Je! Mungu ni yule yule?

Tatizo wanachotaka kunijuza kina contradiction, na contradiction haijaondolewa.

Mimi nikikwambia kuna pembetatu yenye pembe sita katika Euclidean plane geometry, huijui tu, amini, utakubali ipo? Utaamini ipo?
 
Anakuwaje Agent wa shetani wakati hata huyo shetani aamini kama yupo.
Hapo sasa.

Mtu anayeamini Mungu yupo ana uwezo mkubwa wa kuwa agent wa shetani kuliko mimi nisiyeamini Mungu yupo.

Maana ukimuamini Mungu huyu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, na ukiamini vitabu vinavyoitwa vyake, basi utaamini shetani yupo.

Hapo umeshapiga hatua moja mbele yangu mimi ambaye siamini Mungu wala shetani wapo.
 
Tatizo wanachotaka kunijuza kina contradiction, na contradiction haijaondolewa.

Mimi nikikwambia kuna pembetatu yenye pembe sita katika Euclidean plane geometry, huijui tu, amini, utakubali ipo? Utaamini ipo?
Tatizo ni kwamba hautaki kusikia kuamini(imani) ila unajadili suala la imani ya uwepo wa mungu. Hata patolewe maelezo ya aina gani ila mwisho utataka upewe uthibitisho usio na shaka wa kuwa mungu yupo.

Na hapo ndipo hii mijadala inapokwama.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Brother mungu hakushindwa kuwafanya watu wote wakawa watiifu kwake aliweza na anaweza na ataweza ila alicho kifanya ni kutupa muongozo wa vitabu na manabii ili watujuze njia sahihi ya maisha kisha akatupa uhuru hakumtoza mtu nguvu kifuata kwa vile ameshatoa muongozo, kwa hiyo kuwepo kwa matatizo duniani huu ni mtihani tu kwetu kipimwa nani atafaulu
 
Yaani brother mungu yupo kabisa, ata maumbile yako ulivyo umbwa yana thibitisha kama mungu yupo hujataka kufikiri vzur tu
 
Hivi jamani kama maumbile yamekuja nature bila kuumbwa na mungu mbona yana mfanano, kwa mfano binaadam wote tuna maumbile yaliyofanana, wote tuna macho pua mdomo na yote yapo kichwani hoja yangu ipo hapa kwanin hii nature haikufanya macho yakawa makalioni, kwanin pua haikukaa kwenye nyayo kwanin tunatia chakula mdomoni lkn kinatoka mk...... jamani ndo kweli nature imefanya yote haya maana ukijiangalia mwanaadam ulivyoumbwa kwa ustadi lazma ujue kama yupo alie kuswarif hivyo kiranga vp
 
Kiranga, nadhani bado hujanielewa khs mfano wa jua na kivuli. Ni kama useme hivi, haiwezekeni jua lenye kuangaza sayari zote kuanzia Mercury mpaka Pluto iwepo endapo kuna kuna kivuli. Haiwezekani jua lenye kuangaza kote lenye mwanga mkuu lenye kuweza kumulika sayari zote 9 iwepo wakati kuna kivuli. Kwako ww uwepo wa kivuli ni uthibitisho tosha kwamba jua halipo.

Kitu hicho najua huwezi kikubali kwa kua utaonekana hau-make any sense kama ambavyo kwako ww uwepo wa evil na God's existence usivyo-make sense, but the fact still stands, evil doesn't disprove God's existence.

We all know that the sun exists, no matter how many shadows are there. Existence of shadows doesn't disprove the existence of sun, rather it confirms the existence of the sun.
Kwa nini niamini hivyo? Kwa nini nithamini kuamini katika ulimwengu unaotaka kujua?

Kwa nini niamini contradiction?

Kwa nini niamini kuna pembetatu yenye pembe sita?

Hujaondoa contradiction katika idea ya kuwepo kwa Mungu wako.
 
Rafiki yangu kiranga sasa umewezaje kutambua mema na mabaya
Hili ni swali ambalo halijibiki kabisa endapo utasema hakuna Mungu. Tunaamini kwamba there is the source of morality and the source of absolute truth throught which we define any wrong. Huwezi sema kitu flan ni kibaya kama huna reference. Vinginevyo kuua ingekua ni kitu kibaya kwako kwa wengine ni kizuri, but wote tunaona kwamba kuua ni kitu kibaya.

Lakini labda tumuulize Kiranga, je unadhani Hitler ambaye aliua wayahudi zaidi ya mili0ni 2 alitenda haki kuwaua au hakutenda haki. Kama hakutenda haki unatumia reference gani kutoa jibu hilo?

All morality must come from the supreme provider of it, who Institutes that this is wrong and this is right. You can choose to deviate from it, nobody will bother, but the law still stands.
 
Tatizo ni kwamba hautaki kusikia kuamini(imani) ila unajadili suala la imani ya uwepo wa mungu. Hata patolewe maelezo ya aina gani ila mwisho utataka upewe uthibitisho usio na shaka wa kuwa mungu yupo.

Na hapo ndipo hii mijadala inapokwama.
Hujajibu swali nililokuliza.

Unaamini pembetatu yenye pembe sita ipo?
 
Hata swali nililouliza hujalielewa, sijauliza kama Mungu alishindwa kuwafanya watu wote wawe watiifu kwake.

Kama hujaelewa swali, sitegemei uweze kulijibu.

Sijauliza kama Mungu alishindwa kuwafanya watu wote wawe watiifu kwake, nimeuliza kama Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Utiifu hata kama watu wote wakiwa watiifu leo, halafu matetemeko ya ardhi yakaendelea kuua watoto wachanga wasio na hatia, nikauliza, imekuwaje huyo Mungu mnayemsema ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya kama haya matetemeko yanawezekana wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hayawezekani kutokea?

Hili swali halina uhusiano wowote na utiifu.

Na hujalijibu.
 
Mfano wa jua na kivuli hauna contradiction, hivyo hauna swali lisilojibika.

Mfano wa Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, kutoumba ulimwengu huo, na kuumba ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana, una contradiction, hivyo una swali.

Unafananisha "pembe tatu yenye pembe tatu tu" (kitu ambacho hakina contradiction, jua na kivuli) na "pembe tatu yenye pembe sita" (kitu ambacho kina contradiction).

Viwili hivi havifananishiki.

Sijui hata kama unaelewa contradiction ni nini?

Unavyojibu ni kama mtu ambaye haelewi contradiction ni nini.
 
Bado hujanijibu swali langu, kama jua linaloangaza kote lipo, mbona kuna kivuli/vivuli. Nipe jibu, vinginevyo JUA HALIPO. Haiwezekani jua liangaze mpk Pluto halafu kuwe na vivuli kwenye sayari yetu duniani.

Hivyo ndio ambavyo ww unang'ang'ania kwamba kama Mungu muweza yote yupo mbona kuna uovu.?? Unapewa jibu kwamba uwepo wa uovu haumaanishi kwamba Mungu hayupo, ila hutaki kuelewa unakomaa kwamba haiwezekani. Na unaweza kukomaa kwa kuwa una free will, unless otherwise ungeakua unaamini ulichopangiwa kuamini
 
Kwa nini unauliza swali la jua na kivuli? Swali lako halina mantiki, kwa sababu nataka kufananisha jambo ambalo halina contradiction, jua na kivuli, na jambo lenye contradiction, Mungu na ulimwengu.

Nachelea hujui contradiction ni nini na umuhimu wake hapa.

Nikikwambia kivuli kipo kwa sababu mwanga wa jua hauwezi kupita vikingo vyote, ndiyo maana mwanga wa jua ukikingwa panatokea kivuli, utasemaje?

Sasa huyo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hakuna kinachoweza kumkinga na kutotimiza anachotaka na alichotaka.

Aalikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kutokea.

Ninaposema mabaya siongelei mabaya yanayotokana na watu tu.

Naongelea mpaka habari za natural disasters kama matetemeko ya ardhi yanayoua maelfu ya watoto wachanga.

Huyo Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote, kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Jua lina sababu ya kushindwa kuangaza kote, halina uwezo wote, ujuzi wote wala upendo wote.

Mungu wenu mnayesema ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote excuse yake ni nini?
 
Ok, tuachane na mfano wa jua na kivuli. Lets assume kwamba THERE IS NO GOD. I have one question for you, what is the source of life and diversity of all life forms of Earth??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…