Je, Mwanamke Hubeba DNA za Wanaume Wote Aliowahi Kulala Nao? Mtazamo wangu ni huu

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Kuna kauli imekuwa ikisambaa sana mitandaoni siku hizi, kwamba mwanamke akishalala na mwanaume, hata kama hakupata mimba, basi hubaki na DNA yake mwilini. Wengine wanaenda mbali zaidi na kusema kuwa kama amekuwa na wanaume 5 au 10, basi anatembea na DNA zao wote, na huenda hata watoto atakaokuja kuzaa wakawa na tabia au muonekano unaofanana na wanaume hao wa zamani. Sasa swali la msingi linabakihii- ni kweli ya kisayansi au ni imani tu iliyojengeka?

Ukiangalia upande wa sayansi ya urithi, yaani Genetics, mtoto hupatikana pale ambapo yai la mwanamke linakutana na mbegu ya mwanaume mmoja tu. Hapo ndipo DNA za wazazi wawili zinachanganyika na kuunda mtoto. Hakuna mfumo unaoruhusu DNA ya mwanaume wa zamani kuja “kuingilia” mtoto wa mwanaume mwingine. Mfano rahisi ni huu: kama mwanamke alishawahi kuwa na mwanaume A miaka 3 iliyopita, halafu leo akapata mimba na mwanaume B, mtoto atakayezaliwa atachukua vinasaba kutoka kwa mama na mwanaume B pekeesio- A, wala C, wala mwingine yeyote aliyepita.

Chanzo cha mkanganyiko huu mara nyingi hutajwa kuwa ni kitu kinachoitwa Microchimerism. Hii ni hali ambapo seli chache sana za mtu mwingine zinaweza kubaki mwilini, mara nyingi kati ya mama na mtoto wakati wa ujauzito. Kwa mfano, mama anaweza kubaki na baadhi ya seli za mtoto wake kwa muda mrefu baada ya kujifungua. Lakini jambo la muhimu kuelewa hapa ni kwamba hali hii haimaanishi kubeba “DNA kamili” ya watu wengi kwa namna ya kuathiri watoto wa baadaye. Ni kiwango kidogo sana cha seli ambacho hakibadilishi urithi wa mtoto atakayezaliwa.

Ili kuweka wazi zaidi, fikiria mfano huu: kama kweli mwanamke angebeba DNA za wanaume wote aliowahi kulala nao, basi dunia ingekuwa na hali ya kushangaza sanamtoto- angeweza kuwa na mchanganyiko wa sura au tabia za watu ambao si wazazi wake kabisa. Lakini hali hii haionekani katika uhalisia wala haijaungwa mkono na tafiti za kisayansi. Watoto wanafanana na wazazi wao kwa sababu ya vinasaba wanavyorithi, si kwa sababu ya historia ya mahusiano ya mama.

Kwa hiyo hii dhana ya kwamba “uzae na mwanamke bikra ili kuepuka DNA za wanaume wengine” haina msingi wa kisayansi, bali inaegemea zaidi kwenye mitazamo ya kijamii na kitamaduni. Hii haimaanishi kwamba afya ya mahusiano haijalishikinachotakiwa- kupewa kipaumbele ni kujilinda dhidi ya magonjwa ya zinaa, kufanya vipimo, na kuwa na uaminifu katika mahusiano.

Mwisho wa siku, ni muhimu kutofautisha kati ya sayansi na imani. Sio kila kinachosambaa mtandaoni kina ukweli ndani yake. Elimu sahihi ndiyo inasaidia kufanya maamuzi sahihi.

Kwahiyo wanangu bikra sio kitu muhimu sana cha kufanya uogope kuanzisha familia na hawa second hand walio sokoni 😀😀😀
 
Wazo hili lina uzito zaidi kwenye fikra kuliko kwenye sayansi

Mwanamke habebi DNA za waliopita, bali hubeba kumbukumbu, hisia, na athari za uzoefu—na hizo ndizo ‘alama’ halisi za mahusiano.

Kwa maneno mengine, si mwili unaobeba wanaume wote…... ni nafsi

Kuna kipindi cha nyuma nilikuwa na yule binti then tunafanya uzinzi alitamka jina la mwanaume wake ambae alikuwa akiniambia ni rafiki yake.
 
Kwa upande wa nafsi athari ni kubwa mnoo
 
Mkuu unachanganya Vitu microchimerism ipo, lakini haiithibitishi telegony
 
Anabeba vinasaba vya mawazo, kuna alama inawekwa kichwani kwake ndo maana ni mara chache sana mwanamke atamuona mwanaume aliyewahi kushiriki naye tendo halafu asimtambue. Huwa wanakumbuka mpaka mikunjo waliyokunjwa siku husika.

NB: Wanawake wote huzaliwa na bikira. Kutoa bikira siyo mwisho wa matamanio yake, ni mwanzo. Hapo ndo tunasema GAME OON. Sasa hitimisha kuwa ukioa bikira umemaliza halafu likitokea la kutokea ushangazwe. Maadili ndo kila kitu, bila kujali hayo maadili kawa nayo kabla ya kutolewa bikira au baada.
 
Wazo hili lina uzito zaidi kwenye fikra kuliko kwenye sayansi

Mwanamke habebi DNA za waliopita, bali hubeba kumbukumbu, hisia, na athari za uzoefu—na hizo ndizo ‘alama’ halisi za mahusiano.

Kwa maneno mengine, si mwili unaobeba wanaume wote…... ni nafsi

Kuna kipindi cha nyuma nilikuwa na yule binti then tunafanya uzinzi alitamka jina la mwanaume wake ambae alikuwa akiniambia ni rafiki yake.
black joe!
unafahamu nini kuhusu male microchimerism au kwa jina lisilo rasmi Sperm-mediated microchimerism ?
 
Wazo hili lina uzito zaidi kwenye fikra kuliko kwenye sayansi

Mwanamke habebi DNA za waliopita, bali hubeba kumbukumbu, hisia, na athari za uzoefu—na hizo ndizo ‘alama’ halisi za mahusiano.

Kwa maneno mengine, si mwili unaobeba wanaume wote…... ni nafsi

Kuna kipindi cha nyuma nilikuwa na yule binti then tunafanya uzinzi alitamka jina la mwanaume wake ambae alikuwa akiniambia ni rafiki yake.
Nafsi Nafsi Nafsi, hapa unaweza ukawa upo sahihi.
 
Absorption ya DNA inafanyika sana tu. Tena sio hii pekee.
Pia kunakuwa na Energy exchange(trauma).. Soul ties..

Mantiki ya mzazi kuwa mungu wa pili, huanzia hapa.

Zile sifa (traits) ambazo zimehifadhiwa kwenye mwili wa mwanamke kama ni sehemu ya matokeo ya ngono, basi zitaenda kuathiri ukuaji wa kijusi...

Kuna kipindi mtoto anazaliwa, lakini mama mtu akiangalia kichanga anashindwa kuelewa ni cha mwanaume yupi, anasubiri kikue ili kuipata sura au muelekeo wa baba yake. Maamuzi ya Dominant na recessive ndo uhitimisha...

Tafiti zilizofanyika zimeonekana kuwa hizi DNA zikishanyonywa uhifadhiwa kwenye viungo mbalimbali vya mwili kama ubongo, ini nk...
 
Back
Top Bottom