Mungu wapo wengi so lazima ujue kutofautisha maana kuna mizimu ni Mungu na wanaabudiwa, kuna majini ni Mungu,kuna vitu ni Mungu, kuna watu ni Mungu.
Hata Moyo wa mwanzo aliyepewa kusimamia uumbaji (mwanzo 1:1) ni Mungu na aligawanyika katika nafsi za Miungu tisa mitakatifu ikiwemo
1.Mwenyezi
2.Yehova
3.Mungu wa majeshi
4.Mungu wa daudi
5.Mungu wa danieli
6.Mola
7.Aliyetuma wote
8.Mungu wa roho za manabii
9.Mungu wa eliya
Lakini kutokana na uumbaji kutekwa nyara na ufunuo,nyoka na vita (ufunuo 12:1-9) Muumba aliyekuwepo kabla ya chochote (warumi 11:36) alisema katika
1korintho 15:24-28
24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
25Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.
28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana (Yesu) mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Mwisho ni mjumuiko wa waliotumwa wote ukijumlisha na huyo Moyo wa mwanzo (mwanzo 1:1)ambao ndio walikuwa na Mwanzo na Mwisho (Mungu wa majira saba)
Ila Muumba ni mmoja jina ni Mungu Baba na ndiye CHANZO HALISI (warumi 11:36, kolosai 1:17) hana mwanzo wala mwisho.
Ndiye anayesema katika
zekari 14:9
Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
So Muumba ni mmoja na jina ni moja, hayo mengine ni nafsi za waliotumwa japo wengi wamefundishwa ndo huyohuyo na mifumo ya mapokeo.