Kwa nini unafikiri uanasiasa ni kitu ninachotaka mpaka kuweka jitihada? Unajuaje kwamba sijakimbia kazi za kunifanya niwe mwanasiasa?
Tatizo letu si kwamba maneno mengi, tatizo letu watu wanapoogopa maneno mengi.
Hakuna maendeleo bila maneno mengi, hata kama ni kwa minajili ya kuyachuja tu.
Kwa hiyo usiniambie habari za kujitahidi ili niwe mwanasiasa, nimeanza kutembea corridor za Ikulu on a daily basis tangu niko tumboni mwa mama yangu na mpaka leo kuna mzee wa familia yangu yupo baraza la mawaziri la Magufuli, ningetaka habari za siasa ningekuwa ndani yazo miaka 20 iliyopita. Nimezikimbia.
Sasa kama kuna Mungu, muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, kwa nini kawaumba hao watu akiwa na udhaifu na matamanio, halafu wakianguka kwa sababu ya udhaifu na matamanio aliyowaumba nayo, Mungu huyo awadhibu?
Wwewe mzazi unaweza kumtoboa macho mwanao ashindwe kuona, wakati unaweza usimtoboe akaona, halafu mwanao ashindwe kujua kusoma kwa sababu haoni, halafu umuadhibu kwa sababu hajui kusoma?
Kama baba mtu tu, asiye na upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote hawezi kufanya hivi, kufanya hivi ni jambo baya sana, imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote afanye hivyo hivyo?
Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao viumbe wake hawawezi kupata udhaifu wala matamanio?
Mbona mahakama zisizo na mfungamano na dini yoyote zinatoa hukumu kwa aliyeua?
Mbona hata jamii inatoa hukumu kwa aliyeua? Mbona Wakomunisti ambao hawakuamini Mungu walitoa hukumu kwa walioua?
Hii ni logical non sequitur. Umeunganisha vitu ambavyo haviunganishiki.
Ukimbaka mwanao sheria za nchi zitakufunga, huhitaji Mungu hapo.
Ukiendekeza hilo hata kisiri mwanao akapata mimba, sheria za asili zitakuhukumu, utapata mtoto ambaye ni mjukuu ambaye ana matatizo ya genetics.
Huhitaji Mungu kushitakiwa kwa kosa hili.
Na wala sielewi kwa nini unashindwa kuelewa kwamba kosa hili lina hukumu zimewekwa kisheria, katika nchi ambayo sheria ni secular, haziongozwi kidini.
Ssa hapo kigumu cha kuelea kipi?