Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Duuu mjadala mtamu kweli, mtazamo wangu Mimi Ni huu kulingana na kumbukumbu la torati 12:5-17 inaelekeza zaka itolewe mahali atakapopachagua Bwana, kwa mfano mlawi, yatima, mjane, mgeni na Malaki 3:10 inaelekeza ghalani au kwenye nyumba ya Mungu au kanisani. Sasa utajuaje upeleke wapi? Ni lazima umpe Mungu kwanza ( yani unaiombea kwanza) na Kisha umuulize Mungu uipeleke wapi kwa wakati huo! Mfano Ibrahimu aliwahi kumpa Melkizedeki mfalme wa Salemu funhu la kumi, je alijuaje kuwa ampe, jibu ni kuwa aliambiwa na Mungu.

Kimbembe sasa kinakuja hapa Mungu akikujibu utajua? Asipokujibu pia utajua? Ili utoe zaka kikamilifu ni lazima uwe unaukaribu mno na Mungu, Ahsante.
 
Ulitaka apeleke wapi kwa muongozo upi,unaelewa hata maana ya kuanzishwa fungu la 10?
Kumbe sadaka tunazomtolea Mungu zina maana tofauti na kumshukuru yeye kwa kutupa neema ya uhai na maisha..... Kweli dini ililetwa kwaajili ya watu wenye akili ndogo.


Maandiko yapo elimu hamuitafuti
 
Matajiri wote duniani ambao ndio wameshikiria 90% ya fedha zote wakitoa Hiyo zaka 10% kwenye makanisa yao, itakuwaje ,
Je wao hubarikiwaje?
 
Ukweli mchungu uko hapa .Waamini wengi hawaambiwi kuwa zaka unaweza toa kwa watoto yatima au mjane au hata kwa mgeni..Tunatakiwa kukumbuka Mjane kwenye neno ameitwa kama mke wa Mungu na yatima kama watoto kwaiyo ukiwapa hawa unakuwa umetoa kwenye nyumba ya Mungu pia ukiwa..
Kumbukumbu 26:12

“Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;”
 
Fungu la kumi ni fungu la Mungu, peleka madhabahuni unapoabudia.
Kitabu cha Yoeli Mungu anasema mnaniibia kwa kutotoa zaka, leteni zaka kamili ghalani Ili kiwepo chakula nyumbani mwangu.

Misaada kwa yatima hiyo ni sadaka.
Malaki au Joel?
 
Je, fungu la kumi linaweza tolewa kwa wajane, yatima na wenye shida au ni lazima nikatoe kanisani?

Naomba hekima zenu juu ya hili.
Fungu la 10 ni fungu la Imani,,hivyo ukitaka kuona mafanikio Kwa kusudio la fungu la 10 ni vyema ukaandaa chakula kilichotukuka hrf unawaalika watoto wadogo na wazee ambao hawajiwezi Kisha mnakula pamoja kwakuongozwa na sala kulingana na Iman zao,, Mzee wangu ukifanya hivyo hata Kila mwez kulingana na uwezo wako ipo siku utakuja kutoa ushuhuda hapa!
 
Je, fungu la kumi linaweza tolewa kwa wajane, yatima na wenye shida au ni lazima nikatoe kanisani?

Naomba hekima zenu juu ya hili.
Hapana.
Fungu la kumi hutolewa pale unapohudumiwa kiroho, hiyo ni kodi ya Mungu, si kazi yqko kuipangia matumizi
 
yule kijana alimwambia yesu nifanye nini nipate kuurithi ufalme wa mbinguni? yesu akamwambia wazijua amri na kuzishika? Ndio! Ndipo akamwambia umepungukiwa na kimoja,kauze ulichonacho wagawie maskini ! Nahitimisha ivi hakuna sharti la kutoa fungu la kumi likawekewa na ahadi ya kuurithi ufalme wa mungu. nasubiri andiko lenye ahadi ya kwenda mbinguni...kwako studio
 
Kama huwelewi maandiko omba uelekezwe,fungu la 10 lilitolewa maalumu kwa wana walawi waliokua ni makuhani na waangalizi wa hekalu,ambao hata katika urithi wa ardhi hawakupewa,hivyo ili waishi na kuendelea kuhudumia hekalu fungu la 10 lilipelekwa hekaluni
Sasa kwanini Sisi ni Walawi ?
 
Kumbukumbu 26:12

“Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;”
Hili ndio suluhisho la kila baada ya nyumba kumi kuna kanisa
 
Kama kuna Deni ambalo Mungu ni lazima akulipe, tena una haki ya kudai pale ukifikwa na ya Dunia!

Basi ni kwenda kutia Misaada kwa Yatima, Wajane na wasio jiweza, iwe kwa Moyo mmoja, bila Makamera wala Matangazo!

Na ukianza kudai.... Hutumii nguvu nyingi....!

Unamwambia tu Mungu.... Basi naomba ukakumbuke Sadaka zangu nilizotoa kwa Yatima, Wajane na wasio jiweza.....! Mungu atalipa hilo deni.
 
Yani ipo tofaut tatzo wengi mnachanganya zaka na sadaka ...Yani kusaidia yatima na wasiojiweza ni muhimu pia zaka kupelekwa madhabahuni ni muhimu....fanyeni parts zote na sio Moja....kutii ni Bora kuliko dhabihu...
 
Fungu la Mungu au fungu la mchungaji? Hawa hawa manabii wetu wa siku hizi uwapelekee fedha halafu useme umepeleka kwa Mungu? Hawa hawa kina Gwajima na Mzee wa Upako au kina Mwamposa? Kina 'nabii'' Malisa?
Uko sahihi kiongozi wangu
 
Mkuu hiyo ela pelekea watu wenye uhitaji, japo fungu la kumi linapaswa kwenda kanisani.

Nakuomba hiyo pesa pelekea watoto wenye kuishi mazingira magumu, kama utashindwa kufanya hivyo kula mbuzi choma mpaka hiyo pesa iishe.
Kama ni mkristo agiza kitimoto nusu nusu mpaka pesa iishe utaongeza afya na utapata nguvu ya kutafuta nyingine.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Fungu la kumi ni fungu la Mungu, peleka madhabahuni unapoabudia.
Kitabu cha Yoeli Mungu anasema mnaniibia kwa kutotoa zaka, leteni zaka kamili ghalani Ili kiwepo chakula nyumbani mwangu.

Misaada kwa yatima hiyo ni sadaka.
Mungu anataka fungu la kumi la nini kama kila kitu ni chake na yeye ni muweza wa yote
 
Tuache upumbavu, Niliacha kutoa fungu la kumi mwaka 2018, nikiwa huko songea yaani unafuatwa hadi kazini kuletewa kibahasha cha kuwekea fungu la 10.

Ile hali nilivumilia miezi kama mitano hivi, baadae nikawa sipeleki aisee pastor yule alikuwa ananiongea sana mafumbo mwishowe nikaamua kusepa bila kuaga, alinipigia sana simu sikupokea.

1. Kila j5, ijumaa na jpili = SADAKA
2.Mchungaji alipanga nyumba kila mwisho wa mwezi SADAKA YA PANGO
3. Mchungaji akisafiri SADAKA YA NAULI
4. SADAKA YA UMISHENI kila mwisho wa mwezi
5. Michango ya ujenzi
6. Kumtegemeza mchungaji

Ndio maana nikichunguza kwenye makanisa mengi waumini ni maskini vibaya mno

Mkuu umasikini hauji kwa kutoa zaka na sadaka,acha uvivu fanya kazi,
 
Halipelekwi popote kwa sababu fundisho la Fungu la kumi ni fundisho la Torati.. na Wakristo hawapo chini ya torati.

In other words... Mungu hajatuagiza sisi tuliomfuata Yesu kutoa fungu la kumi... Fungu la Kumi sio fundisho la Kristo.

Kujaribu kulileta hili fundisho katika agano hili tunaloishi kwa sasa ni kulazimisha vitu ambavyo havipo.

Kristo alimaanisha nini kusema mpeni Mungu vyake Mungu na mpeni Kaisari vyake kaisari,je wafuasi wa kristo wanajifunza nini katika hilo andiko. ?
 
Back
Top Bottom