Je, Mwanamke mvuta Bangi anafaa Kuolewa?

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Wakuu tujuzane kama mwanamke mvuta bangi anafaa kuoa. Tupo wanaume ambao baadhi yetu tumeshakutana na wanawake warembo lakini wanavuta bangi hali hiyo ikatusikitisha sana.

Je, mwanamke kama huyu ambaye ameshakuwa mtumiaji wa bangi anafaa kuoa? Je anaweza kuhudumia watoto wake kama wanawake wengine na kuishi kwenye familia kama mama wa nyumbani au ndo basi tena akishavuta bangi hafai kuoa mana ataleta usumbufu kwenye familia? Je wazazi, wifi na shemeji wakigundua kuwa mke ni mvuta bangi wanamchukuliaje mme wake?

Mana swali kubwa kwa sisi wanaume kama mke ni mvuta bangi mwanaume atakapofariki ghafla au kupatwa na tatizo upi usalama wa familia na mali zake kama anabaki huyu mwanamke mvuta bangi?
 
Kwann kwa mwanamke picha ya ajabu kwa mwanaume isiwe picha ya ajabu
Mwanaume anaweza kuwa nguzo tu ya familia hata kama anatumia bangi lakini hofu kwa mwanamke mla bangi anaweza kugawa chakula kirahisi kwa walaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…