Kwa story za vijiweni.Kuna swali huwa ninalojiuliza sana peke yangu, naomba nishare hapa
Utasikia watu wakisema ulimwengu wa roho, ulimwengu wa siri. Hivi huo ulimwengu huwa ni upi?
Je, mambo ya ulimwengu wa roho au ulimwengu wa siri huwa ni pamoja na ndoto tunazoota usiku au mchana?
Au tuseme ndoto huwa ni dunia au ulimwengu mwingine?
Kwa sababu unapoota ndoto huwa ni kama upo kwenye ulimwengu au dunia nyingine. Maana unakuwa umelala, lakini ni kama bado kuna mambo yanaendelea kwenye akili yako
Wengine husema ndoto huwa ni matokeo ya mawazo, msongo wa mawazo uliozidi, maongezi au vitendo vya muda fulani
Ndiyo huwa ubongo unakuwa kama unarudi kwenye yale mambo
Mimi binafsi nakiri kuna ndoto zingine mtu huota huwa ni matokeo ya mawazo, shughuli za kutwa nzima au kile akili inachowaza au inachokitamani kifanyike
Unajikuta ukiota hivyo, na unapoamka unajua kabisa hizi ni fikra za mchana kutwa na mawazo tu
Au kuota mambo ya zamani, mfano shule, marafiki wa utotoni n.k. Na hii ya shule wengi wanasema wameota, ila mimi sijawahi kuota kabisa ndoto ya shule
Ninakuwa tu na ndoto zangu kivyangu, ambazo sioni hata watu wakizizungumzia
Swali linakuja kwenye ndoto ambazo nitaziita prophetic dreams, kwa sababu ni ndoto unaota kitu kitakachotokea mbele
Nasisitiza, kitu kitakachotokea mbele. Unakuta siku moja kabla au siku mbili kabla
Hii inanifanya nawaza sana, hivi huwa ni kitu gani kinatokea?
Yaani unaota ndoto kuhusu kitu fulani, halafu kikitokea unakuwa shocked 😲
Ukimwambia mtu haamini, anaona ni uongo, kama unapenda kujifanya special
Hivyo unabaki nayo mwenyewe
Pia kuna mtu ana uwezo wa kusoma mtu anachokiwaza
Yaani mfano ukiwa unachat na mtu unaweza ukawa unahisi huyu fulani ana nia fulani, aidha ana chuki fulani dhidi yangu, japo anaweza kuwa anapretend love
Na kweli hatachukua muda mrefu anajifunua rangi zake halisi
Lakini point kubwa hapa ni, inakuaje mtu anaota mambo yajayo? Ni nini huwa kinatokea??
Au huo ndio huitwa ulimwengu wa roho au wa siri?
Nitatoa mfano. Kuna ndoto niliota kuhusu watu fulani
Hao watu sikuwahi kuwajua kabla na hakuna namna ningewajua
Ila ajabu, hiyo ndoto niliyoota na majina yao kwenye ndoto, nilivyokuja kufahamu baadaye ilikuwa the same names
Yaani hata kama ningemwambia mtu asingeelewa, angesema nataka sifa
Niliwahi kuishi na mtu fulani
Huyo nilikuwa namwambia sana, Nimeona hivi katika ndoto kuhusu wewe,na kweli baada ya siku anakutana na situation kama hizo
Akawa ananiuliza, Wewe ni mganga au mchawi?😢😂
Ni mambo mengine mengi, ila hayo machache yanaeleweka
Je, kuna wengine wapo hivi?
Huota mambo halisi kabisa?
Nini sababu?
Faida au hasara?
Welcome Guy's
ShesRise_1 🤚
Wanasema mtu anapokuwa amekula sana chakula kingi usiku halafu muda ukiwa tayari unakaribia midnight ndipo anapokuwa kwenye nafasi kubwa ya kuota ndoto za ajabu ajabu kwa kile chakula kingi cha late nite hakina faida yoyote zaidi ya kusababisha imbalance tu