Je, mwanamke uko tayari kumpa pesa mchumba wako akakulipie mahari kwenu?

Je, mwanamke uko tayari kumpa pesa mchumba wako akakulipie mahari kwenu?

Pamoja na kuwa MAHAMUZI na wala si maamuzi, bado mahari kubwa ni utapeli wa kutupwa. Mtoze mwanaume kiasi ambacho hakitamuathiri kiuchumi. Na hicho kiasi, mwanamke angalau achangie hata ikiwa ni elfu moja, au potelea mbali miambili. Kwani hakuna kijana miaka 18 na zaidi atakosa 200.
Haiwezekani kutoa kidogo kwani ni suala la kijamii zaidi wala sio la baba na mama mzazi, mfano kuna mbuzi ya shangazi au mjomba, bibi, babu, branketi na shuka la bibi au babu vyote hivo ni hela, hataivo hao wote walikuwa walezi wa huyo binti unayempenda ndio maana wanataka wafanye sherehe ya kujipongeza kwa kumtunza vizuri hadi wewe ukampenda binti yao,Na kama una watoto wa kike utaona ni sahihi, watoto wa kike wanachangamoto kubwa mpaka kumfikisha hapo.
 
sengobad,
Changamoto ipo kwa mtoto wa kiume akiwa Shoga ni kama kifo cha ukoo. Bado huna hoja za kuutukuza utapeli huo. Mtoto ni mtoto awe wa Kike au kiume ni sawa
 
Mimi namshukuru mke wangu alinichangia 200000 nami nikatoa 200000 kukamilisha mahari,hicho ni kipimo tosha cha upendo wake kwangu.Maneno yake nayakumbuka mpaka leo "hata kama hauna mahari kwa sasa twende tu nyumbani wakuone suala la mahari nitajua mimi nitaongea nao vipi" Mpaka sasa ni mama wa watoto wangu wawili.SHE IS A WIFE MATERIAL.
 
Changamoto ipo kwa mtoto wa kiume akiwa Shoga ni kama kifo cha ukoo. Bado huna hoja za kuutukuza utapeli huo. Mtoto ni mtoto awe wa Kike au kiume ni sawa
Unaleta mada nyingine kabsa hakuna aliyesema wa kiume sio mtoto, wote ni watoto na wanapendwa, kwa kifupi ni hivi ukipenda kitu lazima ukigharamikie kwann iwe nongwa kwa huyu binti? tafakari kwa kina. Wanyama/ ndege wanatoa mahari itakuwa binadamu anayejua mema na mabaya.
 
Unaleta mada nyingine kabsa hakuna aliyesema wa kiume sio mtoto, wote ni watoto na wanapendwa, kwa kifupi ni hivi ukipenda kitu lazima ukigharamikie kwann iwe nongwa kwa huyu binti? tafakari kwa kina. Wanyama/ ndege wanatoa mahari itakuwa binadamu anayejua mema na mabaya.
Wewe ni Me au Ke?
 
Mahari ni malipo au zawadi?
Kwa misingi ya uwepo wake, mahari haitakiwi kulipwa yote, kwa kuwa siyo bei ya bidhaa imewekwa kama alama tu ya kuonyesha shukurani kwa familia ya binti kumkuza. Ndiyo maana katika hiyo mahari kuna mlolongo wa kina bibi, babu, wajomba, shangazi na wote waliofanya ulezi kwa namna moja ama nyingine.
 
Kabila nitokalo huwa kama pesa ilitkiwa kuwa kidogo sana kwa ajili ya wazazi kununulia vitu fulani ambavyo utaandikiwa kwenye barua. Vingine ilitakiwa viletwe vitu mfano mikeka kwa shangazi, kikoi cha babu, khanga ya yule n.k. ila watu kwa uvivu huamua kuweka bei ya vile vilivyoandikwa hapo ndipo hufanya mahari ionekane ghali. Na kwa mantiki hiyo bei huwa haipungui kwa kuwa vitu hununuliwa kweli.
 
Mmmh inabidi siku moja ukutane na mke wangu ujifunze jambo ni mzungu wa S.A, mwaka 2007-2012 tulikuwa na mobile relationship tu nikimpiga danadana za hapa na pale hela nilikuwa sina.

Early 2013 alinifata Tanzania na kunitaka nikatoe mahali kwao mwanaume sina hata mia binti bila khiyana akanipa rand 35000 na nilimrejeshea pesa yake mwaka 2017.


Samahani sana mkuu...hana kaka au wajomba huyo wifi?
 
Nature inakataza huo upumbavu...... Vitabu vya dini havijaandika huo upuuzi siwezi kufanya kamweeeeeeeeee....
 
Huu mjadala ni mzito ila naona watu wanaujadili kiwepesi wepesi kwakuwa sehemu yao wanaujadili kwa kuegemea hisia za kingono na sio kindoa. Wakuu maisha ya ndoa ni mwanzo wa maisha ya wahusika sehemu ya pili ambayo inachangamoto nyingi, changamoto zinazotokana na kujuana tabia halisi baada ya kufichana kwa muda wote mrefu wa uchumba.
Mwanaume ukiona mshichana anataka kukulipia mahari yani kutimiza majukumu muhimu yanayokustahili ili yakuguse basi jiulize maswali yasipungue 3, kwanini anajirahisisha? Tutaweza kuishi salama kwa mkike kujilipia mahari? Hivi nimeoa au nimeolewa?
Dada jiulize unamlipia mahari je ataweza kulea familia ikiwa mahari tu kashindwa? Nini kimekusukuma kumlipia mahari? Je kitakuwepo siku zote.
Kwetu mahari ni sehemu ya heshima/utambulisho/alama au ishara kuwa binti ameolewa nyumba fulani ila mahari sio biashara wala thamani ya kumlipa mzazi kwa bint yake.
Wengine tuna watoto watatu na hatujalipa mahari ila tulichosaidia ktk familia ya ukweni ni zaidi ya mara mia moja ya mahari.
 
kwanza mwanamke unaanzaje kumpa mwanaume MAHARI akakulipie..ni sawa na kujiposa mwenyewe...na mwanaume kabisa unapokea na kwenda kutoa...haki unapaswa ufilwe kwanza ndo upewe uende.ijulikane na wewe punga....aibu.....mwanaume kutoa MAHARI (IN YOUR POCKET) ni jambo la ufahari na HESHIMA, hata malaika wanapiga makofi hakika... huna unao wa nini....piga punyeto mpaka mikono upate ujauzito.....
 
Back
Top Bottom