Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Je, Ndoto Zinazoonyesha Mambo Yajayo Ni Kazi ya Ubongo au Ulimwengu wa Roho?

Kama energy yako inatoka kwenye ulimwengu wa Infinite knowledge, kwa nini taarifa inayoingia kwenye mwili huu wenye mapungufu mara nyingi inakuja ikiwa imepotoshwa au imechanganyikana na bias za akili yako?

Kama chanzo ni infinite taarifa inapaswa kuwa kamili lakini unavyosema maono yanakuja kwa metaphor ina maana hiyo nishati inakutana na kikwazo, sasa hauoni kwamba tunapopokea hizi taarifa tunachokiona siyo ukweli wa ulimwengu wa nishati bali ni tafsiri ya akili zetu tu?
Kinachofanya uione taarifa hiyo iwe bias, au ina mapungufu ni mkao wako na udhaifu wako katika kuelewa tafsiri. Huwa haiji nusunusu.
 
Nashukuru sana umenielewa ila kuhusu mambo ya nabii sijui kuhusu hayo

Ila ni kweli mara nyingi hua naona baadhi ya mambo kabla hayajatokea ila kwa kua mtu hukumwambia kabla haamini anaona unajikweza

Nb siwezi kusema kila kitu ila swali langu lilikua nini hua kinatokea mpka unapata ndoto halisi
Ungesoma vizuri nilichokiandika ungenielewa
 
Kwenye kumbukumbu ya MV Bukoba mwaka huu kuna member alisema dada yake aliota kuhusu ajali ile kabla na akaandika kwenye diary. Ile diary baba yake alivyoenda kwenye graduation yake Rugambwa Girls alirudi nayo pamoja na mizigo iliyotangulia. Bahati mbaya yule dada alifariki kwenye ile ajali,baadae kuangalia kwenye vitu vyake ndo wanakutana na ile diary inaelezea ajali. Kama hapo chanzo cha huyo dada kuota kuhusu ajali ni nini ndo swali gumu.
Nani alithibitisha huyo dada aliota kweli hiyo ndoto?

Kuna mtu alikuwa ndotoni pamoja na huyo dada akahakikisha kweli meli inayootwa ni meli ya MV BUKOBA?
 
Nijibu nitakujibu, suala hapa siyo kujua mimi ni muumini au siyo.

Nitakavyo wasilisha hoja yangu itakuwa jibu tosha kwako kuhusu imani yangu.
Nimekuuliza ili nijue nakujibu kama muumini ( njia rahisi kwako kuelewa) au nikujibu kwa science ya akili, ambayo inakutaka uwe unaelewa nini ni UNIVERSE.
 
Haya maswala bwana kuna muda yanahitaji uelewa, uelewa unapofikia mwisho wake, ni kuamini tu tutapata fahamu mbele kwa mbele.
Fatilia kama mimi huenda tutaongezea kwa pale tunapopafahamu
 
Haya maswala bwana kuna muda yanahitaji uelewa, uelewa unapofikia mwisho wake, ni kuamini tu tutapata fahamu mbele kwa mbele.
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa utahakikisha vipi unachokiamini ni ukweli na si uongo?

Hapo ndipo kazi inapoanzia.
 
Kinachofanya uione taarifa hiyo iwe bias, au ina mapungufu ni mkao wako na udhaifu wako katika kuelewa tafsiri. Huwa haiji nusunusu.
Katika information theory taarifa yoyote inayotoka kwenye source kuelekea kwa receiver inapaswa kuwa na mfumo wa error correction.

Kama chanzo ni infinite na kamilifu, lakini mpokeaji ambaye ni binadamu ni finite na mwenye udhaifu, hauoni kama ni wajibu wa hicho chanzo kuhakikisha ujumbe unafika kwa usahihi?

Kama ujumbe unafika kwa metaphor ambayo kila binadamu anaitafsiri tofauti, basi huo mfumo wa mawasiliano una low signal to noise ratio.

Yani mfumo wa kutuma taarifa ni wa kimaajabuajabu halafu unaona tatizo lipo kwa mpokeaji?
 
Nani alithibitisha huyo dada aliota kweli hiyo ndoto?

Kuna mtu alikuwa ndotoni pamoja na huyo dada akahakikisha kweli meli inayootwa ni meli ya MV BUKOBA?
Mkuu, dada aliandika kwenye diary huo ndo uthibitisho, kama aliyesema hayo maneno alitudanganya mimi siwezi kusema kama alitudanganya au lah, labda kama wewe unaweza kuthibitisha utusaidie.
 
Leo usiku nimeota ndoto hii.
Kuna eneo lilikuwa limewekewa uzio kama zizi,mimi nikafungua mlango wa hilo kama zizi nikafungua zipo nikakojoa huki nimeacha mlango wa hilo eneo wazi ghafla nikasikia hicho kimulango kinafungwa na mbele yangu nikakutana na simba.

Huyo simba akanibeba kwa mdomo wake kishaa akatoka nje na mimi,kwa mbele kulikuwa na watu wakawa wanaogopa kumpiga maana nipo kinywani mwake.Badaye hao jamaa waliosimama wakiangalia simba ameniweka mdomoni mwake bila kunidhulu wakawa wanashangaa,simba alikuwa ameniweka mdomoni kwake lakini analalamika hivyo wakaanza kumuangalia wakagundua alikuwa amejeruhiwa.

Wale jamaa wakaanza kumtibu yule simba huku bado mimi nikiwa mdomoni kwake,walipomaliza kumtibia lile jeraha yule simba akanitema chini nikiwa mzima kisha akaondoka kurudi kwenye lile zizi.Vile amenitema tu chini ndio nikashikuta kutoka usingizini

Dah hiyo ndoto sijaisahau hadi sasa hivi,yani hata sijui ina maana gani.
 
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa utahakikisha vipi unachokiamini ni ukweli na si uongo?

Hapo ndipo kazi inapoanzia.
Ndiyo maana imani hufika tamati tu pale linapotukia jambo, pia kujulikana kuwa ni uongo ni muda wa jambo hilo lisipotokea, lakini maswala ya imani ni magumu kidogo
 
Mkuu, dada aliandika kwenye diary huo ndo uthibitisho, kama aliyesema hayo maneno alitudanganya mimi siwezi kusema kama alitudanganya au lah, labda kama wewe unaweza kuthibitisha utusaidie.
Kama huwezi kusema ulidanganywa au lah, Sasa ulihakikisha vipi kwamba ni ukweli?

Maana ukweli unataka proofs zenye verification.
 
Back
Top Bottom