Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Si msikitini wala kanisani,
Japo nimemueleza fungu la kumi linapaswa kupelekwa wapi.

Bora apeleke pesa kwa wenye uhitaji, personal ni bora apeleke kwa wenye uhitaji kuliko kupeleka pesa kwa kitu kinachodai ni muweza wa yote halafu ananiomba pesa yangu.
Kama atashindwa kufanya hivyo nimempa ushauri ale mbuzi choma au kitimoto mpaka pesa iishe.

Fungu la kumi ni madhabahuni sio mbadala,sadaka ndio unaweza wapa wahitaji kwa kadri uwezavyo.
 
Kazi ilofanywa nao ndio inayofanywa sasa na tasisi za kidini hasa makanisa.
Bado ujajibu swali.
Umesema walawi walikuwa hawana ardhi na lilikuwa kabila la makuhani kama nitakua nakosea nirekebishe,hivyo wanakula madhabauni.

Kwanini uchukue mila na tamaduni za kwao uje kupachika kwangu mimi msandawe? Huoni kama unajaribu kuzi standardize hizo sheria kwenye universal level wakati zilikuwa zinahusu jamii fulani?

kwanini asipeleke pesa kwenye kituo cha watoto yatima zikaenda kuwasomesha tupunguze ujinga? Kwanini nikampe mtu ambaye ajakatazwa kuwa na ardhi ana nguvu zake kwa kisingizio cha walawi waliambiwa hivyo? Hao wachungaji hawana ardhi?

Ifike mahala tuache kutetea hivi vitu tusilazimishe kwamba lazima nitoe fungu la kumi.
 
Utii ni bora kuliko dhabihu,wewe kama mkristo sheria inataka utoe fungu la 10 madhabahuni hili halina mjadala,hutaki acha hujalazimishwa,sadaka unaweza wapa wa hitaji kadri uwezavyo.

Pia tambua kwa sasa maisha yamebadilika sana hao wachungaji na maaskofu inabidi wajiongeze ili waweze kuishi mana hata sadaka na matoleo mnatoa kidogo na kwa manunguniko,ili hal mahitaji ya kanisa ni makubwa kuliko makusanyo.
 
Kazi zao ni sawa na zile za walawi hakuna tofauti.
Mbona hujibu maswali?
Embu fata mtiririko sahihi
“Kazi zao ni sawa na zile za walawi” walawi hawakuruhusiwa kuwa na ardhi? Kama ndio je hawa wanyakyusa na wao hawajaruhusiwa kuwa na ardhi?

Mbona maswali mepesi utaki kujibu?
Nimekuambia kwanini unachukua tamaduni za jamii fulani kuziweka kwenye level za universal huoni kama unajaribu kulazimisha vitu?
 
Utii ni bora kuliko dhabihu,wewe kama mkristo sheria inataka utoe fungu la 10 madhabahuni hili halina mjadala,hutaki acha hujalazimishwa,sadaka unaweza wapa wa hitaji kadri uwezavyo.

Pia tambua kwa sasa maisha yamebadilika sana hao wachungaji na maaskofu inabidi wajiongeze ili waweze kuishi mana hata sadaka na matoleo mnatoa kidogo na kwa manunguniko,ili hal mahitaji ya kanisa ni makubwa kuliko makusanyo.
Nimekubali kushindwa kwako.
Siku njema🤝
 
Mbona hujibu maswali?
Embu fata mtiririko sahihi
“Kazi zao ni sawa na zile za walawi” walawi hawakuruhusiwa kuwa na ardhi? Kama ndio je hawa wanyakyusa na wao hawajaruhusiwa kuwa na ardhi?

Mbona maswali mepesi utaki kujibu?
Nimekuambia kwanini unachukua tamaduni za jamii fulani kuziweka kwenye level za universal huoni kama unajaribu kulazimisha vitu?

Je unamini kwa sasa sisi tu waridhi wa ufalme si kwa kabisa ama rangi bali kwa utii na imani katika Yesu kristo?

Sasa kipi kinakupa shida kuamini kazi za walawi wa sasa ambao ni wachungaji na maaskofu?

Pia kristo alisema mmpe Mungu vilivyo vyake we unadhani alikua anasisitiza kitu gani?
 
fransisi ni shoga mkuu.pole najua imekuuma

Yeyote aletaye hoja za ushoga mahali pasipo stahili jua ni shoga na mawazo yake yamejaa ushoga.

Mkuu kama huna mchango katika huu uzi kuhusiana na zaka ni vyema ukapita kimya kimya
 
Je, fungu la kumi linaweza tolewa kwa wajane, yatima na wenye shida au ni lazima nikatoe kanisani?

Naomba hekima zenu juu ya hili.
Unapotoa Msaada lazima uhakikishe WATU wanafahamu na saa nyingine utalenga upate sifa hii huwa ina haribu sadaka maana inakuwa NI Msaada biblia inatuambia hupati kitu ,lakin kama sadaka unataka Unatakiwa utoe kimya kimya na hata mtu akikushukuru mwambie mshukuru mungu maana ndo kakupa ,kingine unapotoa sasa sadaka sikiliza moyo wako usiangalishida za mtu angalia moyo wako unakutuma WAPI,ndo maana yesu alisema nipe Mimi Kwanza maskini hawataisha duniani mpaka dunia inaisha,
 
Tunaye Yesu kuhani mkuu kwa sasa, walawi walishinda hekaluni kwaajiri ya kuchinja sadaka za kuteketezwa kwa ondoleo la dhambi zao, hivi leo mwanakondoo ameshabeba dhambi ya ulimwengu mzima, kwasbbu hiyo walawi hawana kazi Tena, mwanaume kamaliza kila kitu, hivyo katika agano jipya hakuna fungu la kumi ila unatoa ulichonacho unachowiwa kutoa. Ndugu yangu hiyo Hela ni vema wasaidie wahitaji au kula na familia yako roho zenu zifurahi.
 
Peleka kwa wenye uhitaji hakuna Sehemu kwenye biblia inasema upeleke kanisani..
Ila imesisitixa ni kwa ajili ya Wasiojiweza
Hii ilikuwa specific kwa walawi ksb kazi waliyopewa haikuwezesha wao kufanya kazi nyingine, hakuna maagizo kama hayo kwenye agano jipya.ila wachungaji wametumia fursa hiyo kulimbikiza mali. Agano jipya: hakuna sadaka za kuteketezwa, watu waliompokea kristo ni makuhani na Yesu ndiye kuhani mkuu, wachungaji wa sasa ni waajiriwa, wafanyabiashara, wanamiliki mali ikiwemo aridhi, hivyo ni Dhabi kubwa kumpelekea mchungaji mwenye fursa hizo zote ukaacha kuwapa yatima na wenye shida.
 
Utii ni bora kuliko dhabihu,wewe kama mkristo sheria inataka utoe fungu la 10 madhabahuni hili halina mjadala,hutaki acha hujalazimishwa,sadaka unaweza wapa wa hitaji kadri uwezavyo.

Pia tambua kwa sasa maisha yamebadilika sana hao wachungaji na maaskofu inabidi wajiongeze ili waweze kuishi mana hata sadaka na matoleo mnatoa kidogo na kwa manunguniko,ili hal mahitaji ya kanisa ni makubwa kuliko makusanyo.
Jamani msidanganye watu, hakuna Sheria ya fungua la kumi katika agano jipya,ila ni vema kutoa unachowiwa Ili huduma za kiroho ziendelee.
 
Fungu la Mungu au fungu la mchungaji? Hawa hawa manabii wetu wa siku hizi uwapelekee fedha halafu useme umepeleka kwa Mungu? Hawa hawa kina Gwajima na Mzee wa Upako au kina Mwamposa? Kina 'nabii'' Malisa?
Acha wivu wewe.
Unazungumzia "hawa manabii wetu"
Mbona hupingi Padri wa katoliki na mchungaji wa Lutheran kupokea fungu la kumi?

Umeshawahi kupanda daladala ukadaiwa RAMBIRAMBI?
au ukakata tiketi ya ndege ukaambiwa ulipe Mahari?
Ushawahi kwenda kuchumbia ukaambiwa ulipe NAULI?

Hivyo basi , ZAKA/FUNGU LA KUMI linatolewa kwenye kanisa unalosali tu na ukienda kutoa kwa ombaomba wale barabarani hilo sio fungu la kumi huo ni msaada kama wa wazungu wanaotusaidia .
 
Je unamini kwa sasa sisi tu waridhi wa ufalme si kwa kabisa ama rangi bali kwa utii na imani katika Yesu kristo?

Sasa kipi kinakupa shida kuamini kazi za walawi wa sasa ambao ni wachungaji na maaskofu?

Pia kristo alisema mmpe Mungu vilivyo vyake we unadhani alikua anasisitiza kitu gani?
Wewe hatuwezi kuendelea kujenga hoja yesu kristo amefata nini katika walawi wasioruhusiwa kuwa na ardhi na ni kabila la makuhani?

Kama huwezi kujibu maswali yangu mepesi kwanini wasandawe unawafananisha na walawi basi, hujajibu swali lolote nililouliza zaidi ya kuruka ruka.

Asubuhi njema.
 
Jamani msidanganye watu, hakuna Sheria ya fungua la kumi katika agano jipya,ila ni vema kutoa unachowiwa Ili huduma za kiroho ziendelee.
Mkuu,
Binafsi huwa nafurahishwa na watu kama wewe, kusema ukweli kama huu unahitaji boldness(ujasiri) mkubwa sana.

Mimi nimemuuliza kwanini unawafananisha walawi na wasandawe au wanyakyusa kwa mantiki ya wote wanafanya kazi za kilawi.

Kwa madai yake walawi hawakuruhiswa kuwa na ardhi hivyo walikula madhabahuni na ni kabila la kikuhani, nikamuuliza je wachungaji wa kitanzania wapo ambao hawaruhusiwi kuwa na ardhi?

Kwa akili ya kawaida tu huoni mtu huyu anajaribu kupachika mila na desturi za kabila fulani kuziweka ziwe applicable kwenye ulimwengu mzima?
 
Back
Top Bottom