Je, Mungu analo Jina? Jina lake ni lipi?

Je, Mungu analo Jina? Jina lake ni lipi?

Kazi kuu tatu za Mungu wa Mbinguni.

1. Kwenye uumbaji anajulikana kwa sifa ya Baba.
Baba ndiye mzalishaji wa viumbe.

Mathayo (Mat) 6:9
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,

2. Kwenye Ukombozi wa Wanadamu na Nguvu za Kimungu anajulikana kama Roho Mtakatifu.

Mathayo (Mat) 1:18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

3. Kwenye Ukombozi wa Wanadamu anajulikana kama Yesu Kristo Mwana wa Mungu.

Mathayo (Mat) 16:15
Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
Mungu ni mmoja tu

"Sema" alijidhihirisha kwetu kwa namna tatu alizopenda yeye.

Hili ni somo la Hekima ya Mbinguni.

Ona hapa Mungu anajigeuza kama ni Binadamu ili aongee na Nabii wake Ibrahim.

Hii ni kwamba akijidhirisha ktk Utukufu wake.
Mwanadamu akimtokea atakufa kwa ile nguvu yake ya Utukufu.
Ni kwamba Mwanadamu hawezi kuhimili kumwona Mungu katika umbo la Mwili wa Nyama.


Mwanzo 18
1 Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.

2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,

3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.

4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.

5 Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.

6 Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.

7 Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa.

8 Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.

9 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.

10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.

11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.

12 Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?

13 Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee?

14 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.

15 Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka.

16 Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize.

17 Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo,

18 akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?

19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.

20 Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,

21 basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.

22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.

23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu?

24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?

25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?

26 Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.

27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.

28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano.

29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.

30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.

31 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.

32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.

33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.
Mjadala unaenda vyema.

Jina la BABA ni lipi?

Jina la Mwana ni lipi?

Na Jina la Roho mtakatifu ni lipi?

Maana imeandikwa, hao watatu ni UMOJA. (1 Yohana 5:8).
 
  • Thanks
Reactions: 511
Unaniuliza mimi tena mjomba?

Yohana (Joh) 8:58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, {mimi niko}
Ndio nakuuliza wewe.

Litaje Jina la Mungu sawasawa na HOJA hapo juu🙏
 
  • Thanks
Reactions: 511
Mjadala unaenda vyema.

Jina la BABA ni lipi?

Jina la Mwana ni lipi?

Na Jina la Roho mtakatifu ni lipi?

Maana imeandikwa, hao watatu ni UMOJA.
Baba
Mwana
Roho Mtakatifu
Ni namna alivyojidhirisha kwa kazi kuu tatu alizozifanya

Sio Majina na sio viumbe vitatu.

Kazi ya uumbaji, Baba.

Kazi ya kutukomboa na kutupa nguvu ni Roho Mtakatifu.

Kazi ya kutukomboa na kutuhakikishia kurithi Ufalme wa Mungu ni Mwana, Yesu Kristo

Nadhani umeelewa hapa.

Sio viumbe vitatu.
Ni kazi zake kuu tatu dhidi ya Mwanadamu.

Mfano
Wewe ni Baba wa watoto wako pale Nyumbani.

Watoto wakija shuleni wewe unakuwa Mwalimu wao. Kazi yako ni Mwalimu. Pale huitwi Baba tena Bali Mwalimu.

Watoto hao hao wako ukikutana nao kwenye shida zao unakuwa Mshahuri wao.

Hivyo basi wewe kwa watoto wako ulio wazaa utakuwa

1. Baba
2. Mwalimu
3. Mshauri

Na utabaki kuwa mmoja na sio Watatu.

Hebu Soma hapa.


Isaya 9:6

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;

Naye ataitwa jina lake,

1.Mshauri wa ajabu,

2.Mungu mwenye nguvu,

3.Baba wa milele,

4.Mfalme wa amani.

Isaya hajasema majina yake.
Bali Jina lake.
Ingawa ukiangalia kwa haraka kuna viumbe wanne hapo

Hivi umeelewa hapo kweli?
 
Ndio nakuuliza wewe.

Litaje Jina la Mungu sawasawa na HOJA hapo juu[emoji120]
Jina si nimekuwekea hapo juu au wewe ni Juha?

Kutoka (Exo) 3:14
Mungu akamwambia Musa,
[emoji117]MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;
[emoji117]MIMI NIKO amenituma kwenu.

And God said unto Moses, I AM THAT I AM: and he said, Thus shalt thou say unto the children of Israel, I AM hath sent me unto you.
Au wewe ni Abunuwasi ?
 
  • Kicheko
Reactions: 511
anayo mengi
Mada inaomba kujua Jina la Mungu, Si Majina ya office za Mungu kumwakilisha nguvu uweza na mamlaka yake.

Ni sawa na mtu kukuita Baba Ukiwa nyumbani, Ofisini unaitwa manager, sokoni unaitwa mteja, ndani ya ndege unaitwa msafiri au Abiria.

Bt hayo Si Majina Yako, unalo Jina lako.

Litaje ikiwa unalijua.
 
Jina si nimekuwekea hapo juu au wewe ni Juha?

Kutoka (Exo) 3:14
Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.

And God said unto Moses, I AM THAT I AM: and he said, Thus shalt thou say unto the children of Israel, I AM hath sent me unto you.

Au wewe ni Abunuwasi ?
Litaje Jina la Mungu.

Ukiulizwa swali direct, jibu direct.

Ukiombwa evidence, unaleta evidence.

Lugha chafu Si mahala pake hapa 🙏
 
  • Masikitiko
Reactions: 511
Baba
Mwana
Roho Mtakatifu
Ni namna alivyojidhirisha kwa kazi kuu tatu alizozifanya

Sio Majina na sio viumbe vitatu.

Kazi ya uumbaji, Baba.

Kazi ya kutukomboa na kutupa nguvu ni Roho Mtakatifu.

Kazi ya kutukomboa na kutuhakikishia kurithi Ufalme wa Mungu ni Mwana, Yesu Kristo

Nadhani umeelewa hapa.

Sio viumbe vitatu.
Ni kazi zake kuu tatu dhidi ya Mwanadamu.

Mfano
Wewe ni Baba wa watoto wako pale Nyumbani.

Watoto wakija shuleni wewe unakuwa Mwalimu wao. Kazi yako ni Mwalimu. Pale huitwi Baba tena Bali Mwalimu.

Watoto hao hao wako ukikutana nao kwenye shida zao unakuwa Mshahuri wao.

Hivyo basi wewe kwa watoto wako ulio wazaa utakuwa

1. Baba
2. Mwalimu
3. Mshauri

Na utabaki kuwa mmoja na sio Watatu.

Hebu Soma hapa.


Isaya 9:6

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;

Naye ataitwa jina lake,

1.Mshauri wa ajabu,

2.Mungu mwenye nguvu,

3.Baba wa milele,

4.Mfalme wa amani.

Isaya hajasema majina yake.
Bali Jina lake.
Ingawa ukiangalia kwa haraka kuna viumbe wanne hapo

Hivi umeelewa hapo kweli?
Naelewa kabisa.

Kuna njia tatu za kujibu swali.

1. Kujibu Swali Kwa swali.

2. Kujibu Swali Kwa mkato.

3. Kujibu swali Kwa Kutoa maelezo.

Mada inataka ujibu swali Kwa mkato no 2. Simple and clear.

Karibu.
 
Yohana (Joh) 8:58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako,
[emoji117]MIMI NIKO


Jesus said unto them, Verily, verily, I say unto you, Before Abraham was, I am.
 
  • Thanks
Reactions: 511
Mada inaomba kujua Jina la Mungu, Si Majina ya office za Mungu kumwakilisha nguvu uweza na mamlaka yake.

Ni sawa na mtu kukuita Baba Ukiwa nyumbani, Ofisini unaitwa manager, sokoni unaitwa mteja, ndani ya ndege unaitwa msafiri au Abiria.

Bt hayo Si Majina Yako, unalo Jina lako.

Litaje ikiwa unalijua.
Nilitaje mimi tena?
Hivi una akili wewe kweli?

Kutoka (Exo) 3:14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;

[emoji117]{MIMI NIKO} amenituma kwenu.

And God said unto Moses, I AM THAT I AM: and he said, Thus shalt thou say unto the children of Israel,
[emoji117] {I AM} hath sent me unto you.
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Yohana (Joh) 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako,
[emoji117]{MIMI NIKO}

Jesus said unto them, Verily, verily, I say unto you, Before Abraham was,
[emoji117]{I AM}
 
Kwa Ukristo.
Mungu ni cheo cha juu anatambulika kama Jehovah.
Yesu ni nguvu kuu ya utendaji iliyo ndani ya Mungu.
Thus huwezi kemea pepo kwa jina la Mungu bali Yesu.
Shetani anaogopa jina la Yesu na sio Jehovah.
Yesu siyo nguvu za Mungu,Yesu ndiye kiumbe wa kwanza kuumbwa huko mbinguni hata kabla ya kuja duniani,nguvu za Mungu zinaitwa roho takatifu, katika kusali linatumika jina la Yesu kwakuwa yeye ndiye mpatanishi wa binadamu na Mungu kupitia dhabihu yake, ukitaka ushahidi wa maandiko karibu tuelimishane mkuu
 
Unamzungumzia huyu Mungu aliepigwa mitama na Yakobo?

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Hapana, ni yule anayetoa mabikira 72 na kutengeneza vijito vya pombe😂 ili waja wake wakalabuke na kuloweka

Afu cha ziada sasa, hao mabikira 72 wote wana miaka 9 sasa, si unajua tena ndio sampuli anazopenda mtume wake mpendwa😂 a.k.a Kibabu Mudi kipenda vitoto
 
Hilo pia ni Moja ya Jina la office au mamlaka ya Mungu, Si Jina lake personal tulilofinuliwa WANADAMU.
Hapana,Mungu maana yake ni muweza yote sio jina binafsi, ndiomaana Kuna maandiko yanayomwita shetani Mungu wa Dunia hii,lakini Yehova ndiye jina pekee la kibinafsi la Mungu wa kweli,soma 2wakorinto4:4 "ambao kati yao mungu wa mfumo huu wa mambo amezipofusha akili za wasio amini,ili Nuru ya habari njema ya utukufu kuhusu Kristo aliyemfano wa Mungu,isiwaangazie" Hapo utaona shetani ameitwa Mungu pia,ila Yehova ndiyo jina halisi la Mungu.
 
Musa alimuuliza, unaitwà nani? Akajibu

"MIMI NIKO, AMBAYE NIKO"

(I AM, WHO I AM)

hilo ndilo jina lake.
 
Salaam, Shalom!!

Mungu ni Jina la Cheo kikubwa kuliko vyeo na mamlaka yote Mbinguni na duniani.

Swali ni je, Mungu analo Jina lake binafsi?

Jina la Mungu ni nani?

Karibuni 🙏
Kiebrania anaitwa YHWN
Kimasai anaitwa NGAI
Kichaga anaitwa NJARO
Kiluguru anaitwa MLUNGU
Kinyakyusa anaitwa KYALA
Kiswahili ndo huyo MUNGU

Jina lake binafsi lipo karibia makabila yote ya ulimwengu huu
 
Kiebrania anaitwa YHWN
Kimasai anaitwa NGAI
Kichaga anaitwa NJARO
Kiluguru anaitwa MLUNGU
Kinyakyusa anaitwa KYALA
Kiswahili ndo huyo MUNGU

Jina lake binafsi lipo karibia makabila yote ya ulimwengu huu
Hapo unachanganya Majina ya miungu,

Njaro ni Jina la miungu ya wachaga ambaye wao humpa pombe ya mbege kama shukrani.

Ndomana tunataka kulijua Jina la Mungu binafsi mwenye mamlaka ya juu kuliko mamlaka zote za Duniani na Mbinguni.

Litaje Jina lake ikiwa unalifahamu.
 
Back
Top Bottom