Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 1,628
- 2,720
Allah akulipe kheri ndugu yangu.Kwa waislamu (tukiacha posa maana sina ujuzi nayo) mahari anapewa muolewaji. Mahari ni zawadi ya bwana kumpa bibi na wala si thamani ya binti kwamba ananunuliwa kwayo!
Utofauti wa zawadi hii na zawadi nyingine ni kuwa muoaji haamui tu yeye mwenyewe bali lazima amuulize huyo mwanamke anayetaka kumuoa kwamba angependa zawadi gani.
Kwahiyo mahari atakayotaja bibi basi bwana ataileta na itapokelewa na walii wa muolewaji (walii ni baba wa muolewaji au mwanaume yeyote wa upande wa baba wa muolewaji aliyepewa jukumu la kumuozesha binti)
Akishapokea huyo walii atampa binti mahari yake yote iliyotolewa kisha ndoa inafungwa. Maamuzi ya mahari achukue au awaachie wazazi au atumieje yanabaki kwa binti mwenyewe.
Watu sasa (hasa watu wa mila za Kitanzania) kwa kuona sheria hiyo wakaingiza mambo kibao hapo ili wapate ulaji kupitia ndoa. Mara mkaja, mara blanketi, mara makosa, mara... Yaani unakuta unataka kuoa lakini unawalipa hela wana ukoo wote wa binti! Matokeo yake kukitokea jambo kidogo mtu anakimbilia kwenye mahari anaanza kuwianisha thamani ya ndoa au mtu na mahari.
Namshukuru Allah kwa neema ya Uislam.