Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Sehemu za asili.. kwenye miti mbalimbali ambayo bado tafiti zinaendelea..mbali na hewa safi .. Kuna baadhi ya mimea hutoa tiba za kimwili kwa kutoa kemikali mbalimbali ambazo ukivuta na kuingia kwenye mfumo wa hewa mwili huzibeba kwa manufaa flani flani ..
Mimea au miti huongeza activity flani ndani ya Ubongo..na ukizoea basi Ubongo wako unatengeneza hali kama hizo..
Hapa umezungumzia mchakato wa kujitambua kiroho au umezungumzia mchakato wa neurochemical stimulation?
 
Ukienda mbugani kutalii ambapo akili inajua na imeshajiwekea kwamba mazingira ya mbugani (porini) huwa kuna wanyama na wadudu hatari.

Halafu ukiwa Vacation mbugani, ukaota nyoka anakung'ata, lakini kiuhalisia hajakung'ata ni ndoto tu.

Ukaendelea kutalii mbugani hapo kwa siku kadhaa, Halafu ghafla Nyoka akakung'ata.

Utasema ndoto yako uliyoota kabla imetimia kiroho kwa mambo yajayo?

Au akili yako imesha jijenga kwamba kiuhalisia mazingira ya mbugani huwa wanaishi wadudu hatari kama nyoka ndio maana ukaota ndoto kabla ya kung'atwa?
 
Hapa Jf...Kuna mtu aliwahi kuandika ameota ndege imeanguka... Ila hajui ni wapi...baada ya wiki mbili au tatu .. Precision air ilianguka Bukoba.... Watu walijiuliza sana wakakosa majibu
Alionyeshwa ni lini hiyo ndege itaanguka , wapi? na ni ndege ya aina gani?

Mfano mimi kesho niamke, nianzishe uzi kwa kudai kuwa nimeota ndani ya hii week Morogoro road kutatokea ajali, halafu kabla week haijaisha ajali itokee maana yake mtaniamini si ndiyo?
 
Mimi niko kwenye neurochemical stimulation....
Nguvu ya Ubongo inapokutana na mazingira mazuri ..tegemea maajabu
Neurochemical stimulation ndiyo inayozalisha maono au inatengeneza mazingira mazuri tu ya kuipokea taarifa ambayo tayari ipo kwenye universal field?
 
Hayo mambo huwa yanatisha sana ,Juzi kuna kitu kilinijia kwenye brain ambalo linahusu mtu mwingine ,baada ya muda from no where naye huyo mtu anakaniuliza kitu hicho hicho ambacho na mimi kilinijia akilini na si kwamba alishawahi kuniuliza hapana ndiyo mara ya kwanza kuuliza hicho kitu.

KUna mtu wangu pia wa karibu huwa anaona vitu mbele ,akiona kitu kwenye ndoto huwa kinatokea ,sasa baada ya kuona vitu mbele ya muda basi wazee wakamshauri akiota kitu kibaya basi akistuka aamke na akemee ili kisije kutokea.
 
Katika mwili wa binadamu Kuna vitu vingi bado havijagunduliwa jinsi vinavyofanya kazi...

Mfano Ubongo wa binadamu ni very complex kiasi kwamba..ugunduzi wa mambo mbalimbali bado unaendelea kuvumbuliwa..

Ndio maana ndoto binadamu anazoota Kuna vitu vinafanyiwa research...

Kuna watu wakiota ndugu yake labda anaumwa... Kesho yake wakipiga simu wanaambiwa alikuwa hoi kapata nafuu

Au hata sio ndoto tuu.. Kuna watu Ubongo unampa hisia tuu..ondoka hapa.. baadae mnasikia sehemu imevamiwa au Kuna shida imetokea eneo Hilo

Ila sio Kila mtu Ubongo wake unaweza haya mambo.. na ndio maana Kuna tafiti zinafanyika ili kujaribu kuangalia Ubongo wa binadamu na mazingira yake

Wataalamu wa tafiti wanasema Kuna extra sense..(mlango wa ziada wa fahamu) hasa ndoto au hisia ya kitu ambacho ukioni lakini Ubongo unakupa taarifa hasa katika hali ya utulivu sana
Usiseme ubongo sema roho acha kuchanganya kuwa straight wanaopata ajali je hawana ubongo
 
Naweza kuongezea kidogo...

Ukiwa mtu wa asili sana ..(nature) mfano Kwenda sehemu za utulivu sana kwenye mito inayotiririsha maji, kwenye miti , kusikiliza sauti za ndege nk
Basi Ubongo unapokea Yale mazingira na kujiunganisha na asili

Ubongo ukipata utulivu na ukaenda sehemu kama hizi..zenye miti mbalimbali basi hewa ya oxygen inakuwa katika concentration kubwa..

Ubongo ukipata hewa safi mara kwa mara.. kwa utulivu basi pole pole utaanza kupata ndoto za ishara flani flani... Au hata extra sense (Machale) ya kitu Cha hatari
Lakini usiwe mlevi wa chakari..kwakuwa ukilewa chakari ..huwezi kupata ndoto za ishara flani flani

Sehemu za asili.. kwenye miti mbalimbali ambayo bado tafiti zinaendelea..mbali na hewa safi .. Kuna baadhi ya mimea hutoa tiba za kimwili kwa kutoa kemikali mbalimbali ambazo ukivuta na kuingia kwenye mfumo wa hewa mwili huzibeba kwa manufaa flani flani ..
Mimea au miti huongeza activity flani ndani ya Ubongo..na ukizoea basi Ubongo wako unatengeneza hali kama hizo...

Na ndio maana baadhi ya watu anaweza Kukaa mjini akaona mambo hayaendi..anasema naenda kijijini mara Moja... Huko anaenda kutuliza Ubongo katika utulivu katika mazingira ya asili na kupata hewa safi (chakula kikuu Cha Ubongo) na kujaribu kuangalia amekosea wapi...na Ubongo humpa mawazo chanya ya Nini kifanyike
Shukrani sana umeandika vizuri sana
Mimi pia navutiwa na mazingira tulivu yenye uoto asili hua nahisi hali fulani ya raha kuangalia au kutembelea sehem kama hizo

Asantee🥰
 
Alionyeshwa ni lini hiyo ndege itaanguka , wapi? na ni ndege ya aina gani?

Mfano mimi kesho niamke, nianzishe uzi kwa kudai kuwa nimeota ndani ya hii week Morogoro road kutatokea ajali, halafu kabla week haijaisha ajali itokee maana yake mtaniamini si ndiyo?
Aliota ndotoni...akasema nimeota....
Sio kuonyeshwa ni lini...

Sasa wewe ukianzisha uzi...kwamba umedai Ajali ... Morogoro hiyo sio ndoto Bali umedai
Na wewe huna uwezo wa kupata ndoto za maono..wenye hiyo huwa hawasemi
Au wakisema ni kutoa tahadhari
 
ndoto ni tukio lililondani ya timeline yaan past,present,future. ko ndoto inaweza kuwa past oriented(experience) ama future oriented(maono)
Ahaaa sawa
hii iko connected na other dimension beings wanaokushushia taharifa hawa n matime traveller wanakuchunga mwanao uloko duniani usipotee.
Niambie kuhusu time traveller na namna inavyofanya kazi

Inafanya kazi kwa watu gani
Kwa malengo gani na faida zake
 
Mkuu ndoto zinahitaji tafsiri kwa uzoefu wako kivipi huwa unaweza kutofautisha kati ya tafsiri sahihi ya kiroho na tafsiri inayochochewa na hofu au matamanio yako binafsi?
Kila mtu anajua matamanio yake mkuu hata wewe pia unajua unachotamani unachowaza
Yani ni kipimo gani huwa unatumia kuhakikisha kuwa tafsiri yako siyo bias?
Na hapa nimezungumzuia zile ndoto ambazo baadae hugeuka halisi
Na hizi ndio naziongelea hasa
Na nimeuliza kwa sababu inafikirisha namna mtu aote kitu leo na kitokee wiki ijayo
 
Kuna swali huwa ninalojiuliza sana peke yangu, naomba nishare hapa

Utasikia watu wakisema ulimwengu wa roho, ulimwengu wa siri. Hivi huo ulimwengu huwa ni upi?

Je, mambo ya ulimwengu wa roho au ulimwengu wa siri huwa ni pamoja na ndoto tunazoota usiku au mchana?
Au tuseme ndoto huwa ni dunia au ulimwengu mwingine?

Kwa sababu unapoota ndoto huwa ni kama upo kwenye ulimwengu au dunia nyingine. Maana unakuwa umelala, lakini ni kama bado kuna mambo yanaendelea kwenye akili yako

Wengine husema ndoto huwa ni matokeo ya mawazo, msongo wa mawazo uliozidi, maongezi au vitendo vya muda fulani

Ndiyo huwa ubongo unakuwa kama unarudi kwenye yale mambo

Mimi binafsi nakiri kuna ndoto zingine mtu huota huwa ni matokeo ya mawazo, shughuli za kutwa nzima au kile akili inachowaza au inachokitamani kifanyike

Unajikuta ukiota hivyo, na unapoamka unajua kabisa hizi ni fikra za mchana kutwa na mawazo tu

Au kuota mambo ya zamani, mfano shule, marafiki wa utotoni n.k. Na hii ya shule wengi wanasema wameota, ila mimi sijawahi kuota kabisa ndoto ya shule

Ninakuwa tu na ndoto zangu kivyangu, ambazo sioni hata watu wakizizungumzia

Swali linakuja kwenye ndoto ambazo nitaziita prophetic dreams, kwa sababu ni ndoto unaota kitu kitakachotokea mbele

Nasisitiza, kitu kitakachotokea mbele. Unakuta siku moja kabla au siku mbili kabla

Hii inanifanya nawaza sana, hivi huwa ni kitu gani kinatokea?

Yaani unaota ndoto kuhusu kitu fulani, halafu kikitokea unakuwa shocked 😲

Ukimwambia mtu haamini, anaona ni uongo, kama unapenda kujifanya special

Hivyo unabaki nayo mwenyewe

Pia kuna mtu ana uwezo wa kusoma mtu anachokiwaza

Yaani mfano ukiwa unachat na mtu unaweza ukawa unahisi huyu fulani ana nia fulani, aidha ana chuki fulani dhidi yangu, japo anaweza kuwa anapretend love

Na kweli hatachukua muda mrefu anajifunua rangi zake halisi

Lakini point kubwa hapa ni, inakuaje mtu anaota mambo yajayo? Ni nini huwa kinatokea??

Au huo ndio huitwa ulimwengu wa roho au wa siri?

Nitatoa mfano. Kuna ndoto niliota kuhusu watu fulani

Hao watu sikuwahi kuwajua kabla na hakuna namna ningewajua
Ila ajabu, hiyo ndoto niliyoota na majina yao kwenye ndoto, nilivyokuja kufahamu baadaye ilikuwa the same names

Yaani hata kama ningemwambia mtu asingeelewa, angesema nataka sifa

Niliwahi kuishi na mtu fulani
Huyo nilikuwa namwambia sana, Nimeona hivi katika ndoto kuhusu wewe,na kweli baada ya siku anakutana na situation kama hizo

Akawa ananiuliza, Wewe ni mganga au mchawi?😢😂

Ni mambo mengine mengi, ila hayo machache yanaeleweka

Je, kuna wengine wapo hivi?

Huota mambo halisi kabisa?

Nini sababu?

Faida au hasara?

Welcome Guy's
ShesRise_1 🤚
Binafsi nimekuelewa sana, na hilo lipo kwa watu wachache sana

Hilo ni suala la kiroho, una karama ya Unabii, Nabii ni Mtu anayeweza ku foresee na ku foretell

Kuna wanaojiita Manabii ila inaishia kujiita tu ili wapate umaarufu na kutimiza haja zao za kupata pesa,ilq hawajajaliwa karama hiyo

Wewe umejaliwa, ukitumika vizuri kwa Mwenyenzi Mungu utakuwa msaada kwa watu wengi

Kingine, unaweza kuja kupredict hata kifo chako.

Zingatia hayo niliyokueleza.
 
Ukienda mbugani kutalii ambapo akili inajua na imeshajiwekea kwamba mazingira ya mbugani (porini) huwa kuna wanyama na wadudu hatari.

Halafu ukiwa Vacation mbugani, ukaota nyoka anakung'ata, lakini kiuhalisia hajakung'ata ni ndoto tu.

Ukaendelea kutalii mbugani hapo kwa siku kadhaa, Halafu ghafla Nyoka akakung'ata.

Utasema ndoto yako uliyoota kabla imetimia kiroho kwa mambo yajayo?

Au akili yako imesha jijenga kwamba kiuhalisia mazingira ya mbugani huwa wanaishi wadudu hatari kama nyoka ndio maana ukaota ndoto kabla ya kung'atwa?
Yaani hapa hata hujaelewa naongelea nini huo mfano uliotoa na msingi wa swali langu ni mbingu na ardhi

Nimesema hivi mf : mtu aote ndugu yake amepata ajali na kufa hapo hapo
Na wakati huo hajaongea nae chochote kuhusiana na safari au hajaongea nae hata kwa miezi then apigiwe simu aambiwe ndugu yako amapata ajli na amefariki wewe huoni kama mfano wako haufanani?
 
Binafsi nimekuelewa sana, na hilo lipo kwa watu wachache sana

Hilo ni suala la kiroho, una karama ya Unabii, Nabii ni Mtu anayeweza ku foresee na ku foretell

Kuna wanaojiita Manabii ila inaishia kujiita tu ili wapate umaarufu na kutimiza haja zao za kupata pesa,ilq hawajajaliwa karama hiyo

Wewe umejaliwa, ukitumika vizuri kwa Mwenyenzi Mungu utakuwa msaada kwa watu wengi

Kingine, unaweza kuja kupredict hata kifo chako.

Zingatia hayo niliyokueleza.
Nashukuru sana umenielewa ila kuhusu mambo ya nabii sijui kuhusu hayo

Ila ni kweli mara nyingi hua naona baadhi ya mambo kabla hayajatokea ila kwa kua mtu hukumwambia kabla haamini anaona unajikweza

Nb siwezi kusema kila kitu ila swali langu lilikua nini hua kinatokea mpka unapata ndoto halisi
 
Nimekuelewa. Sasa ni nani atawajibika kwa madhara yanayopata watu? Majanga. Shida. Tabu na dhiki.

Whom to blame?.
Kama hakuna anayewajibika, kwanini kuna haki?

Lawama ndiyo kitu pekee kinachotutofautisha na wanyama.

Tukiachana na lawama basi unapaswa kukubalia agency Mkuu.
 
Back
Top Bottom