Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Maandiko yanasema hivyo nakubali. Swali: wana wa walawi wa sasa ni sawa na wale wa zamani? Makuhani wa sasa ni sawa na wale wa zamani? Waangalizi wa hekalu wa sasa ni sawa na wale wa zamani? Hawa wa sasa mbona wanapewa urithi wa ardhi na ''wanatafuna'' kondoo huku wakijirekodi na simu?
Walawi gani wafanyabiashara wanamiliki Hotel na wengine wanasiasa wabunge.
 
Kuliko kupeleka kwenge dhehebu bora kwa yatima
Maana halitamfikia Mungu ila litaingia kwenye miradi, na mifuko ya watu.
Alioaswa achukue mchungaji.
 
Fungu la kumi sio sadaka ya agano jipya ni torati ile sasa kama unafuata torati ni wewe lakini nakuambia hakuna awezaye kuifuata torati kwa 100% umewahi kusoma kumb 14:22 mpaka inapoishia hiyo sura ndo utaelewa kuwa mnapigwa

Katika torati wewe unachukua kipi na unaacha kipi,?kuhusu matoleo Kristo alishasema mpe Mungu vilivyovyake na mpe Kaisar vilivyovyake.
 
Wasichojua watu ni kuwa walawi hawapo kwa sasa maana lawi ni kabila lilitengwa maalum kwa utumishi hawakuwa wanamiliki chochote kazi yao ilikuwa hiyo tu sasa hawa wachungaji wana majumba magari mashamba nk wanakuwaje walawi

Kazi zao ni sawa na zile za walawi hakuna tofauti.
 
Kwanini ipelekwe huko na wasipewe ambao tunadhani wanahitaji

Kumpa mgonjwa akatibiwa nakupeleka msikitini kipi bora??

Hapa kuna walakin
Si msikitini wala kanisani,
Japo nimemueleza fungu la kumi linapaswa kupelekwa wapi.

Bora apeleke pesa kwa wenye uhitaji, personal ni bora apeleke kwa wenye uhitaji kuliko kupeleka pesa kwa kitu kinachodai ni muweza wa yote halafu ananiomba pesa yangu.
Kama atashindwa kufanya hivyo nimempa ushauri ale mbuzi choma au kitimoto mpaka pesa iishe.
 
Fungu la kumi ni kanisani, Kwa wenye uhitaji unapeleka msaada na huko pia Kuna baraka zake,na siyo kila sehemu ni pa kutoa Sadaka au fungu la kumi, maana utoapo ndipo ilipo hadhina ya moyo wako.Maana madhabahu yanaweza yakaharibu au kutengeneza maisha yako

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Kuliko kupeleka kwenge dhehebu bora kwa yatima
Maana halitamfikia Mungu ila litaingia kwenye miradi, na mifuko ya watu.
Alioaswa achukue mchungaji.

Hayo ni mawazo yako ila kanuni inataka fungu la 10 liende madhabahuni,kama unasali dhehebu usiloliamini hata kupeleka zaka basi tatizo ni wewe,ila zaka ni madhabahuni sadaka tumia utakavyo hakuna anayekuzuia.
 
Back
Top Bottom