Je, Mwanamke Hubeba DNA za Wanaume Wote Aliowahi Kulala Nao? Mtazamo wangu ni huu

Je, Mwanamke Hubeba DNA za Wanaume Wote Aliowahi Kulala Nao? Mtazamo wangu ni huu

Kuna mtu nilimsikia anasema, ukimwagia mwanamke sperm ni kama umeweka kumbukumbu mwilini mwake ni kwamba mwili wake utakukumbuka hata ikipita miaka kumi mkakutana ten bila kujuana. Mwili wake utakutambua pale tuu utakapolala nae tena, yaani akili na mwili wake utakuwa bado una memory ya mbegu zako hata wakipita wanaume 100.
 
Anabeba vinasaba vya mawazo, kuna alama inawekwa kichwani kwake ndo maana ni mara chache sana mwanamke atamuona mwanaume aliyewahi kushiriki naye tendo halafu asimtambue. Huwa wanakumbuka mpaka mikunjo waliyokunjwa siku husika.

NB: Wanawake wote huzaliwa na bikira. Kutoa bikira siyo mwisho wa matamanio yake, ni mwanzo. Hapo ndo tunasema GAME OON. Sasa hitimisha kuwa ukioa bikira umemaliza halafu likitokea la kutokea ushangazwe. Maadili ndo kila kitu, bila kujali hayo maadili kawa nayo kabla ya kutolewa bikira au baada.
Niliwahi kuambiwa na binti mmoja kuwa mumewe anamuamini sana kisa alimkuta bikra ila uhalisia ni kwamba anakitembeza sana
 
Kuna mtu nilimsikia anasema, ukimwagia mwanamke sperm ni kama umeweka kumbukumbu mwilini mwake ni kwamba mwili wake utakukumbuka hata ikipita miaka kumi mkakutana ten bila kujuana. Mwili wake utakutambua pale tuu utakapolala nae tena, yaani akili na mwili wake utakuwa bado una memory ya mbegu zako hata wakipita wanaume 100.
True kwa kuwa sperm zako sio kitu kipya mwilini mwake
 
Kuna kauli imekuwa ikisambaa sana mitandaoni siku hizi, kwamba mwanamke akishalala na mwanaume, hata kama hakupata mimba, basi hubaki na DNA yake mwilini. Wengine wanaenda mbali zaidi na kusema kuwa kama amekuwa na wanaume 5 au 10, basi anatembea na DNA zao wote, na huenda hata watoto atakaokuja kuzaa wakawa na tabia au muonekano unaofanana na wanaume hao wa zamani. Sasa swali la msingi linabakihii- ni kweli ya kisayansi au ni imani tu iliyojengeka?

Ukiangalia upande wa sayansi ya urithi, yaani Genetics, mtoto hupatikana pale ambapo yai la mwanamke linakutana na mbegu ya mwanaume mmoja tu. Hapo ndipo DNA za wazazi wawili zinachanganyika na kuunda mtoto. Hakuna mfumo unaoruhusu DNA ya mwanaume wa zamani kuja “kuingilia” mtoto wa mwanaume mwingine. Mfano rahisi ni huu: kama mwanamke alishawahi kuwa na mwanaume A miaka 3 iliyopita, halafu leo akapata mimba na mwanaume B, mtoto atakayezaliwa atachukua vinasaba kutoka kwa mama na mwanaume B pekeesio- A, wala C, wala mwingine yeyote aliyepita.

Chanzo cha mkanganyiko huu mara nyingi hutajwa kuwa ni kitu kinachoitwa Microchimerism. Hii ni hali ambapo seli chache sana za mtu mwingine zinaweza kubaki mwilini, mara nyingi kati ya mama na mtoto wakati wa ujauzito. Kwa mfano, mama anaweza kubaki na baadhi ya seli za mtoto wake kwa muda mrefu baada ya kujifungua. Lakini jambo la muhimu kuelewa hapa ni kwamba hali hii haimaanishi kubeba “DNA kamili” ya watu wengi kwa namna ya kuathiri watoto wa baadaye. Ni kiwango kidogo sana cha seli ambacho hakibadilishi urithi wa mtoto atakayezaliwa.

Ili kuweka wazi zaidi, fikiria mfano huu: kama kweli mwanamke angebeba DNA za wanaume wote aliowahi kulala nao, basi dunia ingekuwa na hali ya kushangaza sanamtoto- angeweza kuwa na mchanganyiko wa sura au tabia za watu ambao si wazazi wake kabisa. Lakini hali hii haionekani katika uhalisia wala haijaungwa mkono na tafiti za kisayansi. Watoto wanafanana na wazazi wao kwa sababu ya vinasaba wanavyorithi, si kwa sababu ya historia ya mahusiano ya mama.

Kwa hiyo hii dhana ya kwamba “uzae na mwanamke bikra ili kuepuka DNA za wanaume wengine” haina msingi wa kisayansi, bali inaegemea zaidi kwenye mitazamo ya kijamii na kitamaduni. Hii haimaanishi kwamba afya ya mahusiano haijalishikinachotakiwa- kupewa kipaumbele ni kujilinda dhidi ya magonjwa ya zinaa, kufanya vipimo, na kuwa na uaminifu katika mahusiano.

Mwisho wa siku, ni muhimu kutofautisha kati ya sayansi na imani. Sio kila kinachosambaa mtandaoni kina ukweli ndani yake. Elimu sahihi ndiyo inasaidia kufanya maamuzi sahihi.

Kwahiyo wanangu bikra sio kitu muhimu sana cha kufanya uogope kuanzisha familia na hawa second hand walio sokoni 😀😀😀
Kitanda hakizai haramu labda kama hakuna mfanano
 
Niliwahi kuambiwa na binti mmoja kuwa mumewe anamuamini sana kisa alimkuta bikra ila uhalisia ni kwamba anakitembeza sana
Hahaha, na wanawake wanajua saikolojia, wanaitumia kweli hizi tech. Ni kama ile ya kuambiwa unamridhisha kuliko mume wake.
 
Back
Top Bottom