Je! Mungu ni yule yule?

Hujaondoa contradiction ya problem of evil.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.
 
Kitendo cha Mungu kubadilika badilika kisikuchanganye saana, kwasababu Mungu wetu sio sanamu

Miungu isio badilika ni sanamu pekee
 
Kwa nini yahitaji mpaka nife?

Mungu huyo alishindwa kuweka mazingira ya kumthibitisha kwamba yupo kabla ya kufa?
Kwanini haujibu swali nalokuuluza?

Ukifa ndipo yale yanayoelezwa kuhusu mungu yatajulikana ukweli wake,kwa sasa suala la kuhusu uwepo wa mungu linabaki imani(wapo watakao amini na wasioamini) ila baada ya kufa ndiyo tutaweza kuthibitisha.

Ni kama vile ulivyokuwa unashindwa kuthibitisha sauti unayoisikia njee hadi utoke njee.
 
Wewe ulikwisha kufa na kuhakikisha ukifa kunatokea nini?

Au unapiga stories tu?
 
Wewe ulikwisha kufa na kuhakikisha ukifa kunatokea nini?

Au unapiga stories tu?
Unaniuliza swali hilo kwa msingi gani? Wewe ulitaka kujua kwanini hadi ufe?nimeshajibu ni kwanini hadi ufe,sasa hayo ya kwamba mie niliwahi kufa au sijawahi kufa ni mada nyengine kabisa.
 
Unaniuliza swali hilo kwa msingi gani? Wewe ulitaka kujua kwanini hadi ufe?nimeshajibu ni kwanini hadi ufe,sasa hayo ya kwamba mie niliwahi kufa au sijawahi kufa ni mada nyengine kabisa.
Hujajibu swali la kwanini hadiufe na kwaninikusiwe na uthibitisho kabla ya kufa.

Umeandika haya chini nanukuu


Umerudia tu kusema "ukifa ndipo yale yanayoelezwa kuhusu mungu yatajulikana..."

Hilo sijibu la swali langu. Nimekuuliza, kwanini yale yanayoelezwa kuhusu Mungu yatajulikana baada ya kufa tu, na hayajulikanikablaya kufa?

Unanijibu "ukifa ndipo yale yanayoelezwa kuhusu mungu yatajulikana...".

Nakuuliza "kwa nini pi ni 3.14?" Unanijibu "pi ni 3.14".

Hujajibu swali, umelirudia kulisema swali lile lile tu na kujifanya umelijibu.
 
Kwenye imani ya uwepo wa mungu kunaelezwa suala la kufufuliwa na kuhukumiwa,hayo ni machache kati ya yale yanayoelezwa.

Sasa ili hayo yatokee ni lazima tufe kwanza,ni sawa na wewe ambaye upo ndani halafu unasikia sauti nje na ukaamini ni sauti ya gari,lakini ili iwezekane kuthibitika hilo kuwa ni sauti ya gari kweli unapaswa kutoka nje kwa sababu nyumba haina madirisha.
 
Kwa nini Mungu kafanya nilazima tufe kwanza ili tuweze kuthibitisha?

Kwa nini tusiwezekuthibitisha kabla ya kufa?

Hujajibu swali hili zaidi ya kutumiahabari ya imani fiat tu.

Mtu mwingine anaweza kukuambia habari hiyo niuongo, ndiyo maana watu wameweka insurance policy ya kwamba huwezi kuthibitisha mpaka ufe, wakijua hakuna anayekufa na kurudi kuhadithia.
 
Ni sawa na mie nikuulize kwanini hiyo nyumba(ambayo unasikia sauti ya gari kwa nje) haina madirisha? Kwanini hiyo nyumba isingekuwa na madirisha ili uweze kuthibitisha ukiwa ndani kwa kuangalia dirishani?

Sidhani kama swali hilo lingekuwa linahusika na kutaka kujua kwanini umeshindwa kuthibitisha sauti ya gari nje ukiwa ndani. Sasa na wewe umeuliza kwanini hadi tufe ndiyo tuweze kuthibitisha,nikakujibu ila ajabu unakuja kuuliza tena kwanini mungu afanye hivyo na asingefanya iwezekane(isiwe imani tena) kuthibitisha bila ya kufa.
 
Ni sawa na mie nikuulize kwanini hiyo nyumba(ambayo unasikia sauti ya gari kwa nje) haina madirisha? Kwanini hiyo nyumba isingekuwa na madirisha ili uweze kuthibitisha ukiwa ndani kwa kuangalia dirishani?

Hata ingekuwa na madirisha,anayekataa kuinuakichwa kutazama nje atakuwa anakataa kuhakiki na kubaki na imani, mfanounabakipale pale.

Hujajibu swali langu,kwa nini nilazima kusubiri kufa ili kuthibitisha?


This point is moot after my input above. Tatizo unadhani sana, huhakikishi unachodhani.
 
Ulichojibu hapa sijui hata kama wewe mwenyewe unakielewa,tatizo wanaokusifia unajua kujenga hoja na kuuliza maswali magumu wanakupumbaza sana.

Na ndiyo maana hapa badala ya kusoma na kuelewa unasoma ili tu uulize maswali ambayo unahisi ni magumu na nitashindwa kujibu.

Kwa kifupi nimeeleza tu kuwa ulichoniuliza hakihusiani na kutaka kujua kwanini hadi ufe ndiyo uthibitishe,sasa hebu angalia ulichojibu wewe!
 
Hujaondoa contradiction ya problem of evil.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.
Mungu huamua vile atakavyo na katika anayoamua hakosei..jibu lipo hapo.
 
Mungu huamua vile atakavyo na katika anayoamua hakosei..jibu lipo hapo.
Hilo si jibu.

Hapo umekubali hujui jibu.

Sijakataa unavyodai kwamba Mungu wako huamua atakavyo. Sijasema kuna mtu anamuamlia.

Ninekuuliza, kwa nini akaamua kuumba ulimwengu wenye mabaya mengi, unaowezekana kuwa na matetemeko ya ardhibyatakayoua watoto wachanga nabkuachavwazazi wao na huzuni, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna matetemeko hayo?

Hujui jibu. Hujui sababu. 7nasemanMungu huamua atakavyo.

Nitakupa mlolongo mzima wa wewe kushindwa kujibubswali hili.

Umeshindwa kujibubswali hili kwa sababu huna jibu.

Huna jibu, kwa sababu hakuna jibu la kimantiki linaloeleweka.

Hakuna jibubla kimantiki linaloeleweka , kwa sababu Mungu hayupo.

Kushindwa kwako kunibubswali hili kunaonesha unamuamini Mungu usiyemuelewa.

Humuelewi kwa sababu haeleweki.

Haeleweki kwa sababu hayupo.

Hayupo kwa sababu dhananya kuwepo kwake inajipinga yenyewe, hivyo, hawezi kuwapo.
 
Mungu huamua vile atakavyo na katika anayoamua hakosei..jibu lipo hapo.
Kwa jibu kama hilo mtu yeyote anaweza kuhalalisha uongo na ujinga wowote.

Naweza kukuambia kuna pembe tatu yenye pembe sita ambayo imekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Kiev kesho.

Ukaniuliza, kwanza pembetatu itakuwaje na pembe sita halafu pembetatu hiyo yenye pembe sita itakuwaje Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, halafu mbona Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa si Kiev Ukraine, halafu mbona habari za kesho unasema kama zimeshatokea tayari?

Nikikwambia "pembe tatu yenye pembe sita imeamua vileitakavyo na katikakuamua inavyoamua haikosei", jibu lipo hapo, nitakuwa nishakujibu jibu kamilifu.

Hujajibu kitu, umekubali hujuij ibu, kwa sababu hakuna jibu, kwa huyo Mungu wako hayupo.

Habari za kuwepo kwake zina contradiction kama habari za kuwepo kwa pembe tatu yenye pembe sita katika plane Euclidean geometry.
 
Tusiende mbali kiranga(politician) nakuuliza swali je unaamini kwamba kunamaisha baada ya kufa?
 
Tusiende mbali kiranga(politician) nakuuliza swali je unaamini kwamba kunamaisha baada ya kufa?
Sitaki habari za kuamini, niambie unachojua.

Kuamini unaruhusiwa kuamini uongo wowote, katiba ya Tanzania inakupa uhuru wa kuamini ujinga wowote mradi huvunji sheria.

Universal Declaration of Human Rights iliyotangazwa December 10 1948 inakupa haki ya binadamu kuamini chochote.

Mimi natetea uhuru wako wa kuamini unachotaka.

Sijadili imani hapa, najadili facts.

Tuongelee facts.
 
Kiranga amani ya Bwana wetu Yesu iwe pamoja nawe?Ndugu yangu bado tu hujampokea Yesu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…