Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Kwa waislamu (tukiacha posa maana sina ujuzi nayo) mahari anapewa muolewaji. Mahari ni zawadi ya bwana kumpa bibi na wala si thamani ya binti kwamba ananunuliwa kwayo!

Utofauti wa zawadi hii na zawadi nyingine ni kuwa muoaji haamui tu yeye mwenyewe bali lazima amuulize huyo mwanamke anayetaka kumuoa kwamba angependa zawadi gani.

Kwahiyo mahari atakayotaja bibi basi bwana ataileta na itapokelewa na walii wa muolewaji (walii ni baba wa muolewaji au mwanaume yeyote wa upande wa baba wa muolewaji aliyepewa jukumu la kumuozesha binti)

Akishapokea huyo walii atampa binti mahari yake yote iliyotolewa kisha ndoa inafungwa. Maamuzi ya mahari achukue au awaachie wazazi au atumieje yanabaki kwa binti mwenyewe.

Watu sasa (hasa watu wa mila za Kitanzania) kwa kuona sheria hiyo wakaingiza mambo kibao hapo ili wapate ulaji kupitia ndoa. Mara mkaja, mara blanketi, mara makosa, mara... Yaani unakuta unataka kuoa lakini unawalipa hela wana ukoo wote wa binti! Matokeo yake kukitokea jambo kidogo mtu anakimbilia kwenye mahari anaanza kuwianisha thamani ya ndoa au mtu na mahari.
Allah akulipe kheri ndugu yangu.

Namshukuru Allah kwa neema ya Uislam.
 
Hizo mila za kununua watu zimepitwa na wakati, wala hampaswi kujificha kwenye mila kiujumla swala mahari halina faida yoyote kwa sasa.

Na siku zote watetea mahari wamejificha kwenye mila ila hawana sababu za msingi mahari inawasaidia nini wanandoa.

Labda namimi nikupe elimu kidogo,
Mahari ilitolewa hapo zamani kwa sababu mwanamke alichukuliwa kama kijakazi anayetoka familia yake kwenda familia nyingine kwajili ya kuzaa watoto na kuzalisha mali. (Ufugaji na kilimo)

Ilionekana ni hasara kumuoa mwanamke kwa mahari Alafu hasizae watoto wengi au kushindwa kuzalisha mali (kilimo) na huyu mwanamke alikuwa kama mtumwa.

Sasa watu kama wewe mnataka tuendeleze utaratibu kama huu kwa kichaka cha mila.

Kama mila haina faida kwa mazingira ya sasa hatunabudi kuachana nayo.
Kwaiyo unashauri kwa mtu asiyetaka kuoa msikitini ama kanisani avute tu mke na kuishi naye na wajichukulie kuwa wameoana?
 
Kwaiyo unashauri kwa mtu asiyetaka kuoa msikitini ama kanisani avute tu mke na kuishi naye na wajichukulie kuwa wameoana?
Sidhani kama utakuwa umeelewa nilichomaanisha.

1. Kufunga ndoa msikitini au kanisani hakuhusiani kabisa na mahari. Unaweza kufunga ndoa bila kutoa mahari kama pande zote mbili mmekubaliana kutofata utaratibu huo uliopitwa na wakati.

2. Simaanishi kutowashirikisha familia au taratibu za kidini namaanisha kutotoa mahari.

3. Ndoa ni jambo la utayari, kama wawili wako tayari kuanzisha familia hilo linatosha kabisa, hizo nyingine ni mbwembwe tu
 
Kama baba mzazi hayupo lazima upande wa baba awape mtu yaan shangazi au baba mdogo na mkubwa. Haiwezekani ukoo mzima wa baba hakuna mtu wa kuwakilisha.
Sijui wewe ni dini gani ama kabila gani, kwa uislam, Mtoto wa nje ya Ndoa ni wa Mama kwa maana hiyo Mahari itatolewa na kupokelewa na ndugu wa upande wa Mama kwa maana ya Mjomba, lakini kubwa unalopaswa kujua ni Mahari ni ya Binti, yeye ndie atasema anachokitaka kama mahari yake na yeye ndie atakayekabidhiwa mahari yake kama akiigawa itakua kwa mapenzi yake,

Lakini kama wewe ni Muoaji hayo wewe sidhani kama yanakuhusu, hiyo ni mipango ya familia wewe utaambiwa siku ya kupeleka mahari na utaipeleka, imepokelewa na nani sio hoja kwako.
 
Hata wajomba nao niwazazi wanaweza kumuozesha mtt wadadao na kupokea mahari bili shida yeyote
 
Peleka mahali, hayo mengine waachie wenyewe, HAYAKUHUSU
 
Mahari za hivyo wanapokea wajomba nimeshawahi kuona my friend hakulelewa na baba kabisa wajomba zake ndo walipokea mahari
 
Kama baba mzazi hayupo lazima upande wa baba awape mtu yaan shangazi au baba mdogo na mkubwa. Haiwezekani ukoo mzima wa baba hakuna mtu wa kuwakilisha.
Utajikuta unamuoa ndugu yako ambae baba yako alipiga akapita hivi wewe kwenye kusorola umempenda kumbe ni dada yako mama mwingine baba mmoja...
 
Huyu binti kalelewa na mama yake pekee yake. Baba yake yupo hajafa ila binti hajawahi kukutana ana kwa ana na baba yake wala katika upande wa baba yake hamjui ndugu yeyote.

Je, kwa scenario kama hiyo binti anafaa kutolewa mahari na kuolewa?

Na taratibu za mahari zipoje? Kwani navyojua mahari ni ya baba na kama baba hayupo mahari ipokelewe na yeyote upande wa baba yaani shangazi au baba mdogo au mkubwa.

Kwanza mahali ni haki ya muolewaji yeye mwenyewe

cha pili mahali inapokelewa na baba au ndugu wa babu yani kiumeni wa binti.

lakini swali linaweza kuja kama huyu bint sio mtoto wa ndani ya ndoa nani atapokea mahari.

jibu mahari atapokea mtu yoyote yule wa karibu au wenye una saba na binti.

lakini swala la kumuozesha/ kutoa idhini ya binti kuolewa lipo chini ya baba mzazi / walihi wake ( yani baba mkubwa/ baba mdogo / kaka) kama ni mtoto wa ndani ya ndoa.

ila kama ni wa nie ya ndoa jukumu hilo analo "Kahazi"
 
Mkuu, unaenda mbele halafu unarudi nyuma.. mwanzoni umesema kuwa kwa upanda wa Baba yake hakuna anayemfaham hata mmoja, halafu hapa unasema lazima wawepo, watakuwepoje wakati hawafahamiani!?? Au unataka sisi tukakusaidie kuwatafuta ndugu zake!??
Maana majibu tayari unayo.

Kama kuna uwezekano wa kuwatafuta hao ndugu zake, basi watafutwe, kama hakuna uwezekano basi mama yake na wajomba wapokee mahari
Kama hajui ndugu zake upande wa baba je anafaa nimtolee mahari? Wewe uoni kama kuna ulazima wa kuwajua ndugu zake upande wa baba?
 
Back
Top Bottom