Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Je, naweza kutumia fungu la kumi kwa kununua mahitaji ya watoto yatima?

Exactly. Linatakiwa lipelekwe HEKALUNI... Na walikuwa wanapeleka Hekaluni Yerusalemu, sio kwenye masinagogi ya mitaani kwao.

Makanisa sio mahekalu... ni majengo ya kuabudia kama yalivyokuwa masinagogi wakati ule.

Hili jambo la kupeleka Zaka kanisani halina basis yoyote ya maandiko in any way kwa sababu hata hekalu la kutolea hiyo zaka halipo.

Kwanini ilikua inapelekwa hekaluni kwa malengo gani hasa ilitumikaje?
 
Katika agano jipya lililofanyika kwa damu ya Yesu, Hakuna mahali popote Mungu amekuagiza wewe utoe fungu la kumi.

Fungu la kumi ni fundisho la Torati. Watu walio chini ya Kristo hawapo chini ya torati. Sasa wewe unatoka wapi na mambo ya fungu la kumi?

Yesu hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza,ndio mana alisema mpeni Mungu vilivyo vyake na mpeni kaisari vilivyo vyake,bado alikazia kuhusu wayahudi kupeleka zaka fungu la kumi hekaluni na pia wasiache kulipa kodi kwa serikali ya roma.
 
Tatizo Kuna watumishi wengi sana wa uongo ambao wanapotosha kweli...ila madhabahu za kweli zipo mfano Lutheran church
Acha zako makanisa yote yamekuwa kama sehemu ya wizi, waumini wamejitaidi sana kufungua vitega uchumi vya kanisa, makanisa saivi yanamiradi mingi sana ila bdo yanazidi kutaka zaidi na zaidi kutoka kwa waumini bora iyoo pesa apeleke kwa yatima
 
Fungu la kumi ni fungu la Mungu, peleka madhabahuni unapoabudia.
Kitabu cha Yoeli Mungu anasema mnaniibia kwa kutotoa zaka, leteni zaka kamili ghalani Ili kiwepo chakula nyumbani mwangu.

Misaada kwa yatima hiyo ni sadaka.
Ila hutopungukiwa kwa kutoa sadaka badala ya zaka. Mungu atakujazia thawabu.
 
Tuache upumbavu, Niliacha kutoa fungu la kumi mwaka 2018, nikiwa huko songea yaani unafuatwa hadi kazini kuletewa kibahasha cha kuwekea fungu la 10.

Ile hali nilivumilia miezi kama mitano hivi, baadae nikawa sipeleki aisee pastor yule alikuwa ananiongea sana mafumbo mwishowe nikaamua kusepa bila kuaga, alinipigia sana simu sikupokea.

1. Kila j5, ijumaa na jpili = SADAKA
2.Mchungaji alipanga nyumba kila mwisho wa mwezi SADAKA YA PANGO
3. Mchungaji akisafiri SADAKA YA NAULI
4. SADAKA YA UMISHENI kila mwisho wa mwezi
5. Michango ya ujenzi
6. Kumtegemeza mchungaji

Ndio maana nikichunguza kwenye makanisa mengi waumini ni maskini vibaya mno
 
Kwahizo fungu la 10 linapelekwa kwenye hekalu la mwilini au sio[emoji28]
Halipelekwi popote kwa sababu fundisho la Fungu la kumi ni fundisho la Torati.. na Wakristo hawapo chini ya torati.

In other words... Mungu hajatuagiza sisi tuliomfuata Yesu kutoa fungu la kumi... Fungu la Kumi sio fundisho la Kristo.

Kujaribu kulileta hili fundisho katika agano hili tunaloishi kwa sasa ni kulazimisha vitu ambavyo havipo.
 
Yesu hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza,ndio mana alisema mpeni Mungu vilivyo vyake na mpeni kaisari vilivyo vyake,bado alikazia kuhusu wayahudi kupeleka zaka fungu la kumi hekaluni na pia wasiache kulipa kodi kwa serikali ya roma.
Kuikamilisha maana yake TO PUT AN END OF. Kuweka NUKTA.. Biblia inasema Kristo ni MWISHO wa sheria. Wakristo hawapo chini ya Torati..

Pili, Kama mnafuata Torati kwa nini hamuifuati yote mnachagua tu fungi la kumi?

Tatu, wewe ni myahudi? Kabila lako ni lipi kati ya yale 12?

Mchungaji wako ni Kuhani? Ni kuhani wa kabila gani? Ni wapi Mungu amemuagiza mchungaji wako apokee zaka?
 
Je, fungu la kumi linaweza tolewa kwa wajane, yatima na wenye shida au ni lazima nikatoe kanisani?

Naomba hekima zenu juu ya hili.
Fungu la kumi peleka kanisani ujue na kanisani hilo fungu hali mchungaji lote, Kuna fungu linabak kwa ajili ya wahitaji na wajane, Mungu ameelekeza fungu la kumi liende kwa makuhani na walawi na wao wana maagizo juu ya hilo fungu
 
Tuache upumbavu, Niliacha kutoa fungu la kumi mwaka 2018, nikiwa huko songea yaani unafuatwa hadi kazini kuletewa kibahasha cha kuwekea fungu la 10.

Ile hali nilivumilia miezi kama mitano hivi, baadae nikawa sipeleki aisee pastor yule alikuwa ananiongea sana mafumbo mwishowe nikaamua kusepa bila kuaga, alinipigia sana simu sikupokea.

1. Kila j5, ijumaa na jpili = SADAKA
2.Mchungaji alipanga nyumba kila mwisho wa mwezi SADAKA YA PANGO
3. Mchungaji akisafiri SADAKA YA NAULI
4. SADAKA YA UMISHENI kila mwisho wa mwezi
5. Michango ya ujenzi
6. Kumtegemeza mchungaji

Ndio maana nikichunguza kwenye makanisa mengi waumini ni maskini vibaya mno
Dah nimecheka sana eti unafatwa kazini na kibahasha 😀😀😅😅🤣🤣🤣

"""2.Mchungaji alipanga nyumba kila mwisho wa mwezi SADAKA YA PANGO
3. Mchungaji akisafiri SADAKA YA NAULI
4. SADAKA YA UMISHENI kila mwisho wa mwezi
5. Michango ya ujenzi
6. Kumtegemeza mchungaji"""

🤣🤣😂😂😂😂
 
Yesu hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza,ndio mana alisema mpeni Mungu vilivyo vyake na mpeni kaisari vilivyo vyake,bado alikazia kuhusu wayahudi kupeleka zaka fungu la kumi hekaluni na pia wasiache kulipa kodi kwa serikali ya roma.
Hakuna sehemu yesu amezungumxia Zaka mkuu acha kuongopa...
Hivi huwa hamuoni Aibu kuongopa kwa ajiki ya maslahi yenu binafsi
 
Je, fungu la kumi linaweza tolewa kwa wajane, yatima na wenye shida au ni lazima nikatoe kanisani?

Naomba hekima zenu juu ya hili.
Mimi binafsi nina kanuni Moja.

Sadaka Nasikiliza moyo wangu na sio sheria ya Dhehebu langu.

Fungu la kumi nina peleka kwa watoto yatima au wazazi wangu huko kijijini.
 
Kwanini ilikua inapelekwa hekaluni kwa malengo gani hasa ilitumikaje?
Makabila yote 11 ya Israel yalipewa urithi.. isipokuwa kabila la Lawi peke yao ndio hawakupewa urithi... wao urithi wao ulikuwa ni kazi ya hekaluni, kumtumikia Mungu...kwa sababu Wao walikuwa makuhani.

Hivyo Zaka ilipelekwa hekaluni ili kabila la lawi ambao ni makuhani waweze kupata riziki yao kutoka katika zile kabila 11.

In other words..kabila 11 ambazo zilikuwa na urithi zilichangia kabila 1 la lawi ambalo lenyewe lilikuwa na kazi special hekaluni.
 
KIBIBLIA fungu la kumi linatakiwa liende kanisani hakuna MBADALA ..hiyo inaitwa ZAKA (TITHES) maana yake ni kurudisha Kwa Mungu madhabahuni.....yatima ,masikini etc wanapelekewa sadaka..na makanisa mengi fungu la kumi ni Kwa ajili ya kulipa mishahara wachungaji ...wewe peleka kanisani umeshamaliza sehemu yako mbele za Mungu ...kama unadhani kanisa unalosali halistahili kupelekewa sadaka either ni la nabii fake etc basi unasali sehemu sio sahihi....Hifadhi vizuri ZAKA zako Kwa uaminifu tafuta kanisa sahii peleka...
 
Fungu la kumi peleka kanisani ujue na kanisani hilo fungu hali mchungaji lote, Kuna fungu linabak kwa ajili ya wahitaji na wajane, Mungu ameelekeza fungu la kumi liende kwa makuhani na walawi na wao wana maagizo juu ya hilo fungu
Ni wapi uliwahi kuagizwa wewe hapo upeleke fungu la kumi kanisani?

Ni wapi mchungaji wako amewahi kuagizwa apogee fungu la kumi?
 
Back
Top Bottom