Kuna watu mimi nawajua ni mwanaume na mwanamke walikuwa kwenye mahusiano, mwanamke alikuwa anafanya kazi na mwanaume hafanyi kazi yupo tu nyumbani kwa baba ake, mwanaume akaleta barua ya uchumba nyumbani akaandikiwa kiasi cha posa ..yule mwanaume alitolewa ile mahari na wazazi wake mana yeye hakuwa na kazi...alimuweka yule mdada miaka mitano nymbn baada ya kutoa mahari kwao, kiasi kwamba yule mdada akaamua kutegesha mimba ili aolewe, na kweli baada ya familia kugundua kuwa yule mdada ni mjamzito , itbd ndoa ifungwe haraka, si unajua tena ndoa za kanisani?, ndugu wakawa wamegharamikia everything kuanzia ghrm za kanisani mpk ukumbini na sherehe ilifana kweli mn ilikuwa ni ya gharama, mwanamke naye akaacha kazi kipindi anaolewa, mwanaume hakuwah hata siku moja kuishi nje ya nyumba yao, hajawah kujitegemea nje ya nyumba yao..kiasi kwamba kataftiwa chumba na vitu vya ndani na ndugu siku ya kwanza tu anafunga ndoa ndiyo wanaenda anza maisha na huyo mke wake, wameingia ndani ss mume hana kazi mke hana kazi, apo ndo patamu sasa...mume anambadilisha mke sehemu mbl mbl tu, mara kwa mjomba mara kwa shangaz mara kwa wakwe,..kiasi kwmba wapo pamoja lkn mwanamke ndiyo anapiga kazi na vibarua mbalimbali ili wale, na waishi na wtt lkn mwanaume akuuu mguu upo juu na sidhani kama anawaza wtt watakula nini na wataishi vipi, but mwanamke ndiyo anafight kwa hali na mali kuhakikisha life lina songa mbele, lkn tangu amuoe ata chupi yule mdada hajawah kununuliwa na yule mumewe...lkn mwanamke ndiyo amependa hasikii la muhazini wala la mshauri....NB wadada tusibebe mimba ili tupate nafasi ya kuolewa, na wala wakaka msikubali kutolewa mahari na wanawake zenu ata wazazi wako wasikutolee...jaribu mwnyw hiyo itakusaidia ktk maisha....hao ni marafki zang kabisa yamewatokea.