Je Mungu anaweza kuwa Mungu; Je mtu anaweza kuwa Mungu?

Tuachane na ulimwengu ,Je binadaamu na viumbe vingine vilitokeaje? Na kwanini vikawa Ke na Me kama vilizuka tu?
Hakuna anayesema vilizuka tu.

Hakuna jibu la uhakika wa 100% ambalo limepatikana mpaka sasa linaloweza kuthibitisha chanzo cha binadamu ni nini.

Lakini kukosa majibu hakutoi mwanya wa kuruhusu majibu mengine ambayo hayajapitia uchunguzi kuwa ndio chanzo cha binadamu.
 
Hivi mkuu mambo ya Quantum nikitaka pata ile basics yake tu naanzia wapi
 
Hivi mkuu mambo ya Quantum nikitaka pata ile basics yake tu naanzia wapi
Alafu mi huwa naanglia sana clip za mambo ya quantum physics, kama unatumia tiktok kuna account moja inaitwa scixlab na quatum theory ni nzuri mno kwa clip fupi fupi au ukiangalia video za brian cox na science talk ya neil degrasse tyson
 
Reactions: Lax
Alafu mi huwa naanglia sana clip za mambo ya quantum physics, kama unatumia tiktok kuna account moja inaitwa scixlab na quatum theory ni nzuri mno kwa clip fupi fupi au ukiangalia video za brian cox na science talk ya neil degrasse tyson
Hao kina cox na degrasse nawapata sema kwenye hizo mada ndo hua natoka sifuri aisee, ngoja nianze na hizo basics ulizo sema
 
Hao kina cox na degrasse nawapata sema kwenye hizo mada ndo hua natoka sifuri aisee, ngoja nianze na hizo basics ulizo sema
Ila ina mambo mengi kwenye zile particle ni nyingi mno mpaka zinachanganya
 
Reactions: Lax
Ukristo na Uislamu ni nusu tu ya dunia,

Ni kweli — Ukristo na Uislamu si dunia yote, ni sehemu yake tu.

Lakini hoja haikuwa wingi wa waumini, bali aina ya Mungu anayezungumziwa.

Hoja ilikuwa hii: Kuna dini nyingi Lakini si zote zinazungumzia Mungu muumba, asiye na mwanzo, asiye na mfano Ukristo (kwa asili ya Agano la Kale) na Uislamu zinadai Mungu wa aina hiyo

Kwa hiyo: Idadi ya waumini si sawa na ukweli wa dhana . Swali linabaki kuwa la hoja, si la kura:

JEE MUNGU AWEZA KUWA MTU ; JEE MTU AWEZA KUWA MUNGU ?????????​

Hilo ndilo lililokuwa linajadiliwa.
 

Kanuni si “kila kitu kina chanzo”, bali “kila kitu kilichoanza kuwepo kina chanzo.”

Ulimwengu ulianza - unahitaji chanzo.
Chanzo cha mwisho hakijaanza - hakihitaji chanzo.

Ukisema hata chanzo hicho lazima kiwe na chanzo hapo utakuwa unaingia kwenye mfululizo usio na mwisho pia hapo ndipo hakuna kitu kingekuwepo leo

Kwa hiyo first cause si kukwepa kanuni, ni hitimisho la mantiki ili kuepuka mgongano.
 
Kama Mungu hawezi kuwa mtu, basi maana yake ni kwamba, kuna vitu Mungu haviwezi kuvifanya!!

Sasa hii pia inaleta mgongano wa kimantiki, kwamba Mungu ni muweza wa yote... Lakini mbona hili haliwezi? 🤔

Uweza wa Mungu haujumuishi mambo yanayojipinganisha kimaana.
Mungu hawezi kuwa asiye na mipaka na mwenye mipaka kwa wakati mmoja — si kwa udhaifu, bali kwa sababu hilo halina maana kiasili.

Kama vile:

2+2 siyo 5
au kusema mraba mviringo haupo

Kutoweza kujikanusha nafsi si upungufu wa uwezo, ni ukamilifu.
 
TATIZO LAKO NI KUSHINDWA KUWA NA AKILI YA KUJUA MTU NI NINI ..PIA MUNGU ANAWEZA KUJIGEUZA KITU CHOCHOTE AU KUTWAA TASWILA YA KITU CHOCHOTE ...HOJA YAKO NI SAWA NA USEME MUNGU AWEZI KUONGEA KIZARAMO AU KISWAHILI KWA SABABU NI MUNGU ....KUMBUKA KUWA KUONA NI MLANGO MMOJA TU WA FAHAMU ...MUNGU ANAWEZA KUJIDHIHILISHA KWA MILANGO YOYOTE YA FAHAMU KWA WANADAMU .
 
MAJIBU YA KISAYANSI KUHUSU MUNGU NI HAYA
1)ENERGY IS ABILITY OF DOING WORK.
2)YOU CAN'T DESTROY OR CREATE ENERGY....BUT ENERGY CHARGE FROM ONE FORM TO ANOTHER.
 

Hakuna anayekataa kwamba Mungu anaweza kujidhihirisha kwa namna anayotaka.
Hoja ni tofauti kati ya kujidhihirisha na kubadilisha asili.

Mungu anaweza kuzungumza Kiswahili au Kiarabu - hicho ni kitendo

Lakini kuwa Mungu asiye na mipaka halafu awe mtu mwenye mipaka - huo ni mgongano wa asili, si mlango wa fahamu

Kujidhihirisha: ni ujumbe unaofikishwa kwa binadamu

Kugeuka kuwa mtu: ni kubadilika asili (kutoka asiyehitaji na kuwa ni mwenye mahitaji)

Kwa hivyo : Mungu anaweza kujifunua kwa njia yoyote, lakini kujikanusha asili yake si uweza, ni kujipinga au kujipinganisha
 
Siyo Yesu tu hata Roho mtakatifu ni hivyo hivyo ni mungu ndani ya mwili wa binadamu wenye nafsi ya binadamu .
 
MAJIBU YA KISAYANSI KUHUSU MUNGU NI HAYA
1)ENERGY IS ABILITY OF DOING WORK.
2)YOU CAN'T DESTROY OR CREATE ENERGY....BUT ENERGY CHARGE FROM ONE FORM TO ANOTHER.

Energy si Mungu.

Ni kweli , Energy haipotei, hubadilika tu
Lakini Energy haina akili , Energy haina hiari , Energy haiweki sheria

Sheria ya “energy hubadilika” inatumika ndani ya mfumo uliopo, haijibu:

Kwa nini mfumo upo kabisa? Kwa nini kuna energy na sheria zake?


Kumfanya Mungu sawa na energy ni kuchanganya makundi (category error).

Energy hufanya kazi, lakini haiwezi kueleza chanzo, mpangilio, na kusudi.
 
Siyo Yesu tu hata Roho mtakatifu ni hivyo hivyo ni mungu ndani ya mwili wa binadamu wenye nafsi ya binadamu .

Hii ni tafsiri ya Utatu (Trinity), si hoja ya kifalsafa.

Yesu na Roho Mtakatifu wana asili ya kibinadamu na uhusiano na Mungu , Lakini kusema: “ni Mungu ndani ya mwili wa binadamu mwenye nafsi ya binadamu” hapo unazalisha mgongano wa kimaana:

Mungu ni asiye na mipaka na Binadamu ni mwenye mipaka, mahitaji, na mwanzo

Kwa hivyo , Kuunganisha asili zisizofanana (mungu asiye na mwanzo na binadamu mwenye mwanzo) haiingii akilini, ndiyo sababu baadhi ya waasisi wa Ukristo wa mwanzo waliikataa.

Kwa ufupi Utatu ni fumbo, si mantiki safi.
 
Energy siyo Mungu ni sahihi ila mungu naye ni Energy ..no energy no God
 
Inatokana na form ya energy, mfano light ni aina ya energy pia inaweza kuwa kama paricles na particles zina behave, hivyo behaviour ni some kind of intelligence
 
Trinity ni tafsiri potovu ya madhehebuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…