Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Ndio unaweza kulingana na kumbkumb la torati 26:12..neno la Mungu linasema zaka anaweza kupewa 1. mlawi(mtumishi wa Mungu) 2.mgeni(mhitaji) 3.yatima 4.wajane
Mlawi sio mtumishi wa Mungu. Mlawi ni mlawi... mtu wa kabila la Lawi... aliyewekwa kwa ajili ya kazi ya hekaluni.

Hao wachungaji wenu ni wa kabila la lawi?
Hao wachungaji wenu wanahudumu kwenye Hekalu gani?
 
KIBIBLIA fungu la kumi linatakiwa liende kanisani hakuna MBADALA ..hiyo inaitwa ZAKA (TITHES) maana yake ni kurudisha Kwa Mungu madhabahuni.....yatima ,masikini etc wanapelekewa sadaka..na makanisa mengi fungu la kumi ni Kwa ajili ya kulipa mishahara wachungaji ...wewe peleka kanisani umeshamaliza sehemu yako mbele za Mungu ...kama unadhani kanisa unalosali halistahili kupelekewa sadaka either ni la nabii fake etc basi unasali sehemu sio sahihi....Hifadhi vizuri ZAKA zako Kwa uaminifu tafuta kanisa sahii peleka...
Hakuna mahali Mungu ameagiza fungu la kumi liende kanisani. HAKUNA.

1. Fungu la kumi liliagizwa lipelekwe HEKALUNI. Kanisa sio hekalu.

2. Fungu la kumi likiagizwa lipokelewe na Kuhani wa kabila lawi. Mchungaji sio Kuhani na sio wa kabila la lawi.

Jifunzeni Biblia
 
KIBIBLIA fungu la kumi linatakiwa liende kanisani hakuna MBADALA ..hiyo inaitwa ZAKA (TITHES) maana yake ni kurudisha Kwa Mungu madhabahuni.....yatima ,masikini etc wanapelekewa sadaka..na makanisa mengi fungu la kumi ni Kwa ajili ya kulipa mishahara wachungaji ...wewe peleka kanisani umeshamaliza sehemu yako mbele za Mungu ...kama unadhani kanisa unalosali halistahili kupelekewa sadaka either ni la nabii fake etc basi unasali sehemu sio sahihi....Hifadhi vizuri ZAKA zako Kwa uaminifu tafuta kanisa sahii peleka...
Kasome tena mkuu uelewe falsafa ya Fungu la Kumi...
Kasome Kumbukumbu la Torati 14:27-29
Na pia soma.....
kumbukumbu 26:12-13

Ukimaliza njoo tena uangalie ulichoandika
 
Fungu la Mungu au fungu la mchungaji? Hawa hawa manabii wetu wa siku hizi uwapelekee fedha halafu useme umepeleka kwa Mungu? Hawa hawa kina Gwajima na Mzee wa Upako au kina Mwamposa? Kina 'nabii'' Malisa?
Hao hao mkuu
 
Nakubali kuhusu utoaji ila kwa Mkristo fungusla 10 halipo maana halituhusu, ila unaweza ukatoa nzuri zaidi ya fungu la 10
 
Fungu la kumi ni fungu la Mungu, peleka madhabahuni unapoabudia.
Kitabu cha Yoeli Mungu anasema mnaniibia kwa kutotoa zaka, leteni zaka kamili ghalani Ili kiwepo chakula nyumbani mwangu.

Misaada kwa yatima hiyo ni sadaka.
Ukishataja tu kitabu cha yoeli ni kutukuza ujinga na upumbavu.

Hakuna fungu la kumi la mali uliyochuma bali ni UNYONYAJI kama unyonyaji mwingine walioanzisha wakoloni ili kujiongezea mwanya wa kuwanyonya WAAFRIKA.

BIBLIA ni kitabu cha mwongozo wa UKOLONI kilichosimamia kuwaibia WAAFRIKA.

Pesa/mali zilizopokelewa kama fungu la 10 zilitumika pia kuendeleza ukoloni kupitia makanisani na nyingine kupelekwa ulaya.

Swali langu ni kitaka kujua hao wachungaji na maaskofu wanaojilimbikizia mali wanazipata wapi na je wanatoa fungu la 10 lao wapi?

WAAFRIKA acheni ujinga toa kwa WAHITAJI wajane,maskini,wagojwa,wagane,machokolaa,wafungwa,wazee,nk utapata baraka sana

MUNGU hawezi kumpa MUHITAJI WAKE pesa/mali halafu amtoze kodi/riba ,HAKUNA kitu kama hicho kwani anatambua hali zao jawana kitu hivyo hawezi kuchukua chochote kutoka ktk alichowabari.

Naimani wewe ni mmoja wa vibaka mnaowaibia WAHITAJI kwa kigezo cha SADAKA,ZAKA na FUNGU la 10 acheni hiyo tabia na fanyeni kazi mjipatie riziki kihalali siyo kuwaibia wahitaji.

MUNGU wa kweli alishabariki kila kazi ya mikono yetu hivyo haitaji chochote kutoka kwetu zaidi ya sisi kumuomba na yeye kutupatia.

Watu weupe wamekuwa wakitoa misaada sana KWA WAHITAJI hasa kipindi cha majanga au magonjwa kuliko WAAFRIKA,kwanini wasitoe fungu la 10?

Ni wakati sasa fungu la 10,sadaka na zaka zirudi kwa WAHITAJI siyo kuingia kwenye matumbo ya wachungaji na maaskofu wanao jimilikisha mali za MASKINI kwa visingizio na familia zao.
 
Back
Top Bottom