Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Allah akulipe kheri ndugu yangu.

Namshukuru Allah kwa neema ya Uislam.
 
Kwaiyo unashauri kwa mtu asiyetaka kuoa msikitini ama kanisani avute tu mke na kuishi naye na wajichukulie kuwa wameoana?
 
Kwaiyo unashauri kwa mtu asiyetaka kuoa msikitini ama kanisani avute tu mke na kuishi naye na wajichukulie kuwa wameoana?
Sidhani kama utakuwa umeelewa nilichomaanisha.

1. Kufunga ndoa msikitini au kanisani hakuhusiani kabisa na mahari. Unaweza kufunga ndoa bila kutoa mahari kama pande zote mbili mmekubaliana kutofata utaratibu huo uliopitwa na wakati.

2. Simaanishi kutowashirikisha familia au taratibu za kidini namaanisha kutotoa mahari.

3. Ndoa ni jambo la utayari, kama wawili wako tayari kuanzisha familia hilo linatosha kabisa, hizo nyingine ni mbwembwe tu
 
Kama baba mzazi hayupo lazima upande wa baba awape mtu yaan shangazi au baba mdogo na mkubwa. Haiwezekani ukoo mzima wa baba hakuna mtu wa kuwakilisha.
Sijui wewe ni dini gani ama kabila gani, kwa uislam, Mtoto wa nje ya Ndoa ni wa Mama kwa maana hiyo Mahari itatolewa na kupokelewa na ndugu wa upande wa Mama kwa maana ya Mjomba, lakini kubwa unalopaswa kujua ni Mahari ni ya Binti, yeye ndie atasema anachokitaka kama mahari yake na yeye ndie atakayekabidhiwa mahari yake kama akiigawa itakua kwa mapenzi yake,

Lakini kama wewe ni Muoaji hayo wewe sidhani kama yanakuhusu, hiyo ni mipango ya familia wewe utaambiwa siku ya kupeleka mahari na utaipeleka, imepokelewa na nani sio hoja kwako.
 
Hata wajomba nao niwazazi wanaweza kumuozesha mtt wadadao na kupokea mahari bili shida yeyote
 
Peleka mahali, hayo mengine waachie wenyewe, HAYAKUHUSU
 
Mahari za hivyo wanapokea wajomba nimeshawahi kuona my friend hakulelewa na baba kabisa wajomba zake ndo walipokea mahari
 
Kama baba mzazi hayupo lazima upande wa baba awape mtu yaan shangazi au baba mdogo na mkubwa. Haiwezekani ukoo mzima wa baba hakuna mtu wa kuwakilisha.
Utajikuta unamuoa ndugu yako ambae baba yako alipiga akapita hivi wewe kwenye kusorola umempenda kumbe ni dada yako mama mwingine baba mmoja...
 

Kwanza mahali ni haki ya muolewaji yeye mwenyewe

cha pili mahali inapokelewa na baba au ndugu wa babu yani kiumeni wa binti.

lakini swali linaweza kuja kama huyu bint sio mtoto wa ndani ya ndoa nani atapokea mahari.

jibu mahari atapokea mtu yoyote yule wa karibu au wenye una saba na binti.

lakini swala la kumuozesha/ kutoa idhini ya binti kuolewa lipo chini ya baba mzazi / walihi wake ( yani baba mkubwa/ baba mdogo / kaka) kama ni mtoto wa ndani ya ndoa.

ila kama ni wa nie ya ndoa jukumu hilo analo "Kahazi"
 
Kama hajui ndugu zake upande wa baba je anafaa nimtolee mahari? Wewe uoni kama kuna ulazima wa kuwajua ndugu zake upande wa baba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…