Je, mwanamke uko tayari kumpa pesa mchumba wako akakulipie mahari kwenu?

We shwaini nangoja ufike sour28 ili ukakalipie kanyo kiduku kako mahari kwa mkopo,,,maliza kucheka kwanza uje!😂😂😂😂😂 ila huwez amini ndiko tunakoelekea, maisha yatakuwa kama India...mke ndio anatoa mahari!
 
Hongera sana, ila kaa tuu ukijua binadamu tunatofautiana.
 
Wanaume mnatutakia Nini lakini
Tuwape Hadi hela ya mahari??
Najua kupenda,na huwa ninapenda Sana ila boss jaribu kutofautisha kupenda na uzwazwa
Hahah, anza assessment na Iyobo na Shishi kisha utakuja kuelewa what deep loving can do to a woman.
Kuna cousin wangu mmoja alifall kwa mtanga mmoja jamaa brazameni tu hana kitu kabisa, i think she lent the bride price to the guy maana yeye yupo vizuri kiuchumi...akaolewa fasta the clock was ticking.

Kwa maisha ya ndoa its almost cousin anafanya kila kitu maana jamaa ni chenga tu mission town maisha ya kushinda kijiweni na wana akila mrungi kila jioni.

Anawekewa mafuta ya gari, ada za watoto zinalipwa na hela za kuendesha maisha. Kama ana mchango ni mdogo sana maana cousin wangu hata akisafiri umeme ukaisha au kitu chochote ndani kikaisha ni mpaka ndugu apigiwe simu. But the guy is a father of 2 kids na kashatia mimba ingine ya 3!
 
Apo umenena kabisa mkuu...wadada wengi wanalazimisha waolewe na wenzi wao ilhali wanajua kabisa huyu mwenzangu hali yake ya kiuchumi kwa sasa haipo sawa na hii yote ni kutokana na ile kupata pressure kutoka kwa wenzie ambao wameshaolewa tyr ,naye ndipo anapoamua kujitolea mahari alowe faster faster...mi naamini hapa duniani hakuna mwanaume anayependa kutolewa mahari na mwanamke, wanaume wengi wakiona hali zao kiuchumi siyo nzuri huwa wanasema kabisa nivumilie mpk nipate pesa na nijipange vizuri ktk maisha...ukiona kuna mwanaume ambaye yeye anakubali kutolewa mahari basi ni kutoka kwa wale wa kisuli suli, wapo km vibenteni na mwsho wa siku wakiingia ktk ndoa lazima iyumbe sbb mwanaume amezoea kutolewa na sio mtafutaji...km mwanaume posa ndogo tu hata ya 30000 inakushnda kutoa ili yule mwanamke wako ajisikie furaha ,je ndani ya nyumba utaweza kweli kuhudumia?, na mwanamke akitake part as kichwa cha familia utaanza lalamika kuwa oh kwsbb ww ndy umejitolea mahari unaninyanyasa, usikute ata nyumba mnayokaa ni ya mwanamke apo ndiko hali inapozd kuwa tete ...mwanaume lazima aweke heshima kwa mwanamke wake.
 
Yani unanikosha nyoyo kwa unayoyaongea...ni ukweli mtupuuu...nina evidence kabisa ya icho kitu kutoka kwa mtu wangu wa karibu.
 
Akina dada mbona mmekua wakali hivyo kwenye huu uzi baada ya kusikia hela zenu zinazungumziwa hapa ?
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mwanaume kupewa mahari Ni umama..
Mwanaume wa hivi Mimi simtaki kwa kweli,,,apite tu pembeni,,yaani ameshindwa hata kuzibua vyoo au kuzungusha karanga??
Huu sio upendo,Ni ujinga
 
Binafsi sioni haja ya mzazi kutaka mahari ili binti yake aolewe. Kumbuka kijana huyo unayemkabidhi binti yako, anaenda kukusaidia majukumu yako kama mzazi katika kumlea. Yeye ndio atahakikisha mwanao anakula, analala, anavaa, anamtunza na vitu vingine. Hivyo kumtoza mahari ni kubariki mwanao akaishi maisha magumu kwani utakuwa umepunguza katika akiba yake ( hapa nazungumzia zile mahari za ndoa za kikristo).

Pili, unapofikia hatua ya binti yako kuolewa maana yake ni kwamba mzazi umri wako unakuwa umesogea. Hivyo uwezo wako wa kutafuta pia unakuwa umepungua. Huyo anayemuoa binti yako naye anageuka kuwa mwanao, ambaye atakuwa na jukumu la kukutunza pia. Kama kwenye mahari ulimpiga Milioni zake 7, kesho ukiumwa unadhani atakuwa na moyo wa kukusaidia kwa asilimia 100 ?

Mwanao anapokuja na kukwambia amepata mchumba anataka kumuoa, mzazi lako ni kujiridhisha kama huyo kijana anaweza mlea binti yako vile ambavyo wewe umekuwa ukimlea na kuwapa baraka tu wakaishi pamoja. Mahari zibaki fadhila anazotoa kijana kwenu wazazi.
 
Bora umsaidie mwanaume matumizi mengine yoyote pale anapokwama na Kuna ulazima wa kumsaidia,kuliko ujinga wa kumpa hela ya mahari.

Mahari inatakiwa asipewe hata na baba yake,maana anaoa yeye.
Kuna watu mimi nawajua ni mwanaume na mwanamke walikuwa kwenye mahusiano, mwanamke alikuwa anafanya kazi na mwanaume hafanyi kazi yupo tu nyumbani kwa baba ake, mwanaume akaleta barua ya uchumba nyumbani akaandikiwa kiasi cha posa ..yule mwanaume alitolewa ile mahari na wazazi wake mana yeye hakuwa na kazi...alimuweka yule mdada miaka mitano nymbn baada ya kutoa mahari kwao, kiasi kwamba yule mdada akaamua kutegesha mimba ili aolewe, na kweli baada ya familia kugundua kuwa yule mdada ni mjamzito , itbd ndoa ifungwe haraka, si unajua tena ndoa za kanisani?, ndugu wakawa wamegharamikia everything kuanzia ghrm za kanisani mpk ukumbini na sherehe ilifana kweli mn ilikuwa ni ya gharama, mwanamke naye akaacha kazi kipindi anaolewa, mwanaume hakuwah hata siku moja kuishi nje ya nyumba yao, hajawah kujitegemea nje ya nyumba yao..kiasi kwamba kataftiwa chumba na vitu vya ndani na ndugu siku ya kwanza tu anafunga ndoa ndiyo wanaenda anza maisha na huyo mke wake, wameingia ndani ss mume hana kazi mke hana kazi, apo ndo patamu sasa...mume anambadilisha mke sehemu mbl mbl tu, mara kwa mjomba mara kwa shangaz mara kwa wakwe,..kiasi kwmba wapo pamoja lkn mwanamke ndiyo anapiga kazi na vibarua mbalimbali ili wale, na waishi na wtt lkn mwanaume akuuu mguu upo juu na sidhani kama anawaza wtt watakula nini na wataishi vipi, but mwanamke ndiyo anafight kwa hali na mali kuhakikisha life lina songa mbele, lkn tangu amuoe ata chupi yule mdada hajawah kununuliwa na yule mumewe...lkn mwanamke ndiyo amependa hasikii la muhazini wala la mshauri....NB wadada tusibebe mimba ili tupate nafasi ya kuolewa, na wala wakaka msikubali kutolewa mahari na wanawake zenu ata wazazi wako wasikutolee...jaribu mwnyw hiyo itakusaidia ktk maisha....hao ni marafki zang kabisa yamewatokea.
 
We jaribu hata siku moja kuomba hela ya mwanamke ukanunue shati la sh 10000 uone moto utakao waka hapo. Ila wao ni sawa kukuomba 50,000 akanunue nguo ya kuvaa kwenye send off ya rafiki yake.
 
Kama mahari inamshindwa Mwanaume kuhudumia Familia ataweza kweli,mahali sio lazima iwe million mwanamke unaangalia uwezo wa mpenzi yaani hata kubeti ili apate mahali kutamshindwa😁😁😁😁
 
Dunia Ina mambo aisee [emoji134][emoji134].
Kwenda kuolewa na mtu anayekaa tu nyumbani Kama mgonjwa,analishwa na wazazi[emoji134][emoji134]!!
Yaani huyu dada nae akaenda kutegesha mimba hapo???
Wanaume kweli wajifunze kutafuta.
Kama mtu hawez tafuta hela ya mahari,, familia ataiwezea wapi kuitunza??
 
Kama mahali inamshindwa Mwanaume kuhudumia Familia ataweza kweli,mahali sio lazima iwe million mwanamke unaangalia uwezo wa mpenzi yaani hata kubeti ili apate mahali kutamshindwa😁😁😁😁
Kubet kungekuwa rahisi hivyo, unafikiri kuna mwanaume angekuwa analalamika ugumu wa maisha ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…