Je, Mungu wa Wakatoliki amebadilika au Wakatoliki wamepata Mungu mwingine?

1 Wakorintho 2:13-15
[13]Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.

[14]Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

[15]Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.


Endelea kumtafuta mungu kwa macho
Au subiri unaweza ukamnusa siku
Ama kumsikia
Au kumuonja
Hisi zako tano hazitakusaidia kumjua
Inahitaji hisi ya sita.

Na pia unawes ukawa umewah kumuon mungu na ukampita
 
expand...
Bado unahubiri dini.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo, sihitaji mahubiri ya dini.
 
Bado unahubiri dini.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo, sihitaji mahubiri ya dini.
Jibu gani tena zaidi
Unataka nikamshike mkono nikuletee
Nimekupa maandiko mazuri kama ww ni mlengwa kuokolewa utaielewa
Ila kama ni mwana wa upotovu utaona ni maneno ya dini

Utakapojua chanzo cha uhai wa vitu vyote
Na asili ya vitu vyoote utajua kuna mungu
Kama maandiko ayo hayakutoshi

Au utaponambia source of nature and life ni nini
Basi nitakuonyesha mungu kutokea apo
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Umeleta maandiko yaliyoandikwa na watu tu, kutoka kwenye kitabu chenye makosa mengi sana ya kimantiki.

Nikikuwekea contradictions zilizomo katika Biblia, huwezi kumaliza kuzitatua hapa.

Bisha.
 
Bado unahubiri dini.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo, sihitaji mahubiri ya dini.
Unahisi nini?
Dunia kukaa kwnye mpangilio wake ni kwa sabab ya nini
Ama inakiwaje haitok kwnye orbit ni nini kiliweka sheria ya kushikiliwa kwenye mzunguko wake
Ama nn kilifanya jua liwe mchana na mwez usiku zikapokezana
Ama asili ga uhali wanyama na mimea uwepk wa jike na dume
Ukuaji wa mtoto tumboni
Uwepo wa maji katika njia zake na ardhi
Nyasi zisiote ote tu juu ya maji.
Bado mfumo wa mwili
Mizunguko ya damu, ubongo mmengenyk wa chakula na vyooooote

Ni sayansi iliviweka kwenye kanuni izo sio

Ni kitu kiliviratibu kikaviweka kwenye mpangilio wake


Utakaponijibu ilo basi kutokea apo nitakuonyesha mungu
 
Usome na hii
 
Mimi ni Mkatoliki, hata papa aseme ameruhusu huo upuuzi nitamchukulia kama binadamu wengine wenye dhambi. Kwa upande wangu ni bora aruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja ila sio ndoa za jinsia moja
 
Kanisa Katoliki haliabudu Sanamu bali linaabudu katika kweli, lakini kwa vile unachukulia vitu juu juu huwezi kuelewa hili.
Isaya 44:9-20
[9] Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.

[10] Ni nani aliyejichongea mungu mmoja, au aliyesubu sanamu isiyofaa kitu?

[11] Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja.

[12] Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kazi kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia.

[13] Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwa mfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani.

[14] Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha.

[15] Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia.

[16] Sehemu moja huiteketeza; kwa sehemu nyingine hula nyama; huoka chakula kiokwacho, akashiba; naam, huota moto, akasema, Aha, nimeota moto, nimeona moto;

[17] na kwa sehemu iliyobakia hufanya mungu, yaani, sanamu yake ya kuchonga; husujudu mbele yake akaiabudu, akaiomba, akasema, Uniokoe; maana wewe u mungu wangu.

[18] Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu.

[19] Wala hapana atiaye moyoni, wala hapana maarifa, wala fahamu kusema, Nimeteketeza sehemu motoni, naam, pia nimeoka mkate juu ya makaa yake; nimeoka nyama nikaila; nami, je! Kilichobaki nikifanye kuwa chukizo? Je! Nisujudie shina la mti?

[20] Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?
 

Duuuh,mbonna biology inakataa.
 

Huko ni kujifariji mkuu.
 
Hapo tatizo ni lugha, ila hakuna mabadiliko ya msimamo
 
amen
 
jana papa katangaza kwamba mashoga wana haki ya kubatizwa na kusimamia ndoa,,,kimsingi ushoga ni ruksa kwa katoliki
Kwa imani yako (sijajua ni ipi), wadhambi hawaruhusiwi kubatizwa na kuwa waumini safi wenye majukumu kanisani?
 
Alishawachoma moto lakini kumbuka Sodoma (sodomy) na Gomora
 
Mbona hapa hakuna kilichobadilika, na masuala yanayoongelewa ni tofauti.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni Mkatoliki, hata papa aseme ameruhusu huo upuuzi nitamchukulia kama binadamu wengine wenye dhambi. Kwa upande wangu ni bora aruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja ila sio ndoa za jinsia moja
Kuoa mke zaidi ya mmoja, hiyo ni zinaa. Dhambi moja haiwezi kufidia, kufuta au kuhalalisha dhambi nyingine.

Usalama wa Ukatoliki na waumini Wakatoliki ni kurudi kwenye Neno la kweli, na kuachana na mapokeo, mafundisho ya mabaraza na maamrisho ya papa.

👉^Ninyi mkikaa katika neno Langu, mmekuwa wanafunzi Wangu kweli kweli.^ Yohana 8:31.
 
Kwa imani yako (sijajua ni ipi), wadhambi hawaruhusiwi kubatizwa na kuwa waumini safi wenye majukumu kanisani?
Hapo wanaoingizwa humo katika mfumo Katoliki kama waumini ni mashoga 100%, wala sio waongofu wapya ambao zamani walikuwa mashoga wakaacha dhambi zao.

Wanaobatizwa kuwa waumini katika mwili wa Kristu ni watu ambao wamekubali kumpokea kama Bwana na Mwokozi wao, na kuacha matendo yao ya zamani ya giza.

👉Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe. Matendo ya Mitume 3:19

👉Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Matendo ya Mitume 2:38
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…