani, matendo mazuri na tuii
Kinyume na Yohana 3:16, efeso 2:8-9,Tito 3:5 haya maandiko hata kwenye biblia yao yako hivyo hivyo ila sasa ugumu ni kwenye mtazamo wao.
Mpaka leo ni wiki ya 3 kila jumamosi wanabadilisha watu wa kunitembelea lakini bado hawajanipa majibu ya kueleweka. Na mimi naendelea kuwasikiliza tu maana kila wakija wanaomba wakapitie vizuri na kuja kunielewesha 😅