Soma Mathayo 2:23.
Dhehebu ni kikundi cha watu wenye mfumo wao mahususi wa imani na mienendo, hasa ndani ya au tofauti na jamii kubwa ya kidini.
Bila kuwa na kanisa, hivi alikuwa akiwahubiri akina nani?
Wakati wa kuanza kwa Ukristo, makanisa yalikuwa majumba ya watu. Filemoni 1:2; 1 Wakorintho 16:19; Warumi 16:4.
Kanisa ni mwili wa Kristu; uko kila mahali penye watu wampendao, hata kama hakuna jengo, kunaweza kuwepo kanisa la Kristu.
Alikuwa anahubiri nakuwapinga viongozi wa dini na madhehebu
Yohana alikuwa akiwapinga viongozi wa dini na viongozi wa madhehebu, waliokuwa hawafuati misingi sahihi ya dini.
Dini ni mfumo wa imani. Madhehebu yapo kwa sababu mfumo huo wa imani unatofautiana baina ya waumini wa dini moja.
Kwenye dini ya Ukristo, kwa mfano, kuna madhehebu ya Ukatoliki, Anglikana, Walokole, nk.
Uislamu una madhebu kama Washia na Wasuni.
Huwezi kupinga dini au dhehebu, then ukasema huna dhehebu au dini. Kwa sababu mtazamo au imani inayokuongoza kuzipinga zingine, hiyo ndiyo dini yako mwenyewe.
Hajawah kuingia kwenye makanisa yao
Alihubiri mitaani na mtoni
Siyo lazima uingie kanisani au kwenye sinagogi, ndipo uwe na dini au dhehebu. Tafadhali jielimishe kidogo kuhusu maana ya kanisa, dini, dhehebu, na imani.