Kupata ajali si jambo geni kwa akili ya mwanadamu.
Akili yako tayari inajua kwamba ajali zipo na huweza kutokea kwa yeyote muda wowote.
Kuota ndugu yako anapata ajali, hakufanyi apate ajali kweli.
Kwa hiyo Kuota ndoto na Kupata ajali ni Mutually exclusive events.
Ni matukio mawili ambayo hayawezi kutokea kwa pamoja kwa wakati mmoja.
Ndugu yako anaweza kupata ajali bila wewe kuota.
Kuota leo ndugu yako amepata ajali, halafu ipite siku, wiki, mwezi au mwaka halafu ndugu yako aje Kupata ajali kweli. Hakufanyi ndoto yako uliyoota kabla iwe ndio imetimia.