Mimi na wewe nani anapotosha?
unajua hata mwongozo wa fungu unalosema?
Kati yako na Mimi nani ana akili ya Mgando...?
Kwa faida ya wengine nitasema maana ya hilo fungu...Na hilo halihusiani na zaka bali linahusiana na ulipaji wa kodi...
Mafarisayo hali wakijua kuhusu sheria za kidini wakati huo Hazikuruhusu kupeleka pesa kwa watu wasio wa kidini (kulipa kodi) wakamfata yesu wakijua kwamba majibu yake yangemchonganisha na serikali..lakini alikuwa ameshawajua...
na Kiufupi halihusiani na ZAKA HATA NUKTA..
Rudia kulisoma...
Marko 12:13-17
[13]Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno.
[14]Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?
[15]Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.
[16]Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari.
[17]Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.