King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,227
- 98,761
Sawa mkuu ila kuna watu wana maono ,kuna watu wamebarikiwa kuona mambo ya mbele....zamani tulikuwa tunawaita manabii ,walikuwa wanatokewa live na kuambiwa ila kwasasa wanatokewa kupitia ndoto.Ulihakikisha vipi na ulithibitishaje kwamba kweli huyo mtu aliota?
Ulikuwa kwenye akili yake usiku huo kuthibitisha ndoto hiyo?
Maana kweli ndugu yake anaweza kuwa alipata ajali.
Lakini je, Utahakikisha vipi na ulithibitishaje kwamba kabla ya ndugu huyo kupata ajali, kuna mtu aliota kweli?
Hiyo ndoto ya kupata ajali uliwezaje kuithibitisha kwamba kweli iliotwa kabla ya ajali?
Halafu habari au stori inayoanza na "kuna siku" kuna mtu" au "kuna jamaa"
Zinakuwaga ni stori za kutunga na wala hazina uthibitisho.
Kwa sababu, Tutahakikisha vipi kwamba habari hiyo ni kweli ilitokea?
Tutathibitishaje kwamba huyo mtu ni kweli aliota?
Tutahakikisha vipi tarehe ya mtu kuota na tarehe ya mtu kufa kama zina endana na kufuatana?
Kuota kupo sikatai.
Lakini kuota tu, hakufanyi jambo fulani litokee kweli kwa sababu linaweza lisitokee ingawa uliota.
Hivyo kuota sio guarantee ya moja kwa moja ya kwamba jambo fulani litatokea.
Na hata jambo likitokea, Si kwa sababu ya kuotwa, Kwa sababu lingeweza lisitokee licha ya kwamba liliotwa kabla.
Sasa mtu aongope ili iweje kuhusu kuota ndoto ya ndugu yake kufa au kupata ajali? Mbona ajali au vifo vimetokea kwenye hiyo familia lakini hakusema hii nilioteshwa?
Mambo ya kiroho yanahitaji imani ,kama hauna imani hauwezi kuamini mpaka ushuhudie wewe na wewe uliyoshuhudia ukija kutuadithie siye hatutakuamini pia tutaona uongo.