Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Mungu anataka fungu la kumi la nini kama kila kitu ni chake na yeye ni muweza wa yote

Utii,pia fungu la kumi kuwezesha kazi ya utume na uinjilishaji,injili itawafikiaje mataifa bila kuenezwa?
 
Kama huwelewi maandiko omba uelekezwe,fungu la 10 lilitolewa maalumu kwa wana walawi waliokua ni makuhani na waangalizi wa hekalu,ambao hata katika urithi wa ardhi hawakupewa,hivyo ili waishi na kuendelea kuhudumia hekalu fungu la 10 lilipelekwa hekaluni
sasa walawi wanahusiana vipi na mimi msandawe?
Tena bora umetupa elimu nzuri.
 
Leteni zaka kamili Ili kiwemo chakula katika nyumba yangu....zaka ni ya Mungu peleka madhabahuni....wahitaj utawasaidia Kwa pesa tofaut na zaka
Acha uongo kwahiyo kanisa ni ghala?
 
Fungu la kumi sio sadaka ya agano jipya ni torati ile sasa kama unafuata torati ni wewe lakini nakuambia hakuna awezaye kuifuata torati kwa 100% umewahi kusoma kumb 14:22 mpaka inapoishia hiyo sura ndo utaelewa kuwa mnapigwa
 
Ndio utulie tuwekane sawa,huo utamaduni na muongozo uliingia hadi katika kanisa la kwanza la kristo,kila sehemu ya 10 ya mapato yalipelekwa kani sana ili kuipa nguvu kazi ya utume na uijilishaji,na hii inafanyika hadi sasa.

Bila hivyo kazi ya utume na uinjilishaji ingekuwa ngumu ndio maana kanisa linaendelea kusisitiza utoaji wa zaka kwa lengo hilo.

Wanawalawi kwa sasa hawapo ila ile kazi yao sasa ni sawa na inayofanyika katika kanisa la leo.
Kwahiyo zaka mnayotoa inafanya uinjilishaji na utume? Wapi umeona hii
 
Kumbukumbu 26:12

“Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;”
Soma na sura ya 14 anzia mstari wa 22 hadi mwisho pale
 
Mkuu hiyo ela pelekea watu wenye uhitaji, japo fungu la kumi linapaswa kwenda kanisani.

Nakuomba hiyo pesa pelekea watoto wenye kuishi mazingira magumu, kama utashindwa kufanya hivyo kula mbuzi choma mpaka hiyo pesa iishe.
Kama ni mkristo agiza kitimoto nusu nusu mpaka pesa iishe utaongeza afya na utapata nguvu ya kutafuta nyingine.
Kwanini ipelekwe huko na wasipewe ambao tunadhani wanahitaji

Kumpa mgonjwa akatibiwa nakupeleka msikitini kipi bora??

Hapa kuna walakin
 
Wasichojua watu ni kuwa walawi hawapo kwa sasa maana lawi ni kabila lilitengwa maalum kwa utumishi hawakuwa wanamiliki chochote kazi yao ilikuwa hiyo tu sasa hawa wachungaji wana majumba magari mashamba nk wanakuwaje walawi
 
Anayeona anamafundisho ya zaka aje nifanye nae battle tuanzie na hilo andiko lenu pendwa la malaki
 
Kuikamilisha maana yake TO PUT AN END OF. Kuweka NUKTA.. Biblia inasema Kristo ni MWISHO wa sheria. Wakristo hawapo chini ya Torati..

Pili, Kama mnafuata Torati kwa nini hamuifuati yote mnachagua tu fungi la kumi?

Tatu, wewe ni myahudi? Kabila lako ni lipi kati ya yale 12?

Mchungaji wako ni Kuhani? Ni kuhani wa kabila gani? Ni wapi Mungu amemuagiza mchungaji wako apokee zaka?
Wako brainwashed hawatakuelewa
 
KIBIBLIA fungu la kumi linatakiwa liende kanisani hakuna MBADALA ..hiyo inaitwa ZAKA (TITHES) maana yake ni kurudisha Kwa Mungu madhabahuni.....yatima ,masikini etc wanapelekewa sadaka..na makanisa mengi fungu la kumi ni Kwa ajili ya kulipa mishahara wachungaji ...wewe peleka kanisani umeshamaliza sehemu yako mbele za Mungu ...kama unadhani kanisa unalosali halistahili kupelekewa sadaka either ni la nabii fake etc basi unasali sehemu sio sahihi....Hifadhi vizuri ZAKA zako Kwa uaminifu tafuta kanisa sahii peleka...
Mafundisho ya wapi haya ni kwa mujibu wa maandiko gani
 
Watoto wa Mungu wanateswa sana na mafundisho manyonge imagine eti kuna riba kwenye zaka usipotoa yaani ni vichekesho lini Mungu alitaka riba?tukitutukia tu hiyo torati zaka inapaswa uile mwenyewe
 
Kumbukumbu la Torati 14 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²² Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
²³ Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.
²⁴ Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;
²⁵ ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;
²⁶ na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
²⁷ na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.
 
Fungu la Mungu au fungu la mchungaji? Hawa hawa manabii wetu wa siku hizi uwapelekee fedha halafu useme umepeleka kwa Mungu? Hawa hawa kina Gwajima na Mzee wa Upako au kina Mwamposa? Kina 'nabii'' Malisa?
Wengine wana hadi namba za lipa pesa!
 
Kama huwelewi maandiko omba uelekezwe,fungu la 10 lilitolewa maalumu kwa wana walawi waliokua ni makuhani na waangalizi wa hekalu,ambao hata katika urithi wa ardhi hawakupewa,hivyo ili waishi na kuendelea kuhudumia hekalu fungu la 10 lilipelekwa hekaluni
Hakuna Walawi bongo.
 
Back
Top Bottom