Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Kuna swali huwa ninalojiuliza sana peke yangu, naomba nishare hapa

Utasikia watu wakisema ulimwengu wa roho, ulimwengu wa siri. Hivi huo ulimwengu huwa ni upi?

Je, mambo ya ulimwengu wa roho au ulimwengu wa siri huwa ni pamoja na ndoto tunazoota usiku au mchana?
Au tuseme ndoto huwa ni dunia au ulimwengu mwingine?

Kwa sababu unapoota ndoto huwa ni kama upo kwenye ulimwengu au dunia nyingine. Maana unakuwa umelala, lakini ni kama bado kuna mambo yanaendelea kwenye akili yako

Wengine husema ndoto huwa ni matokeo ya mawazo, msongo wa mawazo uliozidi, maongezi au vitendo vya muda fulani

Ndiyo huwa ubongo unakuwa kama unarudi kwenye yale mambo

Mimi binafsi nakiri kuna ndoto zingine mtu huota huwa ni matokeo ya mawazo, shughuli za kutwa nzima au kile akili inachowaza au inachokitamani kifanyike

Unajikuta ukiota hivyo, na unapoamka unajua kabisa hizi ni fikra za mchana kutwa na mawazo tu

Au kuota mambo ya zamani, mfano shule, marafiki wa utotoni n.k. Na hii ya shule wengi wanasema wameota, ila mimi sijawahi kuota kabisa ndoto ya shule

Ninakuwa tu na ndoto zangu kivyangu, ambazo sioni hata watu wakizizungumzia

Swali linakuja kwenye ndoto ambazo nitaziita prophetic dreams, kwa sababu ni ndoto unaota kitu kitakachotokea mbele

Nasisitiza, kitu kitakachotokea mbele. Unakuta siku moja kabla au siku mbili kabla

Hii inanifanya nawaza sana, hivi huwa ni kitu gani kinatokea?

Yaani unaota ndoto kuhusu kitu fulani, halafu kikitokea unakuwa shocked 😲

Ukimwambia mtu haamini, anaona ni uongo, kama unapenda kujifanya special

Hivyo unabaki nayo mwenyewe

Pia kuna mtu ana uwezo wa kusoma mtu anachokiwaza

Yaani mfano ukiwa unachat na mtu unaweza ukawa unahisi huyu fulani ana nia fulani, aidha ana chuki fulani dhidi yangu, japo anaweza kuwa anapretend love

Na kweli hatachukua muda mrefu anajifunua rangi zake halisi

Lakini point kubwa hapa ni, inakuaje mtu anaota mambo yajayo? Ni nini huwa kinatokea??

Au huo ndio huitwa ulimwengu wa roho au wa siri?

Nitatoa mfano. Kuna ndoto niliota kuhusu watu fulani

Hao watu sikuwahi kuwajua kabla na hakuna namna ningewajua
Ila ajabu, hiyo ndoto niliyoota na majina yao kwenye ndoto, nilivyokuja kufahamu baadaye ilikuwa the same names

Yaani hata kama ningemwambia mtu asingeelewa, angesema nataka sifa

Niliwahi kuishi na mtu fulani
Huyo nilikuwa namwambia sana, Nimeona hivi katika ndoto kuhusu wewe,na kweli baada ya siku anakutana na situation kama hizo

Akawa ananiuliza, Wewe ni mganga au mchawi?😢😂

Ni mambo mengine mengi, ila hayo machache yanaeleweka

Je, kuna wengine wapo hivi?

Huota mambo halisi kabisa?

Nini sababu?

Faida au hasara?

Welcome Guy's
ShesRise_1 🤚
Ajabu ni kwamba ndoto huja na picha kamili. Nani anatengeneza
 
Kaka umeeleza vizuri mnoo utafiti zaidi unaitajika

shukrani mnoo

Kama kuna vingine vya kuongeza ongeza namatani kujua zaidi
Kuna njia ya kufungua mlango wa mwili wa fahamu je unazifahamu?
Kama unazifahamu tunaomba utupe somo namna ya kuzifungua!!
 
Back
Top Bottom