Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Leo usiku nimeota ndoto hii.
Kuna eneo lilikuwa limewekewa uzio kama zizi,mimi nikafungua mlango wa hilo kama zizi nikafungua zipo nikakojoa huki nimeacha mlango wa hilo eneo wazi ghafla nikasikia hicho kimulango kinafungwa na mbele yangu nikakutana na simba.

Huyo simba akanibeba kwa mdomo wake kishaa akatoka nje na mimi,kwa mbele kulikuwa na watu wakawa wanaogopa kumpiga maana nipo kinywani mwake.Badaye hao jamaa waliosimama wakiangalia simba ameniweka mdomoni mwake bila kunidhulu wakawa wanashangaa,simba alikuwa ameniweka mdomoni kwake lakini analalamika hivyo wakaanza kumuangalia wakagundua alikuwa amejeruhiwa.

Wale jamaa wakaanza kumtibu yule simba huku bado mimi nikiwa mdomoni kwake,walipomaliza kumtibia lile jeraha yule simba akanitema chini nikiwa mzima kisha akaondoka kurudi kwenye lile zizi.Vile amenitema tu chini ndio nikashikuta kutoka usingizini

Dah hiyo ndoto sijaisahau hadi sasa hivi,yani hata sijui ina maana gani.
Hapa hata sijui mkuu ngoja nikuitie huyu mshana Jr
 
Katika information theory taarifa yoyote inayotoka kwenye source kuelekea kwa receiver inapaswa kuwa na mfumo wa error correction.

Kama chanzo ni infinite na kamilifu, lakini mpokeaji ambaye ni binadamu ni finite na mwenye udhaifu, hauoni kama ni wajibu wa hicho chanzo kuhakikisha ujumbe unafika kwa usahihi?

Kama ujumbe unafika kwa metaphor ambayo kila binadamu anaitafsiri tofauti, basi huo mfumo wa mawasiliano una low signal to noise ratio.

Yani mfumo wa kutuma taarifa ni wa kimaajabuajabu halafu unaona tatizo lipo kwa mpokeaji?
Unarelate vizuri sana. Unahitaji kuongeza maarifa kidogo tuu. Theory ulizojifunza ni kwa ulimwengu halisi, huu unaouona. Ninachozungumzia mimi ni cha ulimwengu asilia

Binadamu (finite) ndio pungufu, amelemaa au kulemazwa na ulimwengu halisi. Mtu on the other hand ni infinite katika ulimwengu asilia, huyu anapokea kama ilivyo. Na kutoka huko, taarifa haina hizo noise ratio, hizo zipo huku kwenye masikio ya nje.
 
Unarelate vizuri sana. Unahitaji kuongeza maarifa kidogo tuu. Theory ulizojifunza ni kwa ulimwengu halisi, huu unaouona. Ninachozungumzia mimi ni cha ulimwengu asilia

Binadamu (finite) ndio pungufu, amelemaa au kulemazwa na ulimwengu halisi. Mtu on the other hand ni infinite katika ulimwengu asilia, huyu anapokea kama ilivyo. Na kutoka huko, taarifa haina hizo noise ratio, hizo zipo huku kwenye masikio ya nje.
Unaweza kutofautisha kati ya taarifa kamilifu kutoka ulimwengu asilia na hyper imagination?
 
Kuna swali huwa ninalojiuliza sana peke yangu, naomba nishare hapa

Utasikia watu wakisema ulimwengu wa roho, ulimwengu wa siri. Hivi huo ulimwengu huwa ni upi?

Je, mambo ya ulimwengu wa roho au ulimwengu wa siri huwa ni pamoja na ndoto tunazoota usiku au mchana?
Au tuseme ndoto huwa ni dunia au ulimwengu mwingine?

Kwa sababu unapoota ndoto huwa ni kama upo kwenye ulimwengu au dunia nyingine. Maana unakuwa umelala, lakini ni kama bado kuna mambo yanaendelea kwenye akili yako

Wengine husema ndoto huwa ni matokeo ya mawazo, msongo wa mawazo uliozidi, maongezi au vitendo vya muda fulani

Ndiyo huwa ubongo unakuwa kama unarudi kwenye yale mambo

Mimi binafsi nakiri kuna ndoto zingine mtu huota huwa ni matokeo ya mawazo, shughuli za kutwa nzima au kile akili inachowaza au inachokitamani kifanyike

Unajikuta ukiota hivyo, na unapoamka unajua kabisa hizi ni fikra za mchana kutwa na mawazo tu

Au kuota mambo ya zamani, mfano shule, marafiki wa utotoni n.k. Na hii ya shule wengi wanasema wameota, ila mimi sijawahi kuota kabisa ndoto ya shule

Ninakuwa tu na ndoto zangu kivyangu, ambazo sioni hata watu wakizizungumzia

Swali linakuja kwenye ndoto ambazo nitaziita prophetic dreams, kwa sababu ni ndoto unaota kitu kitakachotokea mbele

Nasisitiza, kitu kitakachotokea mbele. Unakuta siku moja kabla au siku mbili kabla

Hii inanifanya nawaza sana, hivi huwa ni kitu gani kinatokea?

Yaani unaota ndoto kuhusu kitu fulani, halafu kikitokea unakuwa shocked 😲

Ukimwambia mtu haamini, anaona ni uongo, kama unapenda kujifanya special

Hivyo unabaki nayo mwenyewe

Pia kuna mtu ana uwezo wa kusoma mtu anachokiwaza

Yaani mfano ukiwa unachat na mtu unaweza ukawa unahisi huyu fulani ana nia fulani, aidha ana chuki fulani dhidi yangu, japo anaweza kuwa anapretend love

Na kweli hatachukua muda mrefu anajifunua rangi zake halisi

Lakini point kubwa hapa ni, inakuaje mtu anaota mambo yajayo? Ni nini huwa kinatokea??

Au huo ndio huitwa ulimwengu wa roho au wa siri?

Nitatoa mfano. Kuna ndoto niliota kuhusu watu fulani

Hao watu sikuwahi kuwajua kabla na hakuna namna ningewajua
Ila ajabu, hiyo ndoto niliyoota na majina yao kwenye ndoto, nilivyokuja kufahamu baadaye ilikuwa the same names

Yaani hata kama ningemwambia mtu asingeelewa, angesema nataka sifa

Niliwahi kuishi na mtu fulani
Huyo nilikuwa namwambia sana, Nimeona hivi katika ndoto kuhusu wewe,na kweli baada ya siku anakutana na situation kama hizo

Akawa ananiuliza, Wewe ni mganga au mchawi?😢😂

Ni mambo mengine mengi, ila hayo machache yanaeleweka

Je, kuna wengine wapo hivi?

Huota mambo halisi kabisa?

Nini sababu?

Faida au hasara?

Welcome Guy's
ShesRise_1 🤚
samahani lakini ndugu mdau,
kabla sijachangia hoja mahususi mezani,

ningependa kufahamu au kujua kitu kimoja au viwili kutoka kwako,

Je,
kwenye ukoo wenu kuna habari au mambo ya uchawi au ushirikina?

Na je,
kwenye ukoo wenu kuna historia ya masuala ya kiimani, mathalani babu wa mababu zako walikua viongozi wafia dini au watu wa dini sanaaaa?🐒
 
samahani lakini ndugu mdau,
kabla sijachangia hoja mahususi mezani,

ningependa kufahamu au kujua kitu kimoja au viwili kutoka kwako,

Je,
kwenye ukoo wenu kuna habari za uchawi au ushirikina?
Sikuona issue za kichawi wala ushirikina kabisa
Na je,
kwenye ukoo wenu kuna historia ya masuala ya kiimani, mathalani babu wa mababu zako walikua viongozi au watu wa dini sanaaaa?🐒
Familia Muslim sana ile ya kufunika mpka uso kwa niqab kuvaa hijab swala 5

But nili escape nikaenda ukristo
Mpaka now nipo huko japo nako 🤔
Anyway karibuu
 
Sikuona issue za kichawi wala ushirikina kabisa

Familia Muslim sana ile ya kufunika mpka uso kwa niqab kuvaa hijab swala 5

But nili escape nikaenda ukristo
Mpaka now nipo huko japo nako 🤔
Anyway karibuu
Asante sana nakushukuru,

na kwa msingi huo,
hatimae sasa naweza kuchangia hoja mahususi mezani 🐒
 
Back
Top Bottom