Je, mwanamke uko tayari kumpa pesa mchumba wako akakulipie mahari kwenu?

Je, mwanamke uko tayari kumpa pesa mchumba wako akakulipie mahari kwenu?

Mimi nazani mwanaume kama kweli anayonia na utayari wa kuoa hawezi kukosa kutafuta hela ya mahari kama amedhamiria.

Kwani ndoa si inaanza kwa mipangilio?

Tuseme inashindikana kutafuta vibarua hata vya dei worker January to December kupata hela ya kwenda kulipa mahari?

Ni kwamba ile willingness na utayari siyo wa kutosha kwa mwanaume!
 
Hivi mwanamke uliyejilipia mahari dhamiri yako inakushuhudia nini ndani yako?

Kama siyo kujidanganya wewe mwenyewe ni nini?

Sasa kama mwanaume kukulipia mahari kunamshinda Je kutunza familia?

Wanaume wengi wa hivyo huishia kuwa tegemezi kwa wake zao na ndugu zao,

Raha kuolewa utunzwe lakini tena inapikuwa kinyume chake tena eeeh?!

Kuna ndoa hadi wameachana mwanamke hajawahi furahia hela ya mwanaume wake!
 
Na vipi kwa sasa maisha yao yakoje? Hali ilishapendeza? Aman ndan ya ndoa yao ipo?
Mmhhh!! Hapana kwa kweli kujioa, nakumbuka shemeji angu alioa dada angu kwa 50000 kwa sababu hali yake kiuchumi haikua nzuri, hivyo dada aliwaeleza ukweli wazazi na wazazi wakapanga mahari kulingana na hali halisi ya muoaji
 
Kwa hiyo wanataka ROI wazee wetu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Acheni kuwaonea..mlitaka mtuoe bure!?
Haha! Wazee wako makini sana wanapofanya investments zao. Tena hapo ukute alishapiga hesabu zake za kujua PAY BACK PERIOD itadondoka ukiwa na umri gani, akapata ukiwa na miaka 25, sasa ukifika miaka 27 hujaolewa unageuka liability. Kila siku utaanza hojiwa kwa nini unashinda tu ndani na hauendi kusalimia marafiki zako. Mara kwa nini we marafiki zako ni wanawake wenzako tu wakati dunia ina watu wa jinsia mbili ( zinazokubalika duniani kote).
 
Ni utapeli kutoza mahari kubwa. After all siku hizi wanaofaidi ni wazazi na familia ya mwanamke. Utakuta ndugu wa mke wamejazana na wa mume wakija wanapigwa vita sana! Then Kwanini kutoa mahari kubwa?
Ile ni uthibitisho kwa jamii inayomzunguka kuwa binti yao kaolewa kwa heshima kama ilivyo kwa ndoa za kanisani unadhani haiwezekani mchungaji au padre akapita kila nyumba anafungisha ndoa ? na kwa nin sasa maandalizi ya miezi kadhaa yawepo? kila kitu ni sawa sema ni mahamuzi tuu.
 
Mahari ni ya anaeolewa wazazi hata haiwahusu katika uislam hata mwanamke akisema anataka elfu 10,000 ni sawa, ila kwasababu wazazi nao wanaingiza zao ambazo kisheria hazipo, hizo ndo zinakuwa nyingi mno mfano kuna ndugu alitaka kuoa mwanamke mahari yake alitaka laki 1 lakini wazazi wakaongeza zao laki 9 jumla 1M
Alete hata kuku ? Mahari unapanga wewe au wazazi ?
 
Mahari ni ya anaeolewa wazazi hata haiwahusu katika uislam hata mwanamke akisema anataka elfu 10,000 ni sawa, ila kwasababu wazazi nao wanaingiza zao ambazo kisheria hazipo, hizo ndo zinakuwa nyingi mno mfano kuna ndugu alitaka kuoa mwanamke mahari yake alitaka laki 1 lakini wazazi wakaongeza zao laki 9 jumla 1M
Heri yenu nyie ambao mwanamke anapanga yeye mahari ya kutolewa.
 
Achia mbali mwanamke kunipa Mahari nikamlipie kwao nimuoe. Mimi binafsi, swala la kulipa mahari linazidi kutokomea kichwani kwa spidi ya ajabu, nikimpata nitakwenda kwao nitajitambulisha nitawaeleza Adhma yangu kwao na kuwaomba Baraka zao waridhie swala langu sababu siendi kumnunua mtoto wao, nakwenda kuunganisha familia ya kwetu na ya kwao hiyvyo kuna mambo mengi nitahusika kwa hali na mali. Wakikataa wataifurahia shoo tu
 
Na vipi kwa sasa maisha yao yakoje? Hali ilishapendeza? Aman ndan ya ndoa yao ipo?
Aisee Mungu ni wa ajabu sana huwezi amini hali ya maisha yao ilibadilika shemeji alipata kazi nzuri, wamejenga, wana miradi na Mungu amewajaalia watoto 3, walau na usafiri wanao kwa kweli maisha yanaenda na wamekua muhimili kwa familia.
 
Ile ni uthibitisho kwa jamii inayomzunguka kuwa binti yao kaolewa kwa heshima kama ilivyo kwa ndoa za kanisani unadhani haiwezekani mchungaji au padre akapita kila nyumba anafungisha ndoa ? na kwa nin sasa maandalizi ya miezi kadhaa yawepo? kila kitu ni sawa sema ni mahamuzi tuu.
Pamoja na kuwa MAHAMUZI na wala si maamuzi, bado mahari kubwa ni utapeli wa kutupwa. Mtoze mwanaume kiasi ambacho hakitamuathiri kiuchumi. Na hicho kiasi, mwanamke angalau achangie hata ikiwa ni elfu moja, au potelea mbali miambili. Kwani hakuna kijana miaka 18 na zaidi atakosa 200.
 
Na vipi kwa sasa maisha yao yakoje? Hali ilishapendeza? Aman ndan ya ndoa yao ipo?
Na kilichosababisha wazazi kumhurumia shemeji kwanza alikua yatima, pili anajisomesha chuo na anauhitaji wa mwenza wakaona isiwe tabu dada alipoulizwa Je utakwenda na mtu huyu? Akajibu ndio wazazi wakabariki leo hii ndoa yao ina miaka 15
 
Haha! Wazee wako makini sana wanapofanya investments zao. Tena hapo ukute alishapiga hesabu zake za kujua PAY BACK PERIOD itadondoka ukiwa na umri gani, akapata ukiwa na miaka 25, sasa ukifika miaka 27 hujaolewa unageuka liability. Kila siku utaanza hojiwa kwa nini unashinda tu ndani na hauendi kusalimia marafiki zako. Mara kwa nini we marafiki zako ni wanawake wenzako tu wakati dunia ina watu wa jinsia mbili ( zinazokubalika duniani kote).
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]..
Lazima upigiwe hesabu nzito..chuo+a level+olevel[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119].
Ila kiuhalisia ile hela ya mahari hutolewa tu Kama 'asante" Maana huwezi lipa kila kitu alichonihudumia mzazi(kuna muda mzazi Anakupa SI tu msaada wa kipesa)

Sasa Hadi nimefika huu umri wa utu uzima,unakuja kunichukua kwetu,nakuja kwenu,,,nahama ukoo,nakuzalia watoto wanaitwa kwa jina lakoo..hizo fadhila zote hakuna gharama inayoweza kuzilipa
Ndiyo Maana huku kwetu mahari hailipwi hela pekee...hela inakuwepo lakini materials things nahisi inazidi pesa Kama jembe,kitenge Cha mama ,shati la baba nk nk

Eti PBP hahaha mtawasingizia na ROI Sasa,Maana mnawaona wazee wetu kama wahasibu siku hizi (joking)[emoji1787]
 
Ndio ila bado mambo magumu mana wazee wanaweka mambo ya mila hivyo hata mwanamke akisema anataka elf 10, wazee wataweka mzigo wao wa haja
Heri yenu nyie ambao mwanamke anapanga yeye mahari ya kutolewa.
 
Saint anne,
Unajua katika malezi yako mme wako atakuwa na nafasi kubwa sana. Ukiwa kwa wazazi jukumu la kukulea kinakuwa la wazazi wako wote wawili, piga hesabu hapo utakuta umesoma viboarding huko, muda huo wazazi hawakuwa na wewe, ila huyo jamaa akishakuoa tu he has to be there for you all the time tena alone. Utaumwa, utahuzunika, utalia, utafurahi, utaumizwa, utasikitika pamoja n mengine yote yatakayokukuta katika maisha yeye pia itabidi ayapitie hayo, japo kwa wazazi inaweza isiwe hivyo.

Mmeo atakuwa na wewe kila siku mpaka kifo. Kwa hesabu za haraka hapo utaona yeye ndo ataishi na wewe duniani siku nyingi kuliko hata ambazo umeishi ukiwa chini ya himaya ya wazazi wako. Bado tunatozwa mahari kweli ?

Jinsi gani wanaume tulivyo na roho nzuri, eti nakutoa kwenu nakuleta kwangu nakupa jina langu, yet kwangu kunakuwa kwetu.

Huko kutomaliza mahari ndo kunatufanyaga tuone ukweni kuchungu na hata sometimes kuwaogopa baba wakwe, unahisi ukionana nae tu atakumbushia deni lake 😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Emery Paper,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Unadhani kwetu tulikuwa hatuumwi[emoji1787][emoji1787]
Maisha niliyopitia Mimi..misukosuko niliyopitia yaani wazazi wangu wamehustle Sana.
Unataka unichukue bure Bila mahari kisa tu utanihudumia?
Kuhudumia Ni jukumu lako kwa mujibu wa maandiko matakatifu,,ndiyo Maana tuko tofauti Kati ya mwanamke na mwanamke...bila hivyo Basi wote tungekuwa wanawake[emoji2].

Mahari Ni shukrani na Asante tu,kitendo Cha mzazi kukupa mtoto umuhamishie ukoo wako yaani hakilipiki.
 
Back
Top Bottom