Kama kitu hakipo. Unaanzia wapi kuthibitisha kwamba hakipo?
Uthibitisho wa aina gani utakufaa kuonesha kwamba kitu hakipo?
Nikikwambia pembetatu yenye pembe sita ipo, ila wewe huijui na huna akili za kuiona tu (wakati kwa kweli haipo), utanithibitishiaje kwamba haipo?
Aliyeua kwa kisu unaweza kutoa ushahidi wa alama za vidole zake ukasema huyu kaua kwa kisu, kisu kimepatikana eneo la mauaji kina damu, kina alama zake za vidole, jeraha lililoua limetokana na kisu hiki, huyu ambaye alama zake za vidole zipo kwenye kisu hana alibi.Zaidi kuna video imemrekodi akiua. Zaidi, nyumba ina alarm na ikajifunga milango, polisi wakaja wakamkuta muuaji ndani. Jirani walimuona dirishani akiua.
Overwhelming evidence. Huyu kaua.
Sasa kama hakuna aliyeua kwa kisu, utathibitishaje kwamba hakuna aliyeua kwa kisu wakati hakuna maiti, hakuna kisu, hakuna alama za vidole?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kama alivyoandikwa katika vitabu vya Biblia na Quran, hayup
Hayupo kwa sababu, dhana nzima ya kuwepo kwake, inajipinga yenyewe.Contradiction.
Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe, kwa sababu, kwa upande mmoja, Mungu huyu ni mtakatifu sana kiasi kwamba kibaya chochote hakiwezi kutoka kwake. Kwa maana hiyo, angekuwepo, dunia isingewezekana kuwa na mabaya. Ukisema aliumba dunia isiwe na mabaya ila Shetani ndiye akaleta mabaya, nitakuambia hata huo uwezo wa Shetani kuweza kuleta mabaya ni ubaya ambao Mungu mwenye utakatifu unaosemwa hatakiwi kuwa nao.
Kwa hiyo, utaona kwamba, kuwepo kwa mabaya, na zaidi, kuwezekana kuwepo kwa mabaya katika dunia hii, ni uthibitisho kwamba Mungu huyu hayupo.
Wengine wamejaribu kujibu kwa kusema Mungu kaachia mabaya ila katupa uwezo wa kuchagua mabaya na mazuri. Hili ni jibu lisilo na mantiki. Ukiwa na mtoto wako mchanga ambaye uelewa wake ni mdogo sana, na wewe una helewa mkubwa sana kujilinganisha naye, unampenda, utampa chupa ya maziwa na pembeni umuwekee chupa ya sumu ili tu aweze kuchagua anachotaka? Hapana. Utahakikisha nyumba nzima haina sumu anayoweza kuifikia. Utampa maziwa tu.
Sasa kama binadamu mwenye uwezo mdogo, upendo mdogo na ujuzi mdogo anakataa kumpa mtoto wake mchanga maziwa na sumu ili mtoto awe na uhuru wa kuchagua, imekuwaje Mungu huyu mnayemsema mwenye uwezo usio na mwisho, ujuzi usio na mwisho na upendo usio na mwisho ameruhusu ulimwengu uwe na mazuri na mabaya ili watu wawe na uhuru wa kuchagua tu?
Watu kama wangeumbwa katika dunia ambayo haiwezekani kuwa na mabaya na mabaya hata hayajulikani, in fact hayapo kabisa hata kidhana, wangekosaje uhuru wa kitu ambacho hakijulikani wala kufikirika wala kuwepo kidhana tu?
Huyu Mungu yupo kweli au hadithi tu?
Kaachia dunia yenye magonjwa, vita, matetemeko, mafuriko, njaa, umasikini, kuteseka etc, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hivyo vyote haviwezekani watu wakaishibraha mustarehe.
Kwa nini?
Sijajibiwa jibu la kueleweka kwenye swali hili.
Kama kitu hakipo. Unaanzia wapi kuthibitisha kwamba hakipo?
Uthibitisho wa aina gani utakufaa kuonesha kwamba kitu hakipo?
Nikikwambia pembetatu yenye pembe sita ipo, ila wewe huijui na huna akili za kuiona tu (wakati kwa kweli haipo), utanithibitishiaje kwamba haipo?
Aliyeua kwa kisu unaweza kutoa ushahidi wa alama za vidole zake ukasema huyu kaua kwa kisu, kisu kimepatikana eneo la mauaji kina damu, kina alama zake za vidole, jeraha lililoua limetokana na kisu hiki, huyu ambaye alama zake za vidole zipo kwenye kisu hana alibi.Zaidi kuna video imemrekodi akiua. Zaidi, nyumba ina alarm na ikajifunga milango, polisi wakaja wakamkuta muuaji ndani. Jirani walimuona dirishani akiua.
Overwhelming evidence. Huyu kaua.
Sasa kama hakuna aliyeua kwa kisu, utathibitishaje kwamba hakuna aliyeua kwa kisu wakati hakuna maiti, hakuna kisu, hakuna alama za vidole?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kama alivyoandikwa katika vitabu vya Biblia na Quran, hayupo.
Hayupo kwa sababu, dhana nzima ya kuwepo kwake, inajipinga yenyewe.Contradiction.
Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe, kwa sababu, kwa upande mmoja, Mungu huyu ni mtakatifu sana kiasi kwamba kibaya chochote hakiwezi kutoka kwake. Kwa maana hiyo, angekuwepo, dunia isingewezekana kuwa na mabaya. Ukisema aliumba dunia isiwe na mabaya ila Shetani ndiye akaleta mabaya, nitakuambia hata huo uwezo wa Shetani kuweza kuleta mabaya ni ubaya ambao Mungu mwenye utakatifu unaosemwa hatakiwi kuwa nao.
Kwa hiyo, utaona kwamba, kuwepo kwa mabaya, na zaidi, kuwezekana kuwepo kwa mabaya katika dunia hii, ni uthibitisho kwamba Mungu huyu hayupo.
Wengine wamejaribu kujibu kwa kusema Mungu kaachia mabaya ila katupa uwezo wa kuchagua mabaya na mazuri. Hili ni jibu lisilo na mantiki. Ukiwa na mtoto wako mchanga ambaye uelewa wake ni mdogo sana, na wewe una helewa mkubwa sana kujilinganisha naye, unampenda, utampa chupa ya maziwa na pembeni umuwekee chupa ya sumu ili tu aweze kuchagua anachotaka? Hapana. Utahakikisha nyumba nzima haina sumu anayoweza kuifikia. Utampa maziwa tu.
Sasa kama binadamu mwenye uwezo mdogo, upendo mdogo na ujuzi mdogo anakataa kumpa mtoto wake mchanga maziwa na sumu ili mtoto awe na uhuru wa kuchagua, imekuwaje Mungu huyu mnayemsema mwenye uwezo usio na mwisho, ujuzi usio na mwisho na upendo usio na mwisho ameruhusu ulimwengu uwe na mazuri na mabaya ili watu wawe na uhuru wa kuchagua tu?
Watu kama wangeumbwa katika dunia ambayo haiwezekani kuwa na mabaya na mabaya hata hayajulikani, in fact hayapo kabisa hata kidhana, wangekosaje uhuru wa kitu ambacho hakijulikani wala kufikirika wala kuwepo kidhana tu?
Huyu Mungu yupo kweli au hadithi tu?
Kaachia dunia yenye magonjwa, vita, matetemeko, mafuriko, njaa, umasikini, kuteseka etc, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hivyo vyote haviwezekani watu wakaishibraha mustarehe.
Kwa nini?
Sijajibiwa jibu la kueleweka kwenye swali hili.
Ipo tofauti kubwa kujadili HULKA/TABIA ya Mungu na swali letu la msingi "Je Mungu yupo? Pembe tatu ipo lakini siwezi kuitafuta kwenye pembe sita. Kisichokuwepo kabisa hakina jina wala hakijadiliwi. Pembe tatu ipo vile pembe sita ipo. Labda ungetolea mfano wa kitu ambacho hakina jina wala umbo. Kitu kingine cha kushangaza unanukuu Biblia "Mungu ni mtakatifu sana, ana upendo, ana nguvu" ambayo huiamini kuwa ni ya Mungu (ambaye hayupo) lakini ikusaidie kupinga!
Dunia iliumbwa kamilifu. Mungu mara baada ya kumaliza kazi yake ya uumbaji alisema "kila kitu ni chema sana" (Mwanzo 1:31). Mahusiano yake na binadamu wa kwanza yalikuwa mazuri bila dosari yoyote hadi pale dhambi ilipoingia duniani. Katika Mwanzo 3:17 ardhi ikalaaniwa na mateso yakaaingie duniani (Warumi 8:19-21). Aidha, Mwanzo 6:5-7 Mungu akaghairi kwa nini alimwumba mwanadamu kwa kuwa kila aliloliwaza moyoni mwake lilikuwa ovu.
Maswali mengine unayouliza humu si mimi wala wewe mwenye majibu kamili. Kama hilo la uhuru wa kuchagua ni kosa, basi hilo wote hatuna majibu. Ni sawa na chungu kumwuliza mfinyanzi kwa nini niko hivi. Mwanadamu hakuubwa kama roboti. Kwani upendo ungejulikana vipi pasi na hiari ya kuchagua kupenda ama la? Aidha, Mungu angepima vipi upendo wa wanadamu pasi na hiari hiyo?
Wakati mwingine tunalalamika sana kuhusu mabaya duniani. Lakini kuna faida yake. Moto una faida na hasara kwa mwanadamu. Lakini, ebu fikiria iwapo sharti yangu imeshika moto, alafu sina maumivu yoyote! Mwisho wangu ni kifo. Maumivu hunisaidia kubaini tatizo. Ugonjwa wa moyo vilevile.
CHANZO & MATOKEO YAKE
Moja ya mambo ya msingi sana ambayo akili ya binadamu zinaweza kuhoji ni swali la “Je! Mungu yupo?” Pengine Mungu yupo au hayupo. Haiwezekani majibu mawili yote kuwa sahihi. Asiyeamini Mungu (a
theist) kwa ujasiri anadai kwamba hakuna Mungu; naye aaminiye Mungu (
theist) kwa ujasiri anasema Mungu yupo;
mnostiki anasema kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai hayo; na mwenye kushuku (
skeptic) anatilia shaka iwapo uwepo wa Mungu unaweza kuthibitishwa pasi na shaka yoyote. Ni yupi aliye sahihi? Je! Mungu yupo ama hayupo?
Ni dhahiri, njia pekee ya kujibu swali hili, ni kuutafuta na kuuchunguza ushahidi uliopo. Hakika ni sahihi kusema kwamba ikiwa Mungu yupo, basi angetupatia ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha uwepo wake. Je! upo ushahidi huo?
Anayeamini Mungu (
theist) anashikilia kwamba upo ushahidi wa kutosha kabisa kuthibitisha kwamba Mungu yupo. Hata hivyo, tunapotumia neno “thibitisha,” hatuna maana ya kusema kwamba uwepo wa Mungu unaweza kubainika kisayansi kwa njia moja sawa na ambavyo mtu anavyoweza kuthibitisha mfuko wa viazi wa kilo kumi au kwamba moyo wa binadamu umegawanyika katika chemba nne ndani yake. Vitu kama kupima mfuko wa mboga, au aina za misuli, ni mambo ambayo tunaweza kuyathibitisha kupitia milango mitano ya fahamu. Na mbali ya kwamba maada (matters) huthibitishwa kupitia milango ya fahamu na mara nyingi njia hii husaidia sana katika kuhakiki usahihi wa jambo, lakini hiyo si njia
pekee ya kuhakiki jambo.
Kwa mfano, mamlaka zote kisheria zinatambua uhalali wa kile kinachojulikana kama ushahidi unaojitokeza mwanzoni mwa tukio (
prima facie case). Jambo kama hilo hubainika panapokuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha uwezekano wa jambo hilo kuwa na ukweli, isipokuwa kama sababu za msingi za kulipinga vinginevyo, unahesabika kuwa ni ushahidi tosha. Hoja ya wanaomwaamini Mungu ni kwamba pana ushahidi mwingi sana wa kutosha unaoibuka mapema kabisa (
prima facie case) ambao ni msingi imara juu ya uwepo wa Mungu – suala ambalo ni vigumu kulipinga. Tungependa kuwasilisha hapa sehemu ya ushahidi huo ambao unathibitika mapema madai yenyewe husika ya kuwepo kwa Mungu.
CHANZO NA MATOKEO – HOJA YA KOSMOLOJIA
Katika zama zote za historia ya mwanadamu, moja ya hoja iliyojadiliwa kwa ufanisi mkubwa kwa habari ya uwepo wa Mungu ni hoja ya kosmolojia (chanzo na matokeo), ambayo hubainisha ukweli kwamba Mifumo ya Sayari iliyopo hivi sasa ni lazima itolewe maelezo.
Mifumo ya Sayari ipo na ni halisi kabisa. Kila mtu anayejenga hoja kimantiki – ikiwa ni pamoja na hao wanaopinga uwepo wa Mungu na hao wanostiki – hawana budi kukubaliana na ukweli huu. Lakini swali huibuka, “Mifumo ya Sayari imetokea wapi?” Ikiwa hakuna kitu kinachoweza kujiumba chenyewe, basi hoja ni kwamba hakijatokea kwa “nasibu” kwa kuwa uwepo wake hutengemea kitu kingine. Kwa hiyo, Mifumo ya Sayari, haiwezi kujiumba yenyewe au kujieleza ilivyotokea. Ikiwa Mifumo ya Sayari haikujiumba yenyewe, hapana budi pawepo na chimbuko lake.
Hapa ndipo Sheria ya Chanzo na Matokeo huingiliana kabisa na hoja hii ya Mifumo ya Sayari. Hadi hapa jinsi maendeleo ya elimu ya sayansi yanavyozidi kustawi, sheria za asili hazitoa vighairi (
exceptions). Hivi ndivyo ilivyo hasa Sheria ya Chanzo na Matokeo, ambayo kwa dunia nzima ndiyo yenye uhakika zaidi katika sheria zote. Unaweza kusema, Sheria ya Chanzo na Matokeo hubaini kwamba kila panapotokea matokeo fulani lazima pawepo na chanzo hasa kilichosababisha (yaani, chanzo kilichotangulia matokeo).
Hapawezi kuwepo na vitu bila kuwa na chanzo kinachojitosheleza. Aida, vyanzo haviwezi kamwe kuja
baada ya matokeo. Haiwezekani kabisa kusema kwamba vyanzo vilitokea baada ya matokeo, au matokeo hutangulia vyanzo vyake. La nyongeza, matokeo hayawezi kuwa na uwezo zaidi ya kiini chake. Ndio maana wanasayansi wanasema kila panapokuwepo na vitu lazima pawe na chanzo
kinachojitosheleza. Mto hauwezi kugeuka kuwa matope kwa sababu tu chura amerukia ndani ya mto; wala kitabu hakiwezi kudondoka toka mezani kwa sababu tu inzi amepepea juu yake. Hivyo si vyanzo vinavyojitosheleza. Kwa maana kila athari tunayoiona, lazima tupendekeze chanzo kinachojitosheleza – na hili linaturejesha nyuma katika swali letu la msingi: Ni chanzo kipi
kimesababisha kuwepo kwa Mifumo ya Sayari?
Inawezekana tukapata majibu matatu kutokana na swali hili: (1) Mifumo ya Sayari ni ya milele; imekuwepo daima; (2) Mifumo ya sayari si ya milele; lakini ilijiumba yenyewe pasipo chochote; au (3) Mifumo ya Sayari si ya milele, badala yake iliumbwa na kitu fulani (au mtu fulani) aliye nje na mifumo hiyo, na aliye mahiri zaidi ya mifumo yenyewe. Hatuna budi kuyachambua majibu haya matatu.
Je! Mifumo ya Sayari ni ya Milele?
Moja ya msimamo unaomliwaza sana mtu asiyeamini Mungu ni dhana ya kwamba Mifumo ya Sayari imekuwepo hapa daima, na ya kwamba daima itakuwepo, kwa sababu dhana kama hii huepusha si tu tatizo la ilivyoanza au mwisho wake, bali pia haja ya kuwepo kwa “mwasisi wa kwanza” (kwa mfano Mungu). Lakini, sayansi hivi sasa inatambua kwamba Mifumo ya Sayari si ya milele; ina mwanzo wake, na ina hatima yake.
Miongoni mwa sheria thabiti na zilizojizatiti barabara ni sheria za mwendojoto
(thermodynamics). Sheria ya Kwanza ya Mwendojoto (mara nyingi hujulikana kama sheria ya kuhifadhi nishati na/au maada) inasema kwamba si maada (
matter) au nishati (
energy) inaweza kuumbwa au kutokomezwa isiwepo kabisa. Sheria ya Pili ya Mwendojoto (inayojulikana kwa kawaida kama Sheria ya Mparanganyiko) inadai kwamba kila kitu kinapungua nguvu au kuchakaa. Nishati inazidi kupungua na kuwa adimu kwa matumizi. Mparanganyiko (kigezo cha kutofuata utaratibu wake maalumu, kwenda mrama, au utaratibu kuvurugika) unazidi kuongezeka). Maana yake ni kwamba, hatimaye, Mifumo ya Sayari “itachoka.” Sheria ya Pili inabaini hivi (1) mwanzo, hapo awali kabisa, Mifumo ya Sayari ilikuwa katika hali ambayo ilikuwa na nishati ya kutosha kwa matumizi; na (2) hatimaye hapo baadaye nishati yote itatoweka (wanasayansi wanakitaja kipindi hicho kama “kifo cha joto –
heat death”), itakayosababisha Mifumo ya Sayari “kutoweka.” Kwa maneno mengine, mifumo ya sayari ni mithili ya saa kubwa iliyojazwa, lakini saa hiyo inazidi kupungua nguvu kadiri muda unavyoenda. Hitimisho kutokana na data za kisayansi haliepukiki – Mifumo ya Sayari si ya milele. Vitu vya milele havina mwanzo au mwisho, na “havichakai.” Mwanasayansi mmoja mashuhuri, Robert Jastrow wa NASA (asiyemwaamini Mungu), aliandika hivi: Sayansi ya hivi sasa hupingana na Mifumo ya Sayari kuwa ni ya milele.” Yuko sahihi kabisa. Hivi sasa kisayansi tunatambua kwamba Mifumo ya Sayari haijakuwepo hapa milele.
Je! Ulimwengu ulijiumba Wenyewe Pasipo Kitu?
Hapo nyuma, ingekuwa vigumu sana kumpata mwanasayansi maarufu ambaye angekuwa tayari kutetea hoja hii kwamba Mifumo ya Sayari ilijiumba yenyewe. Kila mwanasayansi, hata kijana mdogo, anaelewa ukweli kwamba hakuna kitu kinachoweza “kujiumba chenyewe.” Mifumo ya Sayari
imeumbwa, na wala si
imejiumba yenyewe. Hadi kufikia hivi karibuni, tofauti za mawazo zimeibuka juu ya jambo hili. Lakini, kuna ushahidi mwingi unaothibitisha kwamba Mifumo ya Sayari ina mwanzo (na chanzo hicho ni mahiri zaidi kuliko matokeo) ambayo baadhi ya wanasayansi wasioamini hudai kwamba Mifumo ya Sayari ilijiumba yenyewe pasipo kitu!
Kimsingi, madai kama hayo huonekana kuwa ni ya kijinga, kwa sababu misingi ya sheria za fizikia hubaini kwamba haiwezekani kabisa kuunda kitu pasipo kitu. Na hivyo kama inavyoonekana, hao wasiomwaamini Mungu wamekuwa tayari kulitetea hili. Hakika, mchango huu wa mawazo, ni upotoshaji wa wazi wa Sheria ya Kwanza ya Mwendojoto, inayosema kwamba si maada (matter) wala nishati tunaweza kuiumba upya au kuitokomeza isiwepo kabisa. Mnajimu Robert Jastrow alisema hivi, “Kuumba maada pasipo kitu ni kuzibomoa dhana sahihi zilizopo kisayansi – Sheria ya Uhifadhi Maada na Nishati – inayosema kwamba maada na nishati haviwezi kuumbwa au kutoweshwa visiwepo kabisa. Maada inaweza kubadilishwa kuwa nishati, kinyume chake pia ni sahihi, lakini kiwango chote cha maada na nishati katika Mifumo ya Sayari hubakia daima kile kile. Ni vigumu kuikubali dhana inayokinzana na kanuni thabiti zilizothibitika wazi kisayansi. Aidha, sayansi msingi wake ni katika utafiti, makala sahihi, data jarabati/zilizofanyiwa majaribio (
imperical data). Lakini tunapowataka watupatie data jarabati zinazothibisha madai kwamba Mifumo ya Sayari imejiumba yenyewe pasipo kitu, wasioamini hao hulazimika kukubali kwamba hakuna ushahidi kama huo. Mifumo ya Sayari haikujiumba yenyewe. Dhana kama hiyo ni ya kijinga, katika nyanja mbili zote kifalsafa na kisayansi.
Je! Mifumo ya Sayari Iliumbwa?
Ama Mifumo ya Sayari ina chimbuko lake, ama la. Lakini ushahidi mwingi uliopo unaonesha dhahiri kwamba Mifumo ya Sayari ina chanzo chake. Ikiwa Mifumo ya Sayari ina chanzo, kiini chake ama la. Walakini, jambo moja ni hakika: nalo ni sahihi–kimantiki na kisayansi – kukiri kwamba Mifumo ya Sayansi ina chimbuko lake, maana Mifumo ya Sayari ni matokeo na ikiwa hivyo ni sahihi, hapana budi pawepo na chanzo kinachojitosheleza. Hata hivyo, ni dhahiri kabisa, ya kwamba hakuna matokeo yaliyo makubwa kuzidi chanzo chake.
Kwa kuwa ni dhahiri kwamba Mifumo ya Sayari si ya milele, kadhalika ni kweli kwamba Mifumo ya Sayari haiwezi kujiumba yenyewe, basi hoja pekee iliyobaki ni kwamba Mifumo ya Sayari
iliumbwa na kitu, au Mtu fulani, ambaye: (a) alikuwepo kabla yake – ndio kusema, kitu hicho ni cha milele, kitu cha Kwanza Kuwepo bila chenyewe kuumbwa; (b) yeye ni bora kuliko kiumbe chake– kwa kuwa kiumbe hakiwezi kuwa bora kumzidi muumbaji; na (c) asili yake ni tofauti – kwa kuwa kina mipaka, maada tegemezi ya Mifumo ya Sayari haiwezi kujitolea maelezo yenyewe.
Katika kuliweka hili sawa, hapana budi kuangalia ukweli mwingine. Kama paliwahi kutokea nyakati ambapo hapakuwa na kitu
chochote kabisa, basi pasingekuwepo na kitu chochote kwa sasa, kwa sababu siku zote ikiwa hakuna kitu chochotee basi hakuna kitakachozaliwa. Katika kuliangalia hili,
kwa kuwa kwa sasa kitu kipo, basi kinachofuata kimantiki ni kwamba palikuwa na kitu fulani kilichoishi milele!
Kila kitu ambacho binadamu anajua kipo tunaweza kukigawa katika ama
maada au
akili. Njia nyingine haipo. Hoja hapa ni hii:
1. Kila kitu kilichopo kwa sasa ama ni maada (matter) au akili (mind).
2. Hivi sasa kipo kitu hapa, hivyo basi kuna kitu ambacho kimekuwepo milele.
3. Kwa hiyo, ama ni maada au akili ni ya milele.
A. Ama maada au akili ni ya milele,
B. Maada si ya milele, kwa ushahidi ulioainishwa hapo juu.
C. Kwa hiyo, ni akili iliyo ya milele.
Au tukichambua kwa njia nyingine tofauti:
1. Kila kitu kilichopo sasa ama ni tegemezi (ndio kusema, ili kiwepo hutegemea kingine) au kinajitegemea (si tegemezi).
2. Ikiwa ulimwengu si wa milele, ni tegemezi (ili uwepo hutegemea kingine).
3. Mifumo ya Sayari si ya milele.
4. Kwa hiyo, Mifumo wa Sayari ni tegemezi (ili iwepo hutegemea kingine).
A. Ikiwa Mifumo ya Sayari ni tegemezi, ni lazima ililetwa hapa na kitu fulani ambacho kinajitegemea.
B. Lakini Mifumo ya Sayari ni tegemezi (hutegemea kingine kuwepo).
C. Kwa hiyo, Mifumo ya Sayari iliumbwa na kitu fulani cha milele, nguvu inayojitengemea (isiyotegemea kingine kuwepo).
Hapo nyuma, wanamabadiliko wanaopinga uwepo wa Mungu walidokeza kwamba akili ni kazi tu ya ubongo, ubongo ambao ni maada; basi akili na ubongo ni kitu kimoja, na maada ndio pekee iliyopo. Lakini, mtazamo huo hauna mashiko tena kisayansi, kutokana na sehemu kubwa ya utafiti wa Mwanasaikolojia Mweustralia Sir John Eccles. Dr. Eccles, aliyetunukiwa tunzo ya Nobel kutokana na utafiti wake kuhusiana na jinsi gani sehemu fulani ya ubongo hufanya kazi (inayojulikana “
neural synapses”), aliainisha kwamba akili ni zaidi ya ubongo. Alionesha kwamba eneo linalosaidia mota (
motor) ya ubongo linaweza kuchochewa na
azma tu ya kutenda jambo fulani, bila ya kutumia gamba la nje la mota (ambalo husimamia mienendo ya misuli). Kilichotanguliwa kutajwa hapo awali (mtunza maktaba) hazidiwi nguvu na hicho cha pili (maktaba). Eccles aliainisha kanuni na hitimisho lake kisayansi katika kitabu kinachojulikana
The Self and Its Brain, ambacho alikiandika akishirikiana na Mwingereza mashuhuri mwanafalsafa za kisayansi, Sir Karl Popper.
Basi, kisayansi, ni hiari kudai kuwepo kwa maada pekee au kuwepo kitu kingine zaidi ya maada katika mpangilio murua katika Mifumo ya Sayari. Kwa hiyo, tofauti kati ya modeli hizi mbili ni kati ya: (a) muda, nafasi, na asili ya kumiliki maada; au (b) usanifu, uumbaji, na mpangilio bayana na akili dhahiri. Kiuhalisia, linapotajwa jambo hili, yanatolewa aina mbili tu ya maelezo kisayansi yanayotaja asili ya mpangilio murua katika Mifumo ya Sayansi na uhai unavyopatikana katika Mifumo ya Sayari: ama utaratibu
umewekwa katika maada, au utaratibu ndani ya maada
umeibuka wenyewe bila ya msanifu.
Kwa hao ambao wako tayari kusema kwamba utaratibu umeibuka wenyewe ndani ya maada, tunawajibu kwa kusema hivi hatujawahi kushuhudia mahali popote jambo kama hilo. Aidha, kukosekana kwa ushahidi kisayansi na kifalsafa ni majibu tosha na ya wazi kabisa kuwepo kwa Akili ya milele inayojitegemea, ambayo iliumba Mifumo ya Sayari na kila kitu kilichomo.
Kadiri wenye kushuku wanavyojitahidi, hawajawahi kutoigusia Sheria ya Chanzo na Matokeo iliyowazi. Lakini, hilo halijawazuia kujaribu tena bahati yao, na hivyo wamejitahidi kutoa sababu nyingi zinazokinzana na hilo. Kwa mfano, moja ya hoja inasisitiza kwamba dhana hiyo si kweli kwa kuwa inajipinga yenyewe. Mjadala wao unasema kama ifuatavyo. Kanuni ya chanzo na matokeo husema kwamba kila kitu lazima kiwe na chanzo. Katika dhana hii, vitu vyote vinaelekea kuwepo kwa Chanzo cha Kwanza, lakini ni wapi ghafla chanzo kilikosa chanzo. Lakini kwa jinsi gani ya kuelezea hili? Kwa nini kanuni hii inadai ya kwamba “kila kitu lazima kiwe na chanzo” na ghafla inashidwa kuwa na mashiko? Kwa nini basi hicho kitu kinachujulikana kuwa ndicho Chanzo cha Kwanza kisiwe na aina fulani ya chanzo chake? Ikiwa kila kitu au jambo linahitaji maelezo, au kuwa na chanzo, kwa nini basi Chanzo cha Kwanza pia kisiwe na maelezo, au chanzo chake? Ikiwa chanzo hicho hakipaswi kutolewa maelezo, kwa nini, basi, vitu vingine vyote vinatolewa maelezo?
Tunaweza kutoa majibu mawili kutokana na mashitaka hayo dhidi ya sheria ya chanzo na matokeo. Kwanza, kimantiki haiwezekani kutetea dhana yoyote ile ya “inayorejelea nyuma bila mwisho wake” (
infinite regress) inayodokeza mtiririko wa matukio yasiyo na mwisho na chanzo chake. Wanafalsafa wamelumbana vema kwa habari hii na kwa vizazi vingi. Hakuna kinachotokea pasipo kuwa na chimbuko lake. Chochote kilichopo lazima kiwe na chimbuko lake. Pasipo na chanzo basi hakuna kitachotokea.
Pili, madai yanayotolewa na hao wasioamini Mungu wakihoji kwamba Sheria ya Chanzo na Matokeo inakinzana yenyewe kwa yenyewe, hivyo basi haiitetei sheria husika; bali inakizana na
kauli potofu ya Sheria husika. Ikiwa mtu atasema, “Kila kitu lazima kiwe na chanzo,” basi ni sahihi kuipinga kauli hii. Lakini hayo siyo madai ya Sheria ya Chanzo na Matokeo. Sheria inadai kwamba kila
panapokuwepo na malighafi (material) hapana budi kuwepo na
chanzo chake kinachojitosheleza. Halafu, wakati fulani hapo nyuma kabisa lazima palikuwepo na Chanzo sahihi cha Kwanza kabisa ambacho kwa asili sio malighafi. Mungu sio malighafi.
HITIMISHO
Sheria ya Chanzo na Matokeo, na hoja ya kosmolojia inayoainishwa kutokana na sheria hiyo, inagusa kila nyanja ya maisha ya mwanadamu. Leo hii tuna Mifumo ya Sayari, na hivyo basi hapana budi pawepo na chanzo kilichotangulia kuwepo kinachojitosheleza.
Ili kubainisha hilo Sheria ya Chanzo na Matokeo, mwanasayansi mmoja, R.L. Wysong, alirejelea katika tukio la kihistoria lifuatalo. Miaka kadhaa iliyopita, wanasayansi walikutana Uingereza kujifunza sampuli ya safu murua za miamba duara yenye mashimo katikati – halafu utafiti wa wataalamu wa mambo ya kale wakaiita jina la ‘
Stonehenge’. Kadiri utafiti ulivyoendelea, ilibainika wazi kwamba sampuli hizo zilisanifiwa hasa kwa lengo la utabiri mbalimbali wa tabia za sayari. Maswali kadha wa kadha (kwa mfano, ni jinsi gani watu wa kale waliweza kuchunguza sayari, na ni jinsi gani walizitumia data walizozipata katika tafiti zao, n.k.) haijabainika bado. Lakini jambo moja tunajua kwa uhakika –
chanzo cha safu za miamba ‘
Stonehenge’ ni
usanifu uliotumia akili kuwepo na wala si kwa bahati nasibu.
Sasa, ebu tafakari hali ya safu za miamba ‘
Stonehenge’ ukilinganisha na Mifumo ya Sayari, na uhai uliomo ndani yake. Tunajifunza maisha, na utendaji kazi wake, ebu tafakari utata wake (ambao hapana hata watu wenye weledi mkubwa wanaoweza kuiga, hata kwa kutumia mbinu bora kabisa kisayansi na kiteknolojia), sasa tunahitimisha vipi? Kweli, pengine miamba ya
Stonehenge ilisababishwa na mmomonyoko wa ardhi, au nguvu za asili za majanga zikifanya kazi pamoja na vimondo ili kuunda safu za miamba na katikati kutengeneza mashimo. Lakini ni mwanasayansi au mwanafalsafa gani makini atakayeunga mkono wazo kama hilo?
Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayedai kwamba miamba ya
Stonehenge “imeizuka tu” kwa nasibu, ilhali watu wasioamini Mungu (
atheists), wagnostiki, na wenye kushuku hututaka sisi tuamini kwamba mpangilio huo murua, Mifumo ya Sayari iliyosanifiwa barabara (na utata wa uhai ulioishi ndani yake) “vimetokea kwa nasibu tu.” Kuiafiki dhana hii ni kukosa mantiki, kwa kuwa haina mashiko, na kwa sasa hakuna ushahidi wowote unaunga mkono hoja hiyo. Chanzo hicho [bahati nasibu tu] hakijitoshelezi kuleta matokeo hayo.
Aina hii ya tafakuri hailengi tu Mifumo ya Sayari, bali pia kwetu sisi tunaoishi humo. Yapo mambo ambayo ni dhahiri – uwezo wa kujenga hoja, uwezo wa kubaini mambo, uwezo wa kufikiri kimantiki. Lakini sifa hizi pambanuzi muhimu sana zilitoka wapi? Hakika dhana ya mabadiliko sahili kwenda tata (
evolution) haitoi majibu yanayojitosheleza. Kama alivyosema Norman Geisler: “Chanzo hakiweza kuzalisha kitu ambacho huzidiwa uwezo na kilichozalishwa. Ikiwa nimejaliwa akili au uwezo wangu wa kuelewa mambo, basi hapana budi pawepo na Akili au Mwenye Uwezo aliyenigawia mimi kidogo hiki nilichonacho. “Akili haziibuki pasipo akili; kitu fulani hakiwezi kuwepo pasipo kitu.”
Dr. Geisler yuko sahihi kabisa. Ikiwa wanadamu wana uwezo wa kutafakari, basi hapana budi pawepo na chanzo kinachojitosheleza ambacho kiko nyuma ya uwezo huo – chanzo kinachomiliki uwezo wa kutafakari. Ikiwa wanadamu tuna uwezo wa kubaini mambo (ndio kusema, kuna akili na mwili upande mwingine wa maumbile yetu), kadhalika lazima pawepo na chanzo kinachojitosheleza kikisimama nyuma ya uwezo huo – chanzo ambacho kina uwezo wa kutenda, na hutenda kwa mantiki.
Unaweza kusema, msingi wa hoja kuu ya kosmolojia, na Sheria ya Chanzo na Matokeo, ni hii: kila panapotokea kitu lazima pawepo na chanzo kinachojitosheleza ambacho kimekuwepo kabla ya matokeo. Leo hii Mifumo ya Sayari ipo; maisha yaliyosheheni akili yapo; uadilifu (
morality) upo, elimu ya maadili (
ethics) ipo, upendo upo. Ni nini chimbuko lake linalojitosheleza? Na kwa kuwa matokeo hayawezi kuwepo kabisa kabla ya matokeo au matokeo hayawezi kuzidi uwezo wa chanzo, basi ni sahihi kufikiri kwamba Chanzo cha maisha lazima kiwe kiumbe chenye akili iliyosheheni uadilifu, elimu ya maadili, na upendo. Biblia inapoandika hivi, “Hapo mwanzo, Mungu,” inatutaarifu sisi Chanzo hicho cha Kwanza kuwepo.