Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Na wale wanaoota vitu ambayo hawajawahi hata kuviona au kuvifahamu halafu baadae inatokea kweli inakuwaje?
Unajua kipofu,kiziwi nao wanaota ndoto?
akili ndo inatengeneza mambo yote hayo

Ndo maana ni kazi kutofautisha ndoto na maisha halisi
Inawezekana hata nakujibu hapa nipo ndotoni

Kwenye ndoto tunapambana kama vile tupo kwenye maisha halisi
So ipi ni ndoto na ipi ni halisi?
Mimi naamini nikifa ntazinduka ndotoni!
 
Kuna nadharia ya kifalsafa inasema kuwa muda siyo mstari ulionyooka kama tunavyouona, sisi huwa tunaona jana - leo - kesho lakini inawezekana fahamu zetu zina uwezo wa kugusa tukio ambalo lipo mbele kidogo ya huo mstari wa muda, naamanisha mbele kabisa ya kesho au kesho kutwa.
Hapa naweza kukuelewa umeongea kitu kinafafana sana au kinaendana na tukio husika Shukran
Kwahiyo ndoto zinaweza kuwa ni kuteleza kidogo kwa ubongo wako kuona kitu ambacho kipo kwenye future timeline yako, hapa siyo lazima iwe ni imani ya kidini, inaweza kuwa ni uwezo wa ubongo wako kuona probabilistic outcomes kabla hayajatokea kwenye uhalisia.
Aiseee natamani kujua zaidi ila naona ni kasheshe
 
Je Kiranga una maoni gani hapa?

Ndoto ni mkusanyiko wa mawazo yetu.

Kuna namna fulani tunayaona mambo, tunayasikia, tunayafahamu, bila kuyapa umuhimu, halafu nawazo hayo yanaingia katika subconscious minds zetu, halafu tunayaota, halafu yanakamilika, halafu tunashangaa hili jambo nimeliota, halafu likatokea.

Kumbe liliingia mawazoni kwa kusikia, kuwaza, kuona kwa namna fulani, ambako hatukukupa umuhimu.

Ndiyo unaweza kukuta mtu anatembea, akausikia wimbo fulani redioni, bila ya mawazo yake kujua kikamilifu kuwa kausikia huo wimbo, akausikia tu kwa subconscious mind. Halafu akaanza kupiga mluzi wa huo wimbo, halafu sasa akapata nafasi ya kuusikia vizuri huo wimbo akatambua kuwa huo wimbo imekuwaje aanze kupiga mluzi wake tu, halafu hapo hapo wimbo uwe unapigwa redioni?

Kumbe hapo alianza kuusikia wimbo bila kujua kausikia (subconscious mind), akapiga mluzi wa huo wimbo kutoka subconscious mind, halafu ndiyo akausikia vizuri kutoka redioni.

Asipoelewa hapo anaweza kufikiri ana nguvu za kutabiri wimbo utakaopigwa redioni.

Hivyo hivyo, mfano una mzee wako yuko mbali anaumwa, familia inamuongelea sana, unaweza kufikiri huyu mzee hana muda mrefu wa kuishi, ukaota ndoto amefariki, lakini hata usiikumbuke ile ndoto.

Ila, ukiota ndoto kafariki, halafu kesho yake akafariki kweli, utaikumbuka tu ile ndoto.
 
Unajua kipofu,kiziwi nao wanaota ndoto?
akili ndo inatengeneza mambo yote hayo

Ndo maana ni kazi kutofautisha ndoto na maisha halisi
Inawezekana hata nakujibu hapa nipo ndotoni

Kwenye ndoto tunapambana kama vile tupo kwenye maisha halisi
So ipi ni ndoto na ipi ni halisi?
Mimi naamini nikifa ntazinduka ndotoni!
😂😂😂 leo lazima nichanganyikiwe na nipo tayali kuchanganyikiwa
Marcostilone
 
Nadhan ishu sio muhusika.
Ishu ni anawajibikaje?.

Sisi binadamu tunawajibikaje?.

Weka maanani kuna matetemeko ,vimbunga, volcano ambayo ni nature. Na ambayo yanatuathiri binadamu.
Mtu anayejenga nyumba kwenye njia ya mafuriko au kwenye eneo lenye hatari ya tetemeko bila kuchukua tahadhali, huyo atawajibika kwa madhara yatakayotokea.

Uwajibikaji wetu uko kwenye sayansi ya ujenzi na early warning systems, tunaposhindwa kutumia akili tuliyopewa kujikinga na majanga yanayotabirika, basi sisi wenyewe tunakuwa sehemu ya tatizo.
 
Na wameshindwa kutofautisha hapa hapa hatuongelei hizo ndoto za stress na kazi za kila siku

Issue nikuota kitu ambacho hakijatokea na mwisho kinatokea vile vile
Tena kitu ambacho ukuwahi kuwaza
wala hukuwahi kukijua

MF kuota dawa fulani hujawahi kuisikia ila ndio mara yako ta kwanza katika ndoto then ukiuliza unaambiwa dawa kama hiyo ipo
Sasa ulimwengu wa uhalisia wako, acha huu wa asili, ulimwengu ambao energy yako inaishi daima, huo ulimwengu ni infinite, with infinite possibilities, knowledge n.k, tofauti ni attachement na utayari wa hiyo energy (ya kwako) kupokea hizo taarifa

Unachokiona ni ndoto ya kitu usichokijua na unakuja kukijua kwenye uhalisia, ni energy yako ilipokea hiyo taarifa katika realm ile, ikakuletea wewe (mwili), ukaiexperience in real time
 
Mkuu kuna watu wana maono kupitia ndoto.

1.Kuna mtu usiku aliota ndugu yake kapata ajali na amepata majeraha na damu zinamchuruzika ,asubuhi akapewa taarifa ndugu yake kapata ajali na aliumia sana.
Ulihakikisha vipi na ulithibitishaje kwamba kweli huyo mtu aliota?

Ulikuwa kwenye akili yake usiku huo kuthibitisha ndoto hiyo?

Maana kweli ndugu yake anaweza kuwa alipata ajali.

Lakini je, Utahakikisha vipi na ulithibitishaje kwamba kabla ya ndugu huyo kupata ajali, kuna mtu aliota kweli?

Hiyo ndoto ya kupata ajali uliwezaje kuithibitisha kwamba kweli iliotwa kabla ya ajali?
2.Kuna siku aliota msiba wa mtu wake wa karibu upande wa ushemejini na huyo mtu alikuwa haumwi wala nini lakini baada ya siku kadhaa week 3 -4 akasikia huyo mtu amekata MOTO.
Halafu habari au stori inayoanza na "kuna siku" kuna mtu" au "kuna jamaa"

Zinakuwaga ni stori za kutunga na wala hazina uthibitisho.

Kwa sababu, Tutahakikisha vipi kwamba habari hiyo ni kweli ilitokea?

Tutathibitishaje kwamba huyo mtu ni kweli aliota?

Tutahakikisha vipi tarehe ya mtu kuota na tarehe ya mtu kufa kama zina endana na kufuatana?
Baada ya hayo matukio wazee ikabidi wamuweke chini kwamba akiota kitu kibaya basi aamke na akemee.

Zipo kweli ndoto zinazotokana na kuwaza kitu kwa sana ila kuna nyingine ni ufunuo(maono).
Kuota kupo sikatai.

Lakini kuota tu, hakufanyi jambo fulani litokee kweli kwa sababu linaweza lisitokee ingawa uliota.

Hivyo kuota sio guarantee ya moja kwa moja ya kwamba jambo fulani litatokea.

Na hata jambo likitokea, Si kwa sababu ya kuotwa, Kwa sababu lingeweza lisitokee licha ya kwamba liliotwa kabla.
 
Ndoto za maono, ni ndoto za hatma. Hizi mara nyingi huwa metaphoric, haziji na sura za watu unaofahamu na mara nyingi kama sio mara zote, haziji na tafsiri ya moja kwa
Ni nani huyo anakuwa na mamlaka ya kutafsiri hilo fumbo?

Mungu au ulimwengu unatumia lugha ya mafumbo ili kutupa hatma zetu kwa sababu gani?

Kama hatma ni kitu muhimu cha kuokolewa au kujiandaa, kwa nini ujumbe wake hauji kwa uwazi?
 
Sasa ulimwengu wa uhalisia wako, acha huu wa asili, ulimwengu ambao energy yako inaishi daima, huo ulimwengu ni infinite, with infinite possibilities, knowledge n.k, tofauti ni attachement na utayari wa hiyo energy (ya kwako) kupokea hizo taarifa

Unachokiona ni ndoto ya kitu usichokijua na unakuja kukijua kwenye uhalisia, ni energy yako ilipokea hiyo taarifa katika realm ile, ikakuletea wewe (mwili), ukaiexperience in real time
Energy yangu inawezaje kua tayali kupokea hizo taarifa
 
Ndoto ni mkusanyiko wa mawazo yetu.

Kuna namna fulani tunayaona mambo, tunayasikia, tunayafahamu, bila kuyapa umuhimu, halafu nawazo hayo yanaingia katika subconscious minds zetu, halafu tunayaota, halafu yanakamilika, halafu tunashangaa hili jambo nimeliota, halafu likatokea.

Kumbe liliingia mawazoni kwa kusikia, kuwaza, kuona kwa namna fulani, ambako hatukukupa umuhimu.

Ndiyo unaweza kukuta mtu anatembea, akausikia wimbo fulani redioni, bila ya mawazo yake kujua kikamilifu kuwa kausikia huo wimbo, akausikia tu kwa subconscious mind. Halafu akaanza kupiga mluzi wa huo wimbo, halafu sasa akapata nafasi ya kuusikia vizuri huo wimbo akatambua kuwa huo wimbo imekuwaje aanze kupiga mluzi wake tu, halafu hapo hapo wimbo uwe unapigwa redioni?

Kumbe hapo alianza kuusikia wimbo bila kujua kausikia (subconscious mind), akapiga mluzi wa huo wimbo kutoka subconscious mind, halafu ndiyo akausikia vizuri kutoka redioni.

Asipoelewa hapo anaweza kufikiri ana nguvu za kutabiri wimbo utakaopigwa redioni.

Hivyo hivyo, mfano una mzee wako yuko mbali anaumwa, familia inamuongelea sana, unaweza kufikiri huyu mzee hana muda mrefu wa kuishi, ukaota ndoto amefariki, lakini hata usiikumbuke ile ndoto.

Ila, ukiota ndoto kafariki, halafu kesho yake akafariki kweli, utaikumbuka tu ile ndoto.
Mkuu, tunaongelea vitu ambayo huvifahamu kabisaa yaani hujawahi hata kuvisikia halafu uviote halafu viwe kweli. Mfano ,kuna mahali niliwahi kufanya kazi,boss wetu alikuwa mzee,kumbe boss wetu bibi yake yupo hai ingawa sisi tulijua kwa umri wake boss wetu hana bibi wala babu. Siku moja mfanyakazi mwenzangu akaja kunambia ameota boss kafiwa tena akamtaja kabisa kafiwa na bibi, nikamcheka nikamwambia wewe unaona huo umri bibi wa boss atakuwa hai? Yeye mwenyewe akasema ile ndoto itakuwa uongo maana boss hawezi kuwa na bibi na hajawahi kumtaja bibi yake kwenye maongezi. Pia kipindi hicho boss alikuwa hajaonana na sisi kwa muda mrefu kutokana na kubanwa na majukumu mengine kwahiyo alikuwa hajatupa update yoyote inayohusu maisha yake. Baadae tunaletewa taarifa bibi yake boss kadondoka kafariki nyumbani, watu wakaanza kushangaa kumbe bibi yake boss bado alikuwa hai? Mimi na mwenzangu tukatazamana tu tukashangaa ndoto imekuwa kweli. Scenario kama hii ndo tunajiuliza inaletwa na nini?
 
Unajua kipofu,kiziwi nao wanaota ndoto?
akili ndo inatengeneza mambo yote hayo

Ndo maana ni kazi kutofautisha ndoto na maisha halisi
Inawezekana hata nakujibu hapa nipo ndotoni

Kwenye ndoto tunapambana kama vile tupo kwenye maisha halisi
So ipi ni ndoto na ipi ni halisi?
Mimi naamini nikifa ntazinduka ndotoni!
Na kwa nini ndoto iwe na sheria ambazo hauwezi kuzivunja ukitaka?
 
Ndoto ni mkusanyiko wa mawazo yetu.

Kuna namna fulani tunayaona mambo, tunayasikia, tunayafahamu, bila kuyapa umuhimu, halafu nawazo hayo yanaingia katika subconscious minds zetu, halafu tunayaota, halafu yanakamilika, halafu tunashangaa hili jambo nimeliota, halafu likatokea.

Kumbe liliingia mawazoni kwa kusikia, kuwaza, kuona kwa namna fulani, ambako hatukukupa umuhimu.

Ndiyo unaweza kukuta mtu anatembea, akausikia wimbo fulani redioni, bila ya mawazo yake kujua kikamilifu kuwa kausikia huo wimbo, akausikia tu kwa subconscious mind. Halafu akaanza kupiga mluzi wa huo wimbo, halafu sasa akapata nafasi ya kuusikia vizuri huo wimbo akatambua kuwa huo wimbo imekuwaje aanze kupiga mluzi wake tu, halafu hapo hapo wimbo uwe unapigwa redioni?

Kumbe hapo alianza kuusikia wimbo bila kujua kausikia (subconscious mind), akapiga mluzi wa huo wimbo kutoka subconscious mind, halafu ndiyo akausikia vizuri kutoka redioni.

Asipoelewa hapo anaweza kufikiri ana nguvu za kutabiri wimbo utakaopigwa redioni.

Hivyo hivyo, mfano una mzee wako yuko mbali anaumwa, familia inamuongelea sana, unaweza kufikiri huyu mzee hana muda mrefu wa kuishi, ukaota ndoto amefariki, lakini hata usiikumbuke ile ndoto.

Ila, ukiota ndoto kafariki, halafu kesho yake akafariki kweli, utaikumbuka tu ile ndoto.
Naishiwa power aisee ngoja kwanza nikae pembeni nisome
 
Mkuu, tunaongelea vitu ambayo huvifahamu kabisaa yaani hujawahi hata kuvisikia halafu uviote halafu viwe kweli. Mfano ,kuna mahali niliwahi kufanya kazi,boss wetu alikuwa mzee,kumbe boss wetu bibi yake yupo hai ingawa sisi tulijua kwa umri wake boss wetu hana bibi wala babu. Siku moja mfanyakazi mwenzangu akaja kunambia ameota boss kafiwa tena akamtaja kabisa kafiwa na bibi, nikamcheka nikamwambia wewe unaona huo umri bibi wa boss atakuwa hai? Yeye mwenyewe akasema ile ndoto itakuwa uongo maana boss hawezi kuwa na bibi na hajawahi kumtaja bibi yake kwenye maongezi. Pia kipindi hicho boss alikuwa hajaonana na sisi kwa muda mrefu kutokana na kubanwa na majukumu mengine kwahiyo alikuwa hajatupa update yoyote inayohusu maisha yake. Baadae tunaletewa taarifa bibi yake boss kadondoka kafariki nyumbani, watu wakaanza kushangaa kumbe bibi yake boss bado yupo hai? Mimi na mwenzangu tukatazamana tu tukashangaa ndoto imekuwa kweli. Scenario kama hii ndo tunajiuliza inaletwa na nini?
Imagine scenario kama hiyo inaonekana ya kawaida kweli 🤔
 
Haya majibu ni mepesi jamani hivi huoni tofauti wa mifano yako na mada yenyewe?
Kitu chochote kinaweza kutokea mbele.

Hivyo kuota kitu fulani kitatokea mbele, halafu kweli kikatokea mbele, Wala Si ajabu.

Kwa sababu chochote kinaweza kutokea mbele.

Au kuna vitu unavijua vilitokea zamani tu, haviwezi kutokea mbele?

Maana kiini cha mada yako kinahusu kuota kitu kabla, halafu kitokee mbele.

Na mimi nakwambia uote, Usiote. Kitu chochote kile kinaweza kutokea mbele.
 
Asante sana kwa maoni yako kaka🙏
 
Ni nani huyo anakuwa na mamlaka ya kutafsiri hilo fumbo?

Mungu au ulimwengu unatumia lugha ya mafumbo ili kutupa hatma zetu kwa sababu gani?

Kama hatma ni kitu muhimu cha kuokolewa au kujiandaa, kwa nini ujumbe wake hauji kwa uwazi?
Swali zuri
Wewe ni muumini wa uwepo wa muumba? Kwa imani yoyote ile
 
Sasa ulimwengu wa uhalisia wako, acha huu wa asili, ulimwengu ambao energy yako inaishi daima, huo ulimwengu ni infinite, with infinite possibilities, knowledge n.k, tofauti ni attachement na utayari wa hiyo energy (ya kwako) kupokea hizo taarifa

Unachokiona ni ndoto ya kitu usichokijua na unakuja kukijua kwenye uhalisia, ni energy yako ilipokea hiyo taarifa katika realm ile, ikakuletea wewe (mwili), ukaiexperience in real time
Kama energy yako inatoka kwenye ulimwengu wa infinite knowledge, kwa nini taarifa inayoingia kwenye mwili huu wenye mapungufu mara nyingi inakuja ikiwa imepotoshwa au imechanganyikana na bias za akili yako?

Kama chanzo ni infinite taarifa inapaswa kuwa kamili lakini unavyosema maono yanakuja kwa metaphor ina maana hiyo nishati inakutana na kikwazo, sasa hauoni kwamba tunapopokea hizi taarifa tunachokiona siyo ukweli wa ulimwengu wa nishati bali ni tafsiri ya akili zetu tu?
 
Back
Top Bottom