Je, Musa hakuandika kitabu cha Mwanzo??

Je, Musa hakuandika kitabu cha Mwanzo??

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Habari za jioni wana JF intelligence, natumaini wote wazima humu. Na kama kawaida nitoe angalizo kuwa mada ni sensitive sababu linagusa pia imani za wengine hivyo ningeomba tusome kwa makini tujiridhishe kwa tafiti binafsi kabla hatujachangia hii mada hivyo sitegemei watu waje na kejeli za kidini wala kukashifiana imani zetu maana uzi huu ni wa kuelimishana zaidi kuliko kukosoana. Kwa kusema hayo twende moja kwa moja kwenye mada. Na nitaigawa mara mbili ili tusome kwa urahisi.
images (56).jpg


UTANGULIZI
Kwa miaka mingi sasa kumekuwepo na imani kwamba kitabu cha mwanzo kimeandikwa na Nabii Musa na hata vile vitabu 5 vya kwanza kwenye biblia kwa ujumla wake vinavyoitwa pentateuch pia wengi tunaamini viliandikwa na Nabii Musa na watu wengi wanajikita kwenye mistari hii kuprove hilo

Yohana 5:46
46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.

Kutoka 17:14
14 BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua.

Mistari hii na mingine kama 20 kwa wengi inaonyesha kuwa kwa namna moja au nyingine vitabu 5 vya kwanza (pentateuch) ikiwemo Mwanzo iliandikwa na Musa. Imani hiyo ilivuka mpaka karne ya 20 ambapo baada ya elimu ya theolojia kusambaa dunia nzima,teknolojia na Elimu kwa ujumla kukua hivyo reasoning ya watu ikaongezeka ndio wakaanza kuhoji.

Waliibuka wasomi wa theolojia na dini mbalimbali kama Professor Julius wellhausen wa Ujerumani ambaye alikuja na nadharia ya Documentary hypothesis ambayo ilikuja kuzaa mjadala mkubwa kiasi kufikia karne hii ya 21 wanatheolojia wengi wanakiri kuwa Musa hakuandika kitabu cha mwanzo na pentateuch nzima kwa hoja tutakazoona hapo chini.

NB: Naomba ieleweke kwamba hakuna mahala kwenye maandiko ya biblia inaposema Musa aliandika kitabu cha mwanzo bali wote wanaongelea maandiko ya Musa ila sio vitabu kma vilivyopangwa kwenye Bible. Hivyo msimamo wa wanaopinga uandishi wa Musa ni kwamba, Musa aliandika mambo mengi ya wakati wake kwenye nyaraka kadhaa alafu wakaja waandishi wengine ambao walisoma nyaraka za Musa ndio wakajengea hoja zao ambazo zikazaa kitabu cha mwanzo na pentateuch nzima. Ni kama useme katiba pendekezwa draft yake iliandikwa na warioba ila sitta akaja kuifanyia editing, kuongeza maoni yake na maboresho hivyo ikatoka kuitwa rasimu mpaka kuitwa katiba pendekezwa. Hivyo kwa msimamo huu ni kwamba kitabu cha mwanzo kiliandikwa miaka 600 kabla ya Yesu ilihali Musa aliishi miaka takriban 1400 kabla ya Yesu ikimaanisha HAKUWA MUANDISHI WA KITABU CHA MWANZO.

DOCUMENTARY HYPOTHESIS
Nadharia hii inaamini kwamba kitabu cha mwanzo kiliandikwa na waandishi zaidi ya 4 ambao baadae wakaunganisha kazi zao na kutengeneza kitabu cha mwanzo. Wanawatenganisha watu hawa kwa kuangalia lugha iliyotumika, majina anayotumia, matamshi ya maneno ili kuprove walikuwa watu wanne walioishi vipindi tofauti kabisa. Mfano kitabu cha mwanzo kuna mistari inaongelea Musa kupewa sheria Mlima Horeb na kwingine inasema Mlima Sinai ikimaanisha mmoja wa waandishi aliishi baada ya kuwa jina mlima Horeb lilikwisha badilishwa na kuitwa Sinai and vice versa hivyo muandishi hawezi kuwa mmoja.

Kuna tofauti nyingi sana zimeorodheshwa kwa mifano na mwanatheolojia maarufu Mr Richard Friedman aliyeunga mkono nadharia hii unaweza soma hapa kwa upana wake tofauti zote.... Ningeomba msome hii document kabla hujachangia hii mada.

The Documentary Hypothesis Evidence


USHAHIDI WA KIMAANDIKO
232A-Image Moses Writing.jpg

Mwanzo 11:31

31 Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.

Hapa Mwandishi anamzungumzia Abraham kuwa anaishi kwenye mji wa Uru na akauhusianisha mji huo na kabila la wakaldayo. Lakini kwa ushahidi wa kiacholojia wakaldayo wameanza kuishi hapo Uru 1000 BC ilihali Musa aliishi miaka 1400 BC ikimaanisha kuwa mwandishi wa sura hii aliishi miaka mingi baada ya Musa ndipo akashuhudia wakaldayo wakiishi Uru hivyo akaandika habari za Abraham kuwa aliishi Uru ya wakaldayo kitu ambacho wakati wa Musa kabila hilo halikuwepo.
 
Mwanzo 14:14 mwandishi anaeleza kwamba Abraham aliwafukuzia wafalme wa mashariki waliomteka Lutu hadi kufikia mji wa DAN. Huu mstari pia unakubalika na wanatheolojia kuwa umeandikwa baada ya kifo cha Musa sababu wakati wote mji huo umeitwa Laish hadi pale kitabu cha waamuzi 18 ndio mji huo ulipewa jina la Dan ikimaanisha mwandishi wa kipande hiki aliandika haya miaka zaidi ya 600 baada ya Musa kufa. Mstari huu hapa

Waamuzi 18
Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; tena katika siku hizo kabila ya Wadani wakajitafutia urithi wapate mahali pa kukaa; maana hata siku hiyo urithi wao haujawaangukia kati ya kabila za Israeli.

Mwanzo 12:16
6 Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo

Mstari huu umeandikwa na mtu ambaye alikuwepo kipindi ambacho wakaanani walishafurumushwa Israel na Joshua kitu ambacho Musa hakukishuhudia kabisa maana mpaka anakufa waisrael hawakuwa wameingia Canaan na kuwafukuza wacanaan kabisa.

Kumb. La Torati 34
10 Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso;

Kwa mantiki hii haiwezekani ikawa imeandikwa na Musa mwenyewe wakati wake ilihali hakujua kma watatokea manabii wengine israel ni sawa na Rais Magufuli aseme Tanzania haikupata tena Rais kma yeye ilihali hatokuwepo kushuhudia maRais wengine hapo baadae.... Hii ikimaanisha mwandishi wa hapa aliishi miaka mingi baada ya Musa kutoweka dunia hivyo alishashuhudia manabii wengi wamepita ndio akahitimisha kuwa hakuna kama Musa.

Mwanzo 36:31
31 Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli.

Mstari huu unaonyesha mwandishi wa kitabu cha mwanzo alikuwa ameshuhudia Israel ikipata wafalme maana kipindi cha Musa israel haikuwa ina wafalme ila miaka kadhaa mbeleni ndipo wakapata mfalme wao hivyo Musa asingeweza kuandika hili ilihali hakuwa anafahamu kama israel ilishapata wafalme, hivyo aliyeandika hapa aliishi kipindi israel ilishapata wafalme ndio maana akaandika kwa msisitizo kuwa historia hii ni kipindi kile hawana wafalme bado.

Kumb. La Torati 34 inaelezea kifo cha Musa hivyo isingewezekana akawa ameandika Musa mwenyewe kuhusu kifo chake na maombolezo yake yalivyoenda hivyo wanatheolojia wanaona kuna mtu mwingine zaidi ya musa alieandika kipande hiki.

HITIMISHO
Kwa kuzingatia hoja hizi tunaweza hitimisha kwamba Musa hakuwa mwandishi pekee wa kitabu cha mwanzo ila mjumuiko wa waandishi wengi ambao walikuwa wamesoma nyaraka za Musa na wao kuongeza mawazo yao.

Na kama Musa aliandika basi inatuacha na maswali yafuatayo
1. Ni kwanini lugha inayotumika na misamiati na majina ya maeneo itofautiane kama mwandishi ni mmoja??

2. Pia kuna mistari inaonyesha Musa alikufa lakini bado maandiko ya pentateuch yaliendelea kuandikwa?? Je kivipi Musa aliweza andika akiwa kaburini??

3. Kama ni kweli vitabu hivi viliandikwa na mtu zaidi ya mmoja na wakaweka maoni yako je uhalali wa vitabu hivi kuwa kwenye Biblia ukoje??.

4. Je nini hatma ya Neno la Mungu kama kuna watu wanaweza ongeza maandiko yao kwenye Biblia..... Kwanini Mungu aliruhusu hili??

NB: Nimeuliza maswali haya kuchokoza mjadala ila sio msimamo wangu kupinga uandishi wa Musa, karibuni kwenye mjadala

Cc: Wana JF intelligence wote bila kuwasahau kina Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI Wick Kapwil Dukeson
 
mkuu hoja yako ni nzito sana na maswali hayo hapo juu ni magumu sana kuyajibu kwa sisi tuliofikishiwa maandiko na angalizo la kuyakubali pasipo mashaka na maulizo.
wazee wakanisa wameshasema vitabu 5 vya kwanza katika biblia vimeandikwa na musa, mpaka watakavyoamua vinginevyo ndio na sisi tutawasikiliza.


lakini mtoa mada naomba nikupongeze kutoka ndani ya moyo wangu kwani tokea nilipoanza kufuatilia mada zako hapa jf nimejifunza mengi mno ingawa kwa kweli nimepata changamoto kubwa sana kwenye imani yangu.
 
Musa alipokuwa mlima Sinai siku 40 Mungu alimweleza habari zote tangu mwanzo. Yaani alimweleza asili ya mwanadamu ilianzia kwa Adamu! Alimpa mtiririko wote jinsi mambo yalivyokuwa. Musa aliandika kile alicho ambiwa.
Hebu ngoja kwanza ,ina maana Musa alijua ,yote km mleta hoja alivyoanisha? Sikati alikua mlima Sinai siku 40, aliambiwa hadi mabadiliko ya miji na vitu vingine?

Hapa kuna Darsa na Ilmu zaidi ,nipo nimetulia kujifunza
 
Musa alipokuwa mlima Sinai siku 40 Mungu alimweleza habari zote tangu mwanzo. Yaani alimweleza asili ya mwanadamu ilianzia kwa Adamu! Alimpa mtiririko wote jinsi mambo yalivyokuwa. Musa aliandika kile alicho ambiwa.
Okay unaweza tusaidia yale maswali hapo juu kwa faida ya wasomaji wote waweze kuelewa sintofahamu hii
 
Kwanza maana halisi ya Mtume ni nini ? Kumbuka Yesu aliongelea mambo yaliyopita na yajayo. kwa hiyo Musa kipindi anawasilina na Mungu sio kwamba alipewa maagizo tu, fahamu kwamba Kuna vitu vingine alihitaji kufahamu hivyo alipewa nafasi ya kuuliza na akaelezwa. katika dhana kama hiyo Kama unatafakari kwa undani enzi hizo asingekua na cha zaidi ya kuuliza historia ya kufahamu chimbuko la wana Israel. pili, muda aliokaa mlima Sinai ni muda mrefu mpaka wafuasi wake waka kata tamaa, jiulize utakua ni muda gani watu wakate tamaa baada ya kutolewa kwenye vizuizi vya hatari na maajabu dhahiri na walikuwa wana msujudia Mungu wao kwa ukuu wake na miujiza mingi. hapa inaonyesha kwamba alichukua muda mrefu sana akiwa mlimani. pia kumbuka kwamba hawa Mitume walikua wanachaguliwa na mungu mwenyewe kuanzia utungaji wa mimba mpaka ukubwani, kwa hiyo karma waliyo kua nayo ilikua ni yake yeye mwenyewe Mungu kwa ajili ya kazi yake.
Ni kwa fikra zangu tuu.
 
Musa aliandika kwa sehemu hivi vitabu vya mwanzo kwenye magome ya miti ngozi za wanyama Kutokana na Mafundisho aliopewa na Mungu hi linajidhiirisha katika kitabu Cha kutoka 3:5-18 na pale anapojitambulisha Bwana Mungu kwamba yeye ni Mungu wa Baba yako Ibrahim Isaka na Yakobo kwaio Musa alifundishwa Na Mungu habari za Hawa baba zake na sababu hadi ilipofikia waisrael wapo pale Misri,kwaio Kwa sehemu kubwa maandiko aliyaandika Musa pamoja na wanafunzi wake anaweza akawa Yoshua na kalebu baada ya Musa kufa ambao pia waliandika katika magome yamiti ,ila baadae inawezekana baada ya miaka mingi kupita waandishi wakaja kuyakusanya na kuyaandika Kama historia,....ukiangalia hata injili sio kwamba ziliandikwa na wanafunzi wenyewe halisi wa Yesu Bali waliwasimulia wanafunzi wao wale wanafunzi ndo wakayaandika ila kwakua masimulizi ni ya wanafunzi wa Yesu wanatajwa Kama injili zao mfano ukisoma injili ya Yohana21:24 inadhiirisha wanafunzi wa yohana ndo waliandika injili hi ila kwa masimulizi ya Mtume Yohana mwenyewe
 
Back
Top Bottom